Kumbe pesa ni nini basi? tofautisha pesa na mali, ingawa sehemu kubwa ya mali huweza kupatikana kwa pesa, na hata mali inasemwa ina thamani kwa kulinganishwa na pesa.
Soma andiko langu vizuri, nimeainisha kuwa kuna pesa zinazopatikana kwa njia halali na zile zinazopatikana kwa njia haramu, hili halihusiani chochote na pesa za zindiko au sijui uganga kama mnavyoamini.
Pesa ni zile zile zilizoidhinishwa na Benki kuu ndizo zitazunguka, hao majini wako au mazindiko unawasema wangeingiza pesa kwenye mzunguko basi hata Benki kuu isingekuwa na kazi.
Mtu akilimiliki mali au mapesa kwa kuiba, kufisadi, kudhulumu, kutapeli n.k bado anakuwa na pesa zile zile zilizopo kwenye mzunguko na si kwamba ameingiza pesa zake kutoka kusikojulikana, tofauti yake tu na Wanaopata pesa zao kwa njia halali ni kuwa siku moja utalipwa tu unachostahili iwapo ulidhulumu wenzako (siwafahamu hawa Marehemu hivyo siwahusishi kwenye hili andiko langu).