Ajali Ubungo Riverside


Ni uzembe wa Mambo ya ndani ambayo imeshindwa kabisa kuwadhibiti polisi ili wahakikishe sheria za barabarani zinafuatwa kila siku. Barabara zetu kusema kweli zinatisha sana. Ukitoka asubuhi na kurudi nyumbani jioni unashukuru Mungu, ukiwa safarini roho mkononi ukifika salama unabaki na wasiwasi kama safari ya kurudi itaisha salama. Nchi yetu imeoza hili siyo siri kila mahali pamejaa madudu tu.

Poleni sana wafiwa Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi~AMEN

Umesema ukweli mtupu mkuu,Geshi letu la Police na Macommissioner wake sijui kichwani mwao mna vitu gani,hakika ubongo nafikiri wanao ila hawako tayari kuutumia,tangu nikiwa mdogo naona geshi letu la polisi linafanya utafiti zaidi kuliko kuzui hizi ajali,Trafik wako bize na utafiti sijui ni wakitu gani, huku akiacha uvunjaji wa sheria za usalama barabarani ukiendelea pasipo na mtu wa kukemea.
Trafiki wangeweza kabisa kuzuia ajali nyingi sana ambazo zinasababishwa na madereva wanapuuzia sheria za usalama barabarani kama wangeamua kuwatafuta madereva hao na kuwawajibisha pasipo na huruma kabisa,wangeweza kutambua aina ya madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani na kuwatafuta kwa uwazi na kwa kujificha ili kuwaadabisha,HAKIKA hakuna ambaye angeendelea na uvunjaji wa sheria kirahisi wengi WANGEOGOPA,faini ya 30,000.00 ni kubwa mno kama itatozwa kwa kila avunjaye sheria za usalama. Trafiki wako BIZE na FIRE EXTINGUISHERS,ROAD LICENSE NA LESENI kana kwamba hivyo ndivyo visababishi vya ajali,haya ni MAPUNGUFU ya kiuongozi ndani ya Jeshi letu lisilo na maono ya namna ya kupunguza ajali,wanashindwa hata kuandaa mjadala ili wapate mbinu za kupambana na ajali.
Riverside/Mandela road ni eneo ambalo madereva hasa wa daladala wanajivunjia sheria bila pingamizi wa woga wa aina yoyote,Fikiria dereva anageuza gari (UTURN)Ubungo mataa kana kwamba ni jambo la kawaida kabisa,sasa huko kugeuza madaladala kusiko na mpangilio kwa eneo hilo ni jambo la kawaida,usije kuta mwenye lori amefanya ajali kwa kujaribu kujinasua na ajali iliyotokana na daladala kwa namna moja au nyingine.
Mungu awalaze pema marehemu wote na awasaidie majeruhi kupona haraka...
 
RIP waliotuacha na poleni wafiwa.

Lakini ni yale yale, mungu akipenda, mungu tunusuru, tutasali, tutakemea, tutaomba!

:mad::mad:Swala ni kwanini jali imetokea, je ni uzembe wa madereva? barabara mbovu? taa za barabarani mbovu? hatufuati sheria za barabarani?

Ajali karibu zote TZ zinasababishwa na sie wenyewe, taa nyekundu na hakuna gari watu wanapita, hata wengine wanadiriki kukutukana na kukupigia honi nyingi tu?! Magari mabovu hasa malori ni mengi mno! Kujaza mzigo kupita uwezo wa gari kumekithiri! Uendeshaji mbaya na wa hatari ni kawaida!

Itabidi tubadilike wabongo, ama sivyo ajali kama hizi hazitaisha!
 
Ajali nyingi za jijini husababishwa na madereva wa dala dala, wanasimama popote tna katikati ya barabara...kwa upande mwingine abiria wa wa dala dala pia tunachangia kwa kutosimama kaikati ya vituo may b kwa tamaa ya kuwahi seats or... Police Traffics wanjitahidi kusimamia bt pekeyao hawawezi kumaliza hili tatizo coz dala dala dvrs wako ka crazy kiaina!! Hesabu ya tajiri + small house +Msuba +academic +Posho ya Traffics + Usafi binafsi + Uchovu wa jua la kutwa = Ajalis

RIP WAPENDWA WETU!!
 
wakuu jitoshelezen na taarfa za idadi za watu tuliowapoteza, mkija na taarfa tata mnatutatiza. Msiwe kama vyombo vyetu vya televisheni na radio ambavyo huwa vinakinzana katika idadi ya wahanga kuonesha wasivyomakini. YOU ARE GREAT THINKERS, So fanyeni ya uhakika. Roho za marehem zipumzke kwa amani
 
lori hilo lilikuwa na abiria hivyo lilipoacha njia likapinduka au lilipoacha njia likajimuvuzisha kwa wabongo waliokuwa katika mishe zao? hebu nijue hapo wadau, coz nataka kufanya comment na iziraeli apunguze kidogo coz mwaka mpya umekaribia.
 
Eee Mwenyezi Mungu Rehemu, tunaomba uiokoe hii nchi yetu na ajali hizi, wape madereva moyo wa kuthamini watumiaji wengine wa barabara, waepushe na moyo wa kuwa na papara wawapo barabarani. Ameeeeeeeeni.
 
Ninasikitika kuawaarifu kua kuna ajali mbaya imetokea Ubongo Riverside ambapo gari aina ya lori limeacha njia na kugonga watu.

Kwa uchache inasemekana maiti 20 zimeokotwa eneo la ajali.

Habari zaidi zitawajia hivi punde
kaka hebu peruzi kaswari kangu afu unijibu, nasubiri tafadhali.
 

katikati ni gari ndogo nyekundu iliyokandamizwa chini ya gari kubwa jeupe la mafuta. kuna mtu yuko hai bado hajatolewa. habari zinasema watu watatu wamekufa kati yao mama mjamzito ambaye kichwa na kiwiliwili vimetengana



Baadhi ya watu katika eneo la ajali
Na Mjengwablog

Asante kwa taarifa Fide
 
Pole sna ni mara ya tatu kwa mwaka huu eneo hilo kupata ajali mbaya. Sababu ni njiapanda ya Mzee wa ..........
 
Dala dala kusimamia nje ya kituo ni gonjwa sugu hapa mjini na askari wetu ni kama wameubariki huu uhalifu kwani upo kila mahali lakini hawachukui hatua mpaka ikitokea ajali kama hii ndiyo watasimamia kwa siku mbili kisha upuuzi unaendelea. Napendekeza operesheni maalum kudhibiti dala dala kusimama nje ya kituo wakikutwa wachapwe viboko kumi hapo hapo bila faini wala nini.
 
Back
Top Bottom