Mkuu Jmushi1,Mtanzania huyu ni mkuu Mwakalelei,Mkuu Mwanjelwa kapotea kiaina.
Mh alisema lorry lilikua mbele yake na driver akawaruhusu ku overtake lakini wakati wamepita trailer ya nyuma yule driver wa lorry aka swing kichwa kutaka kuwagonga. Driver wa Mh akaongeza mwendo kukwepa lakini driver wa lorry akawagonga kidogo nyuma kumfanya driver wa Mh akose mwelekeo na ku overturn. Coaster lilikua linakuja kwambali mbele.Mr Mwakyembe explained that a lorry was overtaking his car and suddenly a minibus appeared on the opposite direction.
That is when my driver decided to accelerate so that he could allow the lorry to go back. But the lorry kept on accelerating as well and knocked my car from the back causing it to lose direction before knocking a tree and overturned, he said.
Gari ya Mh Mwakyembe ilikuwa katika mwendo wa kasi.
Dereva wa mwakyembe hakufanya maamuzi sahihi, kitendo chake cha kuongeza mwendo kingeweza kusababisha lorry kugongana na basi la abiria.
Kwa mantiki hiyo basi, inawezekana dereva wa lorry alipoona kuwa gari la Mwakyembe linaongeza mwendo njia sahihi ya kuepusha ajali na basi ni kuilazimisha land cruiser isalimu amri.
Huo uamuzi una hasara na faida zake, kwa hiyo tunaweza kuangalia ni zipi hasara na je zipi ni faida.
Bottom line kama lorry tayari lilikuwa limeruhusiwa kuipita gari ya mheshimiwa basi hakukuwa na sababu za dereva wa mheshimiwa kuongeza mwendo.
Mwakyembe harogeki au ule unga wa Vijisenti bungeni ungemumalizaWote mnakosea! habari za uhakika kabisa ni kuwa Dr Mwakyembe karogwa na kundi la mafisadi RA, EL, nk
...ya nini hiyo, hujiamini au huamini ulichoandika?
Unataka nikuaminishe?
- au?
Mtanzania,
Hakika hatuwezi kusingizia barabara kuwa sababu ya ajali zetu ikiwa sisi wenyewe ndio wajenzi wa hizi barabara..Ni miaka mingapi sasa hivi toka nisikie barabara ya Mbeya - Dar inawaondoa watu kila siku kwa ajali!. Zamani ilikuwa barabara ya kati na hasa pale Sekenke. Huwezi kuamini watu tulikuwa tukiomba Mungu pindi bus linapokaribia eneo hilo..Why? kuyaweka maisha yake mikononi mwa Mungu mahala ambapo sisi wenyewe ndio jukumu letu kuhakikisha usalama. Mbali na yote haya ya Usalama barabara ni kiungo kikubwa sana cha Uchumi wa nchi. Tunasahau kwamba barabara ile Ya Dar Mbeya ilipotengenezwa misafara yote ya magari ya mizigo kwenda Zambia, Zimbabwe na Zaire (Kongo) yaliitumia barabara hiyo na kulikuwepo na ongezeko kubwa sana ktk uchumi wetu enzi hizo..
Tofauti na wenzetu Ulaya, nchi za Kiafrika bado zinashindwa kuelewa mfumo mzima wa Ubepari na hasa ktk ukupanga vipaumbele. Sisi tunajenga miundombinu kwa sababu tofauti kabisa, yaani barabara ya Iringa itajengwa au kuimarishwa kwa sababu ya vifo au ajali zinazotokea na hasara kubwa kwetu ni kupoteza maisha ya watu. Wakati hawa wenzetu Miundombinu hutazama kwanza Uchumi wa nchi na uzalishaji wake, safety ni kipengele kinachoingia ktk ujenzi sii sababu ya Ujenzi wa Muundombinu. Ndio maana siku zote tuko nyuma kaatika mambo mengi kwa sababu hadi mtu afe au malalamiko ya watu ndipo tunapoanza kufikiria ulazima wa kuboresha Miundombinu ili kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi wake. Uchumi unafuatia mahitaji ya watu.. sii kutangulia mahitaji hayo.
Barabara nzuri moja kwa moja hupunguza ajali na kinachotisha zaidi ni kwamba bado tuna tumia elimu ya Kijamaa ktk mambo mengi sana..Tunafikiria Kuboresha maisha ya mananchi pasipo kuboresha Uchumi, yaani ujenzi wa miundombinu itazame kwanza safety na ubora wa vitu hivyo ktk matumizi ya wananchi wake badala ya kutazama vitu hivyo ktk kuboresha Uchumi wa nchi. Ni mara zote nchi zenye Uchumi bora, xenye Miundombinu bora, maisha ya wananchi wake kuboreka zaidi!..Hata hizo kero za wananchi mara nyingi zinahusu huduma na mahitaji yao wao binafsi na sii mahitaji ya vianzio vya kukuza uchumi na kuongoeza ajira ktk mazingira yao.
Mtanzania usijali mkuu nitakushirikisha vingi katika hii shughuli ya consultancy services ni mambo ya technical evaluation za mambo ya barabara na madaraja, design za water supply, design and supervision of civil works( barabara, madaraja na maji) pamoja na design and supervision of building works abazo zinahusika zaidi na majengo, mambo ya test za udongo( geotechnical investigation) na masuala mengine yanayohusiana na mambo ya consultancy katika mambo ya ujenzi(preparation of contract document and tender document). Ndugu yangu nitakuhabarisha zaidi nikirudi tz mwanzoni mwa mwezi ujao.Mkuu Mwakaleli,
Nimependa hii ya consultancy services vijijini. Kama unaweza naomba niandikie zaidi kidogo hata kupitia PM yangu juu ya zina include vitu gani? Huenda kuna mambo ambayo unafanya ambayo na wengine tunaweza kujifunza/kufaidika au kusaidiana. Kuna mambo mengi sana huko vijijini yakifanywa inavyotakiwa, kuna weza kuwa na impact kubwa kwa wananchi wa kawaida.
Kazi njema.
...Hiyo barabara ya Iringa Mbeya kidogo mimi iniweke chini. Kuna dereva ambaye siku zote namtumia, alikuwa na tender nzuri zaidi, akaona kuiachia kwa safari za wiki mbili haitakuwa vizuri. Nikamwelewa na akanitafutia dereva mwingine; njiani nikawa namwambia hii barabara mbaya punguza mwendo. Akawa anapunguza kisha anarudi pale pale, ilifika mahali nikachoka na kumwacha. Ghafla mwendesha...
.......Sijui nini kifanyike lakini mimi nina wasiwasi kweli na hizo barabara zetu.
Ninachoshangaa ni jinsi watu wanavyozungumzia matatizo ya barabara na ubaya wake kana kwamba hao wanaotunga sheria, kusimamia fedha za umma na ambao wanakuja kwenye misiba ya wahanga wa ajali na kuwatembelea majeruhi, wao wanapita angani!
Mnachotegemea ni kuwa mkiimba wimbo mzuri, na kuongeza ala na vibwagizo basi mbuzi atacheza! kwenye suala la barabara na mambo ya ajali hakuna kipya ambacho hawakijui. NONE. Kwani mmeshasahau mwaka huu ulivyoanza?
Ndugu yangu barabara zetu nyingi, zilizojengwa zamani zile hazina standard zinazokubalika kwa sasa. design life ya barabara ya lami ni miaka ishirini pia inatakiwa iwe inapata matengenezo ya mara kwa mara lakini ni bahati mbaya hizi barabara zetu huwa hazifiki hiyo miaka ishirini kwa sababu hazipati matengenezo ya mara kwa mara. standard ya highway carriage way(sehemu ya kupita magari) inatakiwa iwe na upana wa mita saba nakila bega (shoulder) inatakiwa iwe na upana wa mita moja na nusu. lakini ukiangalia leo hii barabara ya Dar Mbeya hasa maeneo ya iringa hazo hizo shoulders hazionekani, mashimo kibao, corrugations na ruts ndiyo usiseme kabisa yaani ni hatari tupu. Hata design life ya hiyo barabara ilishapita muda mrefu na wanachofanya sasa hivi ni kuweka patch kibao ambazo pia zinachangia zaidi kuharibika kwa barabara.Mkuu Mtanzania,
Trust me barabara zetu nyingi, as they stand are MONSTERS ready to kill...any time kwa yeyote yule ambaye ni makini na ambao si makini...the reason behind being
1. Maintenance issues.........it wil be very lucky ku-find barabara inayo-receive timely mtce...na hata zinapo receive hizo mtce.......traffic management facities kwenye sehemu hizo HAKUNA.......imagine Mtce engineer ana-send crew yake ku-deal na let say potholes......wale vibarua watachimba chimba na kuacha lile shimo unattended....i.e without any traffic control measures......one would ask really....why would someone go there in the first place......to make things worse wakti mwingine wana-spray lami...yaani wee acha tu.....in shor tuna tatizo kubwa kwenye mtce
NOTE: mtce si kuziba mashimo peke yake, hata traffic sign posts inabidi ziwe replaced pale zinapokuwa vandalised....usiniulize utazuiaje vandalism.....lol
2. Nafikri Design zetu wakati mwingine zinatakiwa ziwe assessed baada ya kipindi fulani kuangalia kama zina-meet demands/requirements/standards/safety issues.........sina uhakika kama hayo mambo yanafanyika......nasema hivyo kwa sababu miji yetu siku hizi inakuwa haraka sana nahivyo travel parttens zinabadilika
3. Enforcement ni tatizo nalo.....pengine sheria zetu zinahitaji kuangaliwa upya........
4. Public awareness........ni hatua gani serikali inachukua kuelimisha wananchi juu ya matumizi bora na salama ya barabara
well nafikir Morani75 na Fundi Mchundo watakuw ana mengi ya kuelezea ju ya hilo
........si vibaya kuwakumbusha
ya nini? hujiamini, huamini ulichoandika, hujui matumizi ya hilo neno.
Ndugu yangu barabara zetu nyingi, zilizojengwa zamani zile hazina standard zinazokubalika kwa sasa. design life ya barabara ya lami ni miaka ishirini pia inatakiwa iwe inapata matengenezo ya mara kwa mara lakini ni bahati mbaya hizi barabara zetu huwa hazifiki hiyo miaka ishirini kwa sababu hazipati matengenezo ya mara kwa mara. standard ya highway carriage way(sehemu ya kupita magari) inatakiwa iwe na upana wa mita saba nakila bega (shoulder) inatakiwa iwe na upana wa mita moja na nusu. lakini ukiangalia leo hii barabara ya Dar Mbeya hasa maeneo ya iringa hazo hizo shoulders hazionekani, mashimo kibao, corrugations na ruts ndiyo usiseme kabisa yaani ni hatari tupu. Hata design life ya hiyo barabara ilishapita muda mrefu na wanachofanya sasa hivi ni kuweka patch kibao ambazo pia zinachangia zaidi kuharibika kwa barabara.
Barabara zetu nyingi design zake zinawabagua watembea kwa miguu na watumia baiskeli hakuna sehemu za kupita watu wa namna hiyo wakati nao kodi zao zinajenga hizi barabara, ambapo hilo ni tatizo kubwa inabidi tuzingatie pia route za watembea kwa miguu na wa baiskeli. ukienda moshi unaweza toa machozi. barabara inayokwenda KCM toka mjini haina shoulder kabisa mie huwa najiuliza hawa waliodesign hii barabara walikuwa wanafikiria nini sijui ,sasa hivi watu wanapita katikati ya barabara.
Pia barabara zetu nyingi hazina alama za barabarani ambazo zinasaidia kutoa tahadhari, wakati mwingine wananchi huzing'oa hizo alama na kwenda kujengea vyoo na kutengenezea mipini ya mashoka na majembe. watu wanaelimishwa sana lakini hawaelewi. wakati mwingiine hung'oa hata bomba za kwenye madaraja ambazo ni muhimu sana. yaani utafikiri watu tumelogwa yaani kazi ipo.