AJALI TANZANIA: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AJALI TANZANIA: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SMU, Feb 16, 2010.

 1. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Hivi karibuni na hata siku za nyuma tumeshuhudia malumbano kati ya wamiliki wa mabasi ya abiria kwa upande mmoja na serikali (Polisi, Sumatra) kwa upande mwingine juu ya ulazima wa kufunga vidhibiti mwendo (Speed Governor) kwenye mabasi.

  Wamiliki wa mabasi wanasema speed governor hazijasaidia kupunguza ajali za barabarani. Na zaidi wanaona msisitizo wa serikali wa kufunga speed governor unamsukumo wa kibiashara zaidi kuliko kupunguza ajali.

  Je ni kweli speed governor hazisaidii kupunguza ajali? Kama hazisaidii, je nini kifanyike kupunguza ajali za barabarani?
  ------------

  [​IMG]

  Ndg wanabodi Heshima kwenu..

  Bila shaka vifo vingi vinavyotokea kwa kiasi kikubwa hivi sasa ni kutokana na ajali za magari barabarani hasa Mabasi..

  Tunaipongeza serikali kwa hatua mbalimbali ambazo imekua ikichukua ili kukabiliana na Changamoto hii kubwa japo kwa kiasi kikubwa bado ajali ni janga kwa nchi yetu..

  Kwa kua akili ni nywele na kila mtu anazake,nami pia naomba kuwashirikisha fikra nilizonazo kama ifuatavyo..

  1)SERIKALI IANZISHE VYUO MAALUMU KWA AJILI YA MAFUNZO YA UDEREVA WA MAGARI YA ABIRIA PEKEE..

  Serikali na sio vyuo binafsi vianzishe vyuo maalumu kwa ajili ya Madereva wa Abiria pekee...
  Hii itasaidia kupunguza madereva wa Mtaani wanaopiga dayworker kisha baada ya Muda wanaendesha mabasi ya Abiria.

  Nimesema vyuo maalumu na wala si VETA wala vyuo binafsi Kutokana na sababu kua sasa ,VETA na vyuo vingine binafsi vimekosa credibility yaani mtu yeyote anaweza pata leseni hata kwa magumashi ilimradi awe na pesa..

  Lakini pia ili mtu A-qualify kusomea udereva wa magari ya abiria awe amesoma mpaka kidato cha nne na awe amefaulu ili kupata watu makini wanaojielewa na si kuokoteleza hadi STD VII kama ilivyo sasa.

  2)KILA BASI LISAFIRI NA ASKARI WA BARABARANI ANGALAU MMOJA:

  Sio lazima askari aanze mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari...kunaweza kua na utaratibu wa askari maalumu wa barabarani kupokezana kila wilaya ambako gari hiyo itapita..hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kum-control driver hivyo kufata sheria zote za barabarani kama inavyopaswa.

  3)MISHAHARA YA MADEREVA IBORESHWE

  Hii itasaidia watu wengi kuwa motivated na kupenda kazi ya udereva ma mabasi hivyo kupata watu wengi wanaoqualify,hii inamana mtu aiendeshe gari kwa kua ameona ndo sehemu ya kutokea bali udereva uwe tamanio la mtu mwenyewe.

  Wapewe pesa ya kutosha na posho juu ili kumfanya Dereva afurahie kazi yake na kupunguza msongo wa mawazo..

  4)MISHAHARA YA ASKARI WA BARABARANI IBORESHWE

  Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa askari hawa kutoshawishika kuchukua pesa ndogondogo wanazopewa njiani hivyo kupelekea kufanya kazi zao kwa uaminifu na umakini wa hali ya Juu.

  5)ASKARI WA BARABARANI WAPUNGUZWE

  Wingi wa Askari wa barabarani waliopo hivi sasa haimanishi ni kuboresha utendaji na udhibiti wa ajali barabarani..unaweza kua na askari wachache na wakafanya kazi nzuri yenye zaidi,iwapo madereva hawataokotwa mitaani,wakalipwa pesa vizuri na askari nao wakalipwa pesa vizuri hakika makosa barabarani yatapungua kwa kiasi kikubwa..hii ina apply kwa madereva wa magari yote barabarani...

  Iwapo adadi ya askari barabarani itakua ndogo itakua rahisi kuwa hudumia financially na kwa pesa nzuri zaidi.
  Nashauri askari barabarani walipwe kuanzia milioni 1 kwa Mwezi.
  Utitiri wa askari barabarani haimanishi ndio uimarikaji wa utendaji kazi.

  6)UKAGUZI WA MABASI YA ABIRIA KABLA YA SAFARI UIMARISHWE..

  Ukaguzi wa maramojamoja unaofanywa na askari wa barabarani kwa sasa unamapungufu makubwa..
  Pawe na kikosi kazi maalumu ambacho kazi yake ni kukagua mabasi yote ya abiria siku moja kabla ya safari na gari hiyo iwe na alama kua imekidhi vigezo vya kusafirisha abiria kesho yake..Hii itasaidia hasa kupunguza ajali zitokazazo na uchovu wa magari yenyewe hasa yale yanayounga safari bila kupumzishwa..
  ikiwa na pamoja na kumpima dereva kabla ya kuanza safari kama hatumii madawa ya kulevya wala kilevi chochote..

  7)SUMATRA WASIFANYE KAZI KWA MATUKIO PEKEE

  SUMTRA Wasisubiri kupaza sauti katika kuwaambia umma kua nauli zitapanda kutokana na bei za mafuta kuongezeka,na wasisubiri mpaka matatizo yatokee ndo wajitokeze kwa waandishi wa habari kama wanavyofanya hivi sasa.SUMATRA Ifanye kazi yake ipasanyo na isifanye kazi kisiasa...

  Nimesema ni mawazo tu sio msaafu wala Biblia unaweza kosoa au kuboresha kwa Mtazamo chanya ili kutoa mawazo sahihi kisha yafanyiwe kazi na mamlaka husika.

  Karibuni kwa Mawazo chanya pia.

   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,649
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Hazisaidii mkuu

  madereva na wamiliki wa mabasi wana HOJA kwa sabau hii kitu ilikuwa introduced like 15 yrs ago, lakini ajali ndo zimezidi

  hakuna aliyekuwa anafatilia mbona yale mabasi yaliyodaiwa kufungwa , bado yalikuwa yanakimbia? na ajali zikawa pale pale

  mi naona kwanza serikali ijisafishe:

  1. jeshi la polisi liache kutoa leseni kwa rushwa. Madereva waende shule, wapimwe, wapite mitihani, wapimwe hadi akili ndo wapewe leseni

  2. Leseni zote sasa hivi zibadilishwe..tuwe na mfumo wa leseni amboa ni computerised, data za kila dereva ziwepo, na akisababisha ajali kuwe na point system apunguziwe na kosa likiwa kubwa anyang'anywe kabisa leseni

  3. mabasi yote ambayo ni malori yaondolewa barabarani..kwa maana ya kwamba ni mabasi ya abiria tu yaruhusiwe kubeba abiria. chasis za malori zilizojengewa bodi zisiruhusiwe kabisa. Inasikitisha serikali inalifahamu hili lakini bado wanaendelea kuwafumbia macho.

  4. mabasi yote yakagyuliwe pia kama yanakidhi viwango, mfano matairi nk. kampuni itakayoonekana kuwa na mabasi mabovu mabovu ifungiwe.

  5. Sheria za usalama barabarani zifuatwe. Mwendo kasi wa juu uongezwe kutoka 80km/h hadi 120km/hr iwe ndo maximum..tuwe realistic kwenye hili. bara bara zetu zimetengenezwa kwa sasa na kama kuna madereva makini, mabasi imara, nk hakuna sababu ya ajali

  6. Madereva wawe na mikataba kabisa na matajiri wao. walipwe kisheria na iwe inajulikana hata serikalini. Huu mtindo wa kulipwa posho tu unawafanya wasiwe na confidence na kazi yao, hivyo kuwaza mambo mengi ikiwemo kukimbiza magari ili wawahi kufika na hivyo kuonekana wanafaa zaidi kuliko wengine.
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  Kaizer,

  Asante kwa mchango wako. Kama kina Kombe wanapitia humu:rolleyes: huenda wakapata mwazo mapya!

  Pengine pia tunahitaji vigezo ili tuweze kupima kama ajali zinaongezeka ama zinapungua.

  Najua kuna watu wanajenga hoja kuwa magari yameongezeka. So kama kwa mfano mwaka 2000 kulikuwa na magari ya abiria 50,000 na tukawa na ajali 5,000 kwa mwaka, then unaweza sema kwa kila magari 10 ya abiria unategemea ajali moja kwa mwaka.

  Kama mwaka 2010, tuna magari ya abiria 140,000 barabarani na mwisho wa mwaka tukawa na ajali say 7,000, then 'in absolute terms', ajali zimeongezeka lakini 'in relative terms' zimepungua sana kwa sababu katika kila magari 20 inatokea ajali moja tu.

  Hata hivyo kwa kutizama idadi ya vifo in absolute terms, kwa hakika tunahitaji kufanya kitu kupunguza zaidi ajali hizi.
   
 4. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,830
  Likes Received: 20,818
  Trophy Points: 280
  OVERSPEEDING ni moja ya sababu za ajali,kama sio sababu kuu,sasa utazuiaje hili tatizo la speeding?huwezi kuweka traffic officers every mile from dar-mbeya-arusha...
  SPEED GOVERNOR zina work kama kukiwa na ufuatiliaji mzuri,tatizo hizi speed governor zao wanaweka kienyeji na madereva wanaweza kuzidisconnect then wana reset wakikaribia destination zao..tatizo ni madereva na traffic officers wasio waaminifu
  Ukisema speed limit 120km/hr hawa wavuta bangi(baadhi ya madereva wa mabasi )utawacontrol vipi waendeshe within limit?ukiwawekea muda wanaendesha faster wanasimama wakikaribia destination hadi muda ufike.
  Gari zote tunazoendesha ni ELECTRONICALLY LIMITED TO THE MAX SPEED unayoiona kwenye odometer mostly japanese cars(except those coming to europe and other western cars are limited to approx 180km/hr=110miles/hr, european models like bmw/merc ziko limited to 155mil/hr which is approx 260 km/hr
  Kama serikali iko serious iweke sheria hayo mabasi huko yanakotoka yawe ELECTRONICALLY LIMITED to speed which they think is safe,otherwise hizi governor zao za vichochoroni watu wata-temper nazo kila siku.
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Feb 16, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Spidi Govana si suluhu hata kidogo, tabu ama shida yetu tunatafuta majibu rahisi kwenye matatizo magumu, speed 80Km/Hr inaweza kuua kama sheria za usalama barabarani haitazingatiwa ama kusimamiwa vyema, naamini Trafic hawatimizi wajibu wao hatakidogo....natutakufa tu kama hatutabadili mfumo wa udhibiti wa Kanuni na sheria zetu .
   
 6. njugilo

  njugilo Member

  #6
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  I n my opinion maybe we need to go back to those days where we were having the state owned transport before start discussing this one.Je is any one who can at least gives us the accident statistics of those days? Again we can now ask on this:-
  1.Are our drivers have permanent employment?
  2.Did they have /receive packages and services like others normal government/private workers?
  Nadhani na maswali mengine of this type ,then ndio tuanze na kuona maisha yetu wanayadhamini vipi |
   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  Feb 16, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Hilo lawezakuwa Jibu kwa upande mmoja ama mwingine, lakini swala la msingi ni kutimiza sheria kwa makini, na zile legelege zipewe makali zaidi, Police wetu wa barabarani wazisimamie kwa umakini bila kujali huyu dereva ni wagari la Kikwete ama Pinda....
  Dereva atakae gonga na kuua, ikithibitika ni kwa uzembe wake afugwe kifungo kirefu kuanzia miaka saba.
  Faini ziwekwe kali na na zakuogopesha
   
 8. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2010
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  They need to think twice! What if accidents continue after the installation of speed governor???
   
 9. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #9
  Feb 16, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kwani walivyoweka gavana hizo miaka 1996 nakumbuka, zilisaidia nini, ajali ziliendelea kuwepo, maana hakuna Polisi wanaotimiza wajibu wao barabara katika upande wa Usalama barabarani.
  weka mabango ya mwendo unaopaswa kwenda kwenye barabara kuu zote, hata iwe 30Km/hr kisha ukimkamata dereva kazidisha, mpe adhabu itakayokuwa funzo na kwa wenzake, mwanzoni itakua ngumu ila wakizoea wataogopa nakuziheshimu sheria ipasavyo.
  kama kungekua na usimamizi makini wa sheria alama ya PUNDAMILIA kwenye vivuko vya waenda kwa miguu vingetosha badala ya matuta kwenye barabara zetu kuu......
  ukitaka kujua tatizo ni usimamizi duni wa sheria zetu angalia hata kazi ya kusimamia routes za daladalla zimewashinda Police wetu hadi kufikia kubinafsisha kazi hiyo...AIBU.
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  AAAAH mie nilipanda basi moja kupitia nairobi Dereva amefungasha kifurushi naulizia nini hii naambiwa mirungi ...speed tulikuwa tunaenda nadhani 150 ikipungua 130 nilikoma kupanda hayo mabasi
  Hivi hiyo mirungi haina kilevi na kwa nini barabara zima dereva yeye ni kutafuna tu ..
  nadhani waajiri wa hawa madereva wakiwa serious ajali zitapungua namna fulani
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Feb 16, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  SASA hapo jiulize, dereva anakula mirungi kwenye safari ndefu kama hiyo, hapo bado hajachanganya baghi na bia .
  kweli tunapozungumzia matatizo ya barabarani hapa Tz lazima tunayatizame kwa mapana hayo.....kuliko kung'ang'ana na spidi gavana..........Mtatufungia hizo gavana, wakati madereva wanakula unga , Mirungi plus baghi njia nzima.
   
 12. L

  Lukwangule Senior Member

  #12
  Feb 16, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna overspeeding kuna bad driving. Kama tukiondoa hii bad driving tutakuwa na nafasi ya kuzungumza. Ni kweli kama wanataka kufunga hayo magavana yao waende huko viwandani lakini si kutumia teknolojia ya kuibana pumzi mashine kubwa iliyotengenezwa miaka 15 baada ya kutolewa teknolojia ya gavana hii ambayo tunaingangania ahh tunaing'ang'ania. Polisi wanakuwa bure kichwani bure akilini. Hivi huu ugawaji wao wa leseni za kuendesha mabasi ya abiria si ndio wao wanaufanya kama pipi? hata wendawazimu wanatuendesha siku hizi. Akili zao bure bilesh katika kona badala ya kupunguza yeye anaongeza halafu analala kwa mwenzake upande ule ambao anakwenda... anambana anayekuja.Katika eneo ambalo ameambiwa kuna mtelezo yeye anasema hapa ndio bomba pa kuteleza anatanua pumzi anakanyaga zaidi anaitia mashine kujifukua zaidi. Bad driving na kama tusipoondoa bad driving tutaisha tu, ovateki nyingine ni laana tupu, hakuna hesabu . Na hao matajiri nao wanawapeleka watu kilimita 600 bila kuwapumzisha nao ni wendawazimu kabisa. Ni hayo tu, pokonya watu leseni waambie jifunzeni.
   
 13. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mpwa what u've elaborate ni good sana nakukubali,

  Tatizo linakuja kwa serikali yetu imejipangaaaaa kwenda kwa new technologies zinazokujaaa na hao police wanavifaaaa vya kudhibiti hii haliii?

  Nadhani twahitaji kuwa tiali kwa hili janga na pasiwepo longolongo na ufisadi,
  Mfano mzuri ni mabasi ya Mombasa Raha siju the owner ni yuko shinyanga au Mwanza au Dar ila nasikia tu utaratibu wao ni mzuri wan Databse system ambayo wejiunga kwa Satellite system ambayo ina tracker ya mabasi yote na mwendo kasi na kama kweli yafanya kazi vyema kwanini wengine wasijitumbukize kwa system kama izo?

  Hizo speed governor zenu kwanza zilisha shindwa iweje leo tena zirudishweeee ivi serikali imeshindwa kweli kuja mawazo ya kimsingi ivi huko USA,EUROPE na kwingineko huwa mwaenda kura rahaaaaa hamchunguzi mambo wenzetu huko wanafanyaje??

   
 14. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #14
  Feb 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Hapo umenena Mkuu, nasisitiza kuwa hakuna OVERSPEEDING kuna BAD DRIVING.
   
 15. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Shule, shule, shule,

  Nilipata bahati kutembelea nchi moja nilishangazwa na utaratibu wao wa kutoa leseni.

  Hebu cheki utaratibu huu halafu mfananishe na TZ.

  1. Mtu unaingia darasani mwaka mzima kujifunza theories. Hapa ina maana unajifunza alama zote za barabarani na kuzielewa maana yake. Wakati huo huo unaingia barabarani Practical ukiwa na mwalimu kwenye gari maalum.

  2. Baada ya mwaka mmoja, unapewa provisional licence ambayo unaruhusiwa kuendesha gari ila ukiwa na mtu mwenye senior licence pembeni. Hii nayo ni kwa mwaka mzima halafu ndo unapata full licence.

  3. Ukitaka kuwa dereva wa public service vehicles (Taxi, Buses) unatakiwa kuwa na leseni yenye miaka kumi au zaidi. Huko hamna mambo ya class A, B, C, D, au E. Huko ni experience na nidhamu.

  4. Ukifanya kosa pointi zinatolewa, zikifika kiasi fulani unatakiwa kuingia darasani si chini ya miezi sita. Hapo ndipo unalipia gharama za shule ambazo si mchezo.

  5. Dereva wa public transport (buses) kwa mwezi analipwa si chini ya $ 1,000. Wanaheshimu kazi ya udereva.

  6. Hairuhusiwi kuagiza nje ya nchi gari lenye umri wa zaidi ya miezi 12.

  Sasa kwa hali kama hii, ajali bado zipo lakini si fatal kama bongo. Ajali ni chache sana ukilinganisha hata na America ingawa wapo kwenye car ownership ratio sawa.
   
 16. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kwamba soeed fovernors zilikuwa introduced 15 years aga ba hazikuweza kupunguza ajali kutokana na wqamiliki wa mabasi kuziwekea electronic switch ya kuzima na kuwasha. Hata sasa watafanya hivyo hivyo kinachotakiwa na ammbacho watanzania hatukufanya wakati ni kuwapeleka mahaka,ani wamiliki wa mabasi kuwadai compensation kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya lesenu,

  Sectuioin 14 ya Katiba inasema hivi "Ki8la mtu ana haki ya uhai na kupata ulinzi wa misha kutoka kwa jamii kwa mujibu wa sheria" Hibyo speed governors ni moja ya sheria zilizowekwqa kulinda maisha. Mmmiliki wa basi aspofunga kifaa na kuhakikisha kinafanya kazi sawa sawa na basi likaendeshwa kwa mwendo kasi na kuua watu au kujeruhi.

  Apart from fidia ya bima ambayo huwa ni kidogo lwa iy is assimed that ajali husika lilikuwa ni tendo la bahati mbaya, ndugu wa marehemu na waliojeruhiwa wanapaswa kufungiua mashataka katika mahakama kuprove kuwa basi hilo lilikuwa mwendo kasi na ndio chanzo cha ajali iliyopoteza maisha ya ndugu zao na kiujeruhi; na hivyo kudai fidia kubwa sana ambayo itapelekea mabasi kuuzwa ndipo hawa wamiliki watajapo shika adabu.

  Utaratibu huu hufanyika nchi za jiranim basi la SCANDINAVIA liliwahi kuginga punda katika bumps yenye alama ya 30 KMs anout 7 years ago. Mwenye punda alikomaa hhadi akalipwa equivalent of 900,000/= za Kitanzania wakati huo. Basi lingine likaangika na kuua mama mmoja ilibidi mabasi ya 2 ya kampuni hiyo yauzwe kutosha kumlipa pampja na matibabu yake huko Kenya,

  Sio kweli kwamba ni vigogo wameagiza, ila ni sisi wanaharakati tulioingia katika sekta hii baada ya ajali za mabasi kuongezeka ndio tulividai tarehe 09 January 2010, ili wananchi waweze kupata conclusive evidence ya kuwafilisi wamil;iki wa Hazardous buses. HAYA WANANSHERIA CHANGAMKIENI TENDA HII

  Naomba wanasheria watusaidie mawazo ya kufanikisha wananchi wanaopoteza ndugu zao au kujeruhiwa kutpokana na mwendo kasi watakavyoweza kuwadai wamiliki wa mabasi haya fidia kubwa kubwa
  Thanks
   
 17. Mr. Miela

  Mr. Miela JF-Expert Member

  #17
  Feb 17, 2010
  Joined: Aug 2, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hoja kuhusu vyanzo vya ajali hazina research suport na kwa mimi binafsi siungi mkono hata moja!

  Mabasi yamejengwa juu ya chasis za malori.....
  ........Takwimu zilizopo zinazoonyesha kwamba hili linaweza kuwa ni tatizo?
  ........Na kama ni tatizo ni kwa kiwango gani?
  ........Je tatizo ni chasis au spidi iliyosababishwa injini kubwa?
  ........Je kuna tofauti ya spidi kati ya marcopolo ya brazili yenye gia nane (designed to carry passengers) na marcopolo ya kenya yenye gia 10?(Modified to carry passenger) ...vipi nissani yenye gia sita? uhusika wa aina hizi za magari ulivyo?

  Madereva wawe na mikataba ya ajira........
  ........Kwa vile kwa sasa hawana mikataba ya ajira, wanasababisha ajali kwa makusudi! Confidence inatokana na mshahara au kuijua kazi?
  ........Mwalimu wa madereva ana uelewa wa kutosha (kinadharia na kivitendo)

  Mabasi yakaguliwe kama yanakidhi viwango.......
  ........Yakaguliwe na nani (Vehicle inspector, afisa wa TBS, SUMATRA au Majembe?) na kufuata viwango vipi (TBS, JAAI vya India au Italy?)
  ........Vipuli feki vya magari vina mchango gani katika hili? (matairi, na vipuli vingine vinavyohusiana na breki za haya magari? Je vinahitaji ukaguzi madhubuti kabla havijafika sokoni?

  Miundombinu.......
  .........Barabara zimekaaje (upana wa barabara, alama za barabara, mawimbi barabarani ujenzi wa barabara usiokua wa viwango unaosababisha utelezi, n.k)

  Rushwa......
  .........Nafasi ya rushwa katika tatizo zima la ajali barabarani ikoje inaweza kudhibitiwa? na nani?

  Spidi gavernor.......
  .........Dereva anayeijua kazi yake anahitaji spidi governor? je inafanya kazi kwenye miteremiko mikali ambapo madereva hupiga kofi gia?

  Tunahitaji utafiti zaidi ili kuja njia sahihi ya kupambana na ajali nchini!
   
 18. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,649
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280

  Hili nalo ni wazo zuri sana mkuu. Ila kama tu watanunua mabasi na sio chasis za malori.

  kwa hiyo unaweza kuona kwamba tunatakuiwa kwanza mabasi yaliyo malori kwanza yaondoliewe kwa sababu engine capacity zao ni kubwa lakini mzigo mdogo soi yanakuwa very powerful and hence high speed. Pili yanakuwa sio mazima ki ivyo.

  tungeweka standards kwamba basi lazima liwe basi kweli na liwe na speed ambayo imesetiwa electronically

  halafu hizi speed governors hazina interference na mfumo mzima wa gari kweli?
   
 19. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Speed governor ni mradi tuu wa watu huo.
  Ni kheri wafunge GPS ambayo ni more efficient and cheap.
  Unaweza kuta CCM wanataka kusanya ela ya uchaguzi bure maana uyo Tosi amekomaa
   
 20. L

  Lukwangule Senior Member

  #20
  Feb 19, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda kuwataarifu wasomaji na wadau wa JF kuwa mambo ya gavana yamepigwa stop kw amuda kidogo na jamaa wanarejea mezani kwa mazungumzo kuona jambo la maana la kufanya ili kupunguza ajali.Hii ni kwa mujibu wa Mssika msemaji wa POLISI.
   
Loading...