Ajali ni nyingi Barabara ya Morogoro Dar es Salaam

benja

JF-Expert Member
May 10, 2011
318
196
Nawasalimu

Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufulu inajitahidi sana kujenga miundombinu nchini ikiwemo barabara. Dhumuni la kuandika uzi huu ni kuelezea ajali ambazo nimekuwa nikizishuhudia katika barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam hususan kuanzia Kimara Mwisho kuelekea Kibamba n.k.

Mkandarasi amejenga ile barabara kwa ustadi lkn kuna step ambayo imeachwa kwa muda mrefu sana ambapo imekuwa ikisababisha ajali nyingi sana. Nimeshuhudia magari, bajaji na bodaboda zikiserereka na kuanguka ama kuacha njia pale zinapojaribu kupanda step hiyo. Mkandarasi huyu aimize namna ya kuzuia magari kupanda step huku kazi ikiwa inaendelea ili kupunguza ajali nyingi zaidi.

Wasalaam!

Mtumiaji wa Barabara ya Morogoro

#TujilindeNaCovid19
 
benja,

Tangu Uhuru barabara ya Dar es Salaam kwenda Morogoro ni ya lami na wakati huo haikuwepo serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, hata hivyo ilikuwa ikiongoza kwa ajali.

Tuambie nini lengo la Post yako.
 
Hii barabara kila Mtawala akiingia lazima ataitekenya! Why hawawezi kuijenga kwa projection ya miaka 100?

I bet kuna Mtawala atakuja kung'o Mwendokasi aweke CITY TRAIN

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Barabara ina step?
Yes sijui niitumie lugha gani nieleweke ila ni kama "kampando" au step kama ilivyo step za kwenye ngazi hasa unapohama kutoka lane moja kwenda nyingine unakuwa unashuka au unapanda ili upate hiyo lane husika
 
Last week pale kimara kabla ya kufika Stop-Over kuna IST ilipigwa mbele na nyuma baada ya kubana barabara, wa ipunguza upana kwa yale masimenti, madereva hawakujua wakajiachia, likatokea la kutokea.
 
Yangu Uhuru barabara ya Dar es Salaam kwenda Morogoro ni ya lami na wakati huo haikuwepo serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, hata hivyo ilikuwa ikiongoza kwa ajali.
Tuambie nini lengo la Post yako.
Wananchi walishajua mbinu,unasifia kwanza serikali ndio unaeleza shida yako.
 
Aise zile step zinasababisha sana ajali, hasa kile kipande kutokea Stop ver mpk temboni, na kutokea mbezi stend Chuo aise ni noma sana, pikipiki na magari madogo na bajaji imekuwa sehemu ya kuchinjiwa.

Sent using kidole gumba
 
Yes sijui niitumie lugha gani nieleweke ila ni kama "kampando" au step kama ilivyo step za kwenye ngazi hasa unapohama kutoka lane moja kwenda nyingine unakuwa unashuka au unapanda ili upate hiyo lane husika
Ita tu step

Sent using kidole gumba
 
Tatizo mnazipanda kwa pupa, zina utaalam wake.
Unachosema ni kweli ukizipanda kama umeshika usukani kilegelege lazima ile kwako. Kwa madereva wageni wa kuendesha magari na wale wageni wa jiji la Dar wanakula mieleka sana.
 
Unachosema ni kweli ukizipanda kama umeshika usukani kilegelege lazima ile kwako. Kwa madereva wageni wa kuendesha magari na wale wageni wa jiji la Dar wanakula mieleka sana.
Yaah inatakiwa ukaze uskani ili isikuvute kwa maana ukipanda step gari linavutwa kwa nguvu kama umeshika kilegelege inakutoa kwenye njia, hasa ukiwa mwendo mkali inakuwa hatari zaidi.

Sent using kidole gumba
 
Nawasalimu

Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Mh, Dr. John Pombe Joseph Magufulu inajitahidi sana kujenga miundombinu nchini ikiwemo barabara. Dhumuni la kuandika uzi huu ni kuelezea ajali ambazo nimekuwa nikizishuhudia katika barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam hususan kuanzia Kimara Mwisho kuelekea Kibamba n.k.

Mkandarasi amejenga ile barabara kwa ustadi lkn kuna step ambayo imeachwa kwa muda mrefu sana ambapo imekuwa ikisababisha ajali nyingi sana. Nimeshuhudia magari, bajaji na bodaboda zikiserereka na kuanguka ama kuacha njia pale zinapojaribu kupanda step hiyo. Mkandarasi huyu aimize namna ya kuzuia magari kupanda step huku kazi ikiwa inaendelea ili kupunguza ajali nyingi zaidi.

Wasalaam!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mtumiaji Wa Barabara ya Morogoro
#TujilindeNaCovid19
Ni kweli mkuu zile step ni ndefu mnoo namimi ni muhanga wa hili kuna siku nimeanguka na pikipiki nilikua nahama kutoka pembeni kuingia katikati sasa zile step ni ndefu mnoo yaani niliulamba chini sema mungu mkubwa kulikua hakuna gari inakuja na sikua speed sana hiki ndo kiliniokoa

Otherwise hata ukiangalia bajaji au gari pindi linavohama huwa linayumba kabisa

Yote 9 unashauriwa kutohama hama ile barabara maana ma step ni makubwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi hawafuati kanuni, spead limit zimewekwa lkn unakuta anakimbia sana, pale karibu na round about kimara kuna siku nimekuta magari manne yamevaana. Hadi unafika hatua unajiuliza walikuwa speed gani.
 
Back
Top Bottom