Ajali Ubungo Riverside

Ajali Ubungo Riverside

wana jf tuache upumbavu na kuwa na mawazo machafu ..barabara zetu ni mbovu na magari ni mambovu ajali zikitokea tunasingizia freemason..haya si ni masaburi kweli?
 
Haya Watanzania haya ndo mambo ya Leseni Mpya za Madereva, ajali kila siku, haya yote yanatokea sababu yana maslai ya watu wachache wanaojijali wenyewe, Leseni Mpya walisema zitapunguza ajali kwa kuwabaini Madereva wazembe lakini Leseni hizo ndizo zinazotolewa kwa rushwa kwa Watu wasio na ujuzi wala kusomea udereva na chanzo chake ni ajali kama hizi.
 
hizi dala dala ni shida sana, na bado zitaendelea kusababisha ajari maana anaeamuru gari liende au lisimame ni konda.
 
jamani pole zao wooote Mungu awasaidie walionaswa watolewe salama. Ee Mungu tunusuru na hizi ajali too much
 
Mimi sikuwahi kumlaumu marehemu mzuzuri kwa kumtwanga risasi yule dereva daladala ...marehemu mbonde. Kutoa uhai wake sikupenda, lakini kumtwanga risasi ilikuwa awa kabisa.
madereva wa daladala ni tatizo kubwa sana hapa mjini...
Yeyote anayeingia kwenye anga zangu nampa ya takoni akamuonyeshe mkewe.
mimi nilikuwepo tanker lilkuwa linatoka ubungom kuelekea buguruni kufika kituo cha daladala cha riverside likakuta daladala limepaki njiani na kwa kuwa lilikuwa mwendo kasi likashindwa kufunga breki likapanda ukuta na kugonga gari zilizo kuwa kwenye foleni zinatoka buguruni kuja ubungo,yule mwenye daladala mwenye makosa kakimbia,ajali ni mbaya sana kuna mama kakatika kichwa hapohapo,lecturer mmoja wa chuo kikuuu namfahamu kwa sura amepona pia ila amenusurika na gari yake.
 
Mimi sikuwahi kumlaumu marehemu mzuzuri kwa kumtwanga risasi yule dereva daladala ...marehemu mbonde. Kutoa uhai wake sikupenda, lakini kumtwanga risasi ilikuwa awa kabisa.
madereva wa daladala ni tatizo kubwa sana hapa mjini...
Yeyote anayeingia kwenye anga zangu nampa ya takoni akamuonyeshe mkewe.

I can feel the lump in my throat...daladala ni tatizo
 
I can feel the lump in my throat...daladala ni tatizo

Jamaa wanaendesha kama wanamiliki barabara.......all they can think of is how much money they can make in a day.....
Pole kwa wahanga...RIP marehemu....
 
Mbali ya lawama kwa trafiki,lkn pia madereva wetu wanachangia sana,mathalani; ajali ya leo chanzo ni dereva wa daladala aliyekuwa anapakia/shusha juu kwa juu ktk attempt ya kumkwepa ndo lori imeparamia mgema na kuvuka ng'ambo ya pili ya road,, angalia picha tulizowekewa juzi kati mabasi matatu yanaovertake tanker kwa pamoja kona za Iyovi,,recklessly,,ajali ikitokea pale tunawalaumu askari trafiki kweli?
 
dah polen sana mliopatwa na msiba na marehemu wote wapumzike kwa aman.Lakin cwaelewi mbna kuanzia huyu mwenye izi taarifa mpaka baadh ya media kwan wamefarik wa ngap
 
bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihidimiwe

achaha kutia watu moyo kizembe, huu ni uzembe wa watu wachache na wawajibishwe kwa hili,
bwana hajatwaa kuna washenzi wamewapoleka wenzetu.....alaaaa
 
Sijaipata vema, ila ni ajali mbaya, watu watatu wamekufamo na wengine bado wamekwama mu-gari.
Source: East Africa Radio

Nasikia ni eneo hilo hilo la Riverside juzi mutu mumoja nae alikufamo baada ya kugongwa na lilori wakati akijaribugi kuvukaga libarabara kuwahi ligari la Gongo la mboto lililokuwa liki U-turn pale darajani. Wakati wa jioni pale mahali si salama sana, kuna msongamano mkubwa sana na pilika nyingi za kuhangaikia magari na mahitaji. Serikali ni vizuri ikakomesha ile tabia ya kugeuzi daladala pale maeneo na kuondoa wamachinga ambao wamekua kero na kuongeza vibaka wanaoiba na kukimbilia chini ya daraja.

Mungu awarehemu Marehemu na kuwanusuru walioumia katika ajali hiyo.
 
Mimi niligongwa na daladala mwishoni mwa October lilipokuwa lina-overtake kushoto ili kuwahi abiria wakati najiandaa kupanda daladala lingine, nilivunjika mkono na kuwekewa vyuma, hadi sasa nina POP na kesi iko makao makuu traffic, maandalizi ya kuipeleka mahakamani yanaendelea............

Daladala ni janga hapa nchini, hususan jijini Dar,
 
Nimesoma simulizi kwenye thread hii, kweli inasikitisha. RIP marhemu wote!

Sasa tusubiri kinara wetu wa magogoni naye aje afariji kwa kauli zake nyepesi nyepesi kama kawaida yake.
 
inasikitisha sana.
R.I.P marehemu wote.
 
Hii ndiyo tzania yetu. Na sasa tunasherehekea miaka 50 ya uhuru huku miundo mbinu mibovu, madereva hawana ujuzi wowote kuhusiana na ethics za barabarani, maaskari wa usalama barabarani hawajui watendalo, viongozi wa juu nao hawajui nchi ipo ktk hali gani, wanavyoona kwao mambo ni shwari wanadhani watanzania wote ndio wapo hivyo, kwakuwa wao wanapopita mabarabarani ving'ora hupigwa na magari yote hujibanza pembeni, wanafikiri ndivyo na sisi wapiga kura wao tunavyoishi.
Mungu ibariki tzania, tulinde wanyonge tunaopoteza maisha kila siku kwa uzembe wachache tulio wapa dhamana ya kutuongoza, zilaze mahali pema peponi roho za marehemu wasio na hatia amen.
Poleni wafiwa wote na wahanga wa ajali hii mbaya.
 
Back
Top Bottom