AJALI: Mkuu wa kitengo cha Leseni - Mayfair afa ajalini Kisarawe

AJALI: Mkuu wa kitengo cha Leseni - Mayfair afa ajalini Kisarawe

Apepe askari mtoa leseni.
Kifo pia ni funzo. Alivaa mkanda kwa wenye kujua kuchunguza?

Halafu mbona kama watu wamekemea utoaji wa picha hizi kuliko zingine? Nimewaza tu!
 
Jamani tunatakiwa kuwa waangalifu kuhusu upigaji picha za marehemu na kuzitundika mtandaoni. Hivi angekuwa baba yako, kaka yako, dada yako, ungepiga pjcha hizo. Nashutumu sana aliyepiga na nalalamikia sana moderator kwa kuziachia picha hizi na zile za musoma muwa mtandaoni. Tuheshimj haki za marehemu. Ndio maana wakifa mahospitalini wanafunikwa.

Mkuu unaweza kuwa sawa kulaumu lakini kwa upande wa pili unatakiwa ufahamu picha pia utoa fundisho kwa mtu kuona athari za ajali uingiwa na woga na utambua madhara ya ajali na hususani uendeshaji mbovu wa madereva wetu kuliko kuishia kutaja idadi ya majerui na marehemu.
 
Apepe askari mtoa leseni.
Kifo pia ni funzo. Alivaa mkanda kwa wenye kujua kuchunguza?

Halafu mbona kama watu wamekemea utoaji wa picha hizi kuliko zingine? Nimewaza tu!

nenda kwenyevitafunio walivyojazana loh

RIP
 
Umewaza mbali sana Pdidy
Watu wanabagua picha. Tujifunze tu! Hivi alivaa mkanda huyo?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ... picha pia utoa fundisho ... kuliko kuishia kutaja idadi ya majerui na marehemu.

Upo sawa sana. Apepe askari. Tuliobaki tujifunze. Picha husema sana kuyazidi maneno mara elfu...........
 
Jeshi la Polisi nchini limepata pigo jingine baada ya askari wake kutoka Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kufa katika ajali huko Kisarawe mkoani Pwani jana.

Aliyepoteza maisha ni Mkuu wa Kitengo cha leseni Mayfair

ukimwangalia jamaa ajaumia huyu wamemlamba msukule jaman
 
Poleni sana wafiwa na jeshi la polisi kaa ujumla kwa msiba huu.

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la Mungu lihimidiwe.

Sia ajabu wakaja vikaragosi hapa na kutoa matusi na kejeli kwa wafu hawa wasio na hatia kwa sasa mbele zetu bali kwa mungu pekee mhukumu...tuvute suubira!

Raha ya milele uwape Ee Bwana na mwanga wa milele uwaangazie. Amina
 
Hizi ajali hazitatubakiza,tutatafuta mchawi mpaka tuchoke kumbe wachawi sisi wenyewe tunajimaliza.
 
namfahamu vizuri sana marehemu alikuwa ni veco na kweli eneo lake la kazi ilikuwa ni pale mayfair sijapata vizuri maelezo ya ajali ilikuwaje lakini sio vizuri kukejeli marehemu
 
Hizi ajali hazitatubakiza,tutatafuta mchawi mpaka tuchoke kumbe wachawi sisi wenyewe tunajimaliza.

Rafiki yangu aliwahi kusimamisha Hood isiendelee na safari zaidi ya masaa 4 kwa kuwa dereva alikua kalewa! Baada ya Polisi kufika na dereva kupimwa, abiria wengine ndo wakamsapoti. Ingawa mwanzoni alionekana anachelewesha wengine.

Usalama barabarani ni jukumu letu sote. Shime abiria wenzangu tuamke na kukemea madereva wasiojali uhai wetu. Chonde chonde!
 
Hivi leseni zao zinakaguliwa watu hao? Au uzoefu na kujuana tu? Kinondoni na Kisarawe wapi na wapi jamani mwe?

Anyways, RIP afande wetu.

Mapolisi wakaguliwe leseni zao na pia magari yao traffic wayakague kama yale ya raia. Kuoneana aibu madhara yake ndo haya. Yasemwayo mnaweza kuyapuuza, lakini hata wosia wa makaburini sio kwa ajili ya marehemu, bali kukumbushana tuliobahatika kubaki tuwe waangalifu zaidi.

Mtu asiye na akili atadhani hiyo ni kejeli, hakuna anayefurahia kifo cha binadamu mwenzie kwani kifo cha mmoja huacha mlolongo wa mateso kwa waliokuwa wanamtegemea.



RIP Kamanda

Wa kuzikagua ni nani, mara nyingi wao huzingatia sheria kwakuwa ndiyo watoa elimu ya usalama barabarani, yawezekana ajali ilisababishwa na mechanical fault kwenye gari
 
Nakuunga mkono Mkuu hii tabia ya kutuma picha za marehemu wa ajali za barabarani au kwa tukio lolote lile si nzuri hata kidogo. Inawezekana kabisa kwamba ndugu wa karibu wa marehemu hata hawana taarifa ya kifo na labda mmoja wa ndugu wa marehemu anaingia hapa na kukuta picha ya ndugu yake akiwa amekufa. Tuwape heshima marehemu na ndugu zao na kuacha mara moja hii tabia inayoshamiri kwa kasi ya kutisha hapa jamvini.

Jamani tunatakiwa kuwa waangalifu kuhusu upigaji picha za marehemu na kuzitundika mtandaoni. Hivi angekuwa baba yako, kaka yako, dada yako, ungepiga pjcha hizo. Nashutumu sana aliyepiga na nalalamikia sana moderator kwa kuziachia picha hizi na zile za musoma muwa mtandaoni. Tuheshimj haki za marehemu. Ndio maana wakifa mahospitalini wanafunikwa.
 
Ungetoa pole na kukaaa kimya ilikuwa inatosha sana

Atakuwa polisi huyo, na jinsi anavoona anaifanyia jamii anaona kuwa lazima akitutoka watu watashangili. Rip japo marehemu inaonekana hakuvaa hata mkanda.
 
Back
Top Bottom