Ajali iliyohusisha Magari Nane, maelezo ya Polisi yanatia shaka

B0DD4EA4-482E-4C4E-84A8-443505942301.jpeg
Ripoti ya uchunguzi inasema makosa ni ya dereva wa lori (jeupe) alikuwa anaovertake sehemu isiyoruhusiwa!
 
Mkuu Shalom,
Kwa hiyo unasuspect lori lililosababisha ajali limekimbia?

Kinaweza likawa halijakimbia ila huenda maelezo ya polisi ni ya uongo.

Lori linalotajwa hakuna mtu ameliona kwenye picha.

Lorry lililipo kwenye picha ni FAW na siyo HOWO.

Huenda hilo Lorry la Howo wanalitaja ili kufunika makosa yao. Lakini hiyo haibadili chochote kwamba askari aliyetanua alifanya makosa.

Kisheria mkipata ajali hakitakiwi kuhamishwa kitu chochote eneo ajali na polisi wanalifahamu hili.

Sasa kwanini Hilo Lori la Howo halionekani pichani?
 
View attachment 2015323Ripoti ya uchunguzi inasema makosa ni ya dereva wa lori (jeupe) alikuwa anaovertake sehemu isiyoruhusiwa!
Lori linalotajwa kwenye report siyo linaloonekana pichani.

Sasa swali ni je lori linalotajwa kwenye report liko wapi?

Kwenye report imetajwa Howo kwenye picha inaonekana FAW.

Watu hawavioni hivi vitu.
 
Kinaweza likawa halijakimbia ila huenda maelezo ya polisi ni ya uongo.

Lori linalotajwa hakuna mtu ameliona kwenye picha.

Lorry lililipo kwenye picha ni FAW na siyo HOWO.

Huenda hilo Lorry la Howo wanalitaja ili kufunika makosa yao. Lakini hiyo haibadili chochote kwamba askari aliyetanua alifanya makosa.

Kisheria mkipata ajali hakitakiwi kuhamishwa kitu chochote eneo ajali na polisi wanalifahamu hili.

Sasa kwanini Hilo Lori la Howo halionekani pichani?
Uko sahihi sana Kiongozi, nimekubali.
Analysis yako iko sawa.
 
TUKIO LIMEKAGULIWA NA

ACP. SOFIA JONGO RPC TANGA

AKISAIDIWA NA

SSP LEOPORD .N. FUNGU RTO TANGA , SP. ELIAS RWAMBANO OCS KABUKU, A/INSP RAJABU KAIMU DTO HANDENI PAMOJA NA G.3191 CPL

MUSSA AMBAYE NDIYE AMECHORA NA KUPIMA ENEO LA TUKIO
Ningekuwa na mamlaka , hawa wote wangekuwa hawana kazi mpaka sasa kwa kosa la kufanyakazi chini ya kiwango
 
Jambo la muhimu ni kwa watu wote kutumia akili wakati wote, hata kama wanadanganya basi aibu iwepo. Ustaarabu ni kutumia akili.
Kudanganya (ambapo ni kubaya kwa kuwa ni kukosa maadili mema) hakukubaliki kwa namna yoyote.
 
Picha iko clear kabisa. Gari moja ya Polisi ilikuwa inajaribu kuivertake ile nyingine ya polisi (tena kwenye eneo lisiloruhusu overtaking kabisa).then ikakutana na roli. Technolojia huwa haidanganyi
 
Back
Top Bottom