Ajali Ubungo Riverside

wana jf tuache upumbavu na kuwa na mawazo machafu ..barabara zetu ni mbovu na magari ni mambovu ajali zikitokea tunasingizia freemason..haya si ni masaburi kweli?

Toka watu wasikie kuna freemasons basi kila kitu kinachowalazimu wafikirie nje ya box ili wakielewe wanakihusisha na masonry (wamezoea kufikria ndani ya box na hawataki kuacha).
 
Inauma sana...Poleni Sana wafiwa wote na wale wote waliopata majeraha. Hivi hawa madereva wanaosababisha ajali hizi na kisha kukimbia....hatuwezi hata kushinikiza wanaomiliki magari kuhusu utaratibu wa kuwa na taarifa kamili za watu wanaowaajiri! Inakera sana kuona hawa washenzi wanatokomea kila wasababishapo ajali!..Naitamani sana UDA ya enzi zile na sio hii uchwara ya sasa hivi!!!
 
Mimi niligongwa na daladala mwishoni mwa October lilipokuwa lina-overtake kushoto ili kuwahi abiria wakati najiandaa kupanda daladala lingine, nilivunjika mkono na kuwekewa vyuma, hadi sasa nina POP na kesi iko makao makuu traffic, maandalizi ya kuipeleka mahakamani yanaendelea............

Daladala ni janga hapa nchini, hususan jijini Dar,

pole sana mkuu!
 
Back
Top Bottom