Ajali iliyohusisha Magari Nane, maelezo ya Polisi yanatia shaka

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
45,525
2,000
Nimejaribu kusoma kwa utulivu kisha nikaangalia picha, naona kama yanapingana na uhalisia, anyway Wajuvi nisaidieni, lory HOwo ame-ovrtake kweli hapo??

Afande taarifa ya ajali:

KAB/TR/ar/16/2021(×)ajali ya magari manane kugongana na kusababisha majeruhi na uharibifu wa magari (×) mnamo tar 14/11/2021 majira ya saa 18:30 huko katika kijiji cha Kwedilomba kata ya Kwedibomba tarafa ya mzundu wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga barabara kuu ya Segera-Chalinze gari No.T.131 DVU aina ya HOW yenye tela No.T.329 DMR ikiendeshwa na Saimon S/O kristo @Mwanyila, 36yrs, Mbena, mkazi wa Kibaha Pwani akitokea kabuku kuelekea Chalinze alipokuwa akijalibu kulipita gari la mbele yake mahala pasipo ruhusiwa ndipo ghafla mbele yake kukatokea gari nyingine iliyokuwa ikitokea Chalinze kuelekea kabuku yenye No.Pt.4036 ashok leyland mali ya jeshi la polisi Tanzania likiendeshwa na H.3637 CPL Juma wa chuo cha Polis CCP Kilimanjalo na ndipo dereva wa gari No.Pt.4036 alisimama ghafla ili kuepuka ajali isitokee na ndipo baada ya gari hiyo kusimama ghafla ikatokea gari nyingine kwa nyuma iliyokuwa ikitokea Chalinze kuelekea Kabuku PT.4087 ashok leyland ikiendeshwa na F.7658 CPL John Robert wa makao makuu madogo ya polisi DSM na kugonga kwa nyuma.

Ghafla tena ikaja gari nyingine kwa nyuma No.Pt.4097 ashok leyland ikiendeshwa na F.5889 CPL Kigiri wa Polisi makao makuu madogo ya Polisi DSM na kusimama ghafla PT.4087 ashok leyland na kusababisha gari No. PT.2370 Isuzu bus ikiendeshwa na g.6123 CPL abel wa chuo cha polisi Kidatu na kugonga ubavuni gari no.Pt.4087 ashok leyland pia ikatokea tena gari No.T.573 AYR toyota corolla ikiendeshwa na Amin S/O UR Rasul@Khan, 60yrs, mkazi wa Tanga na kusimama ghafla baada ya kuona ajali na kusababisha gari no.SU 44275 gx v8 mali ya TANESCO DSM ikiendeshwa na Tuma S/O Hassan lean na kuigonga kwa nyuma gari hiyo no.T.573 AYR Toyota corolla pia ikasababisha gari nyingine yenye no T.773 CND Toyota hilux kuigonga kwa nyuma gari hiyo no.Su.44275 GXV8 TANESCO na kusababisha majeruhi kwa watu 16 ambao ni 1.D.8420 s/SGT John Mwakipesile 2.Pf.18891 insp sister 3.G.6123 CPL Abel ambao wote watatu wamepelekwa hospitali ya rufaa Bombo kwa matibabu

Na 4.Pf.17534 insp Rashida 5.Pf.18326 insp Nyalugembe 6.Pf.17896 insp Gonga 7.Pf.18202 insp Said 8.Pf.17166 insp Ally juakal 9.Pf.17899 insp Sanya 10.Pf.18445 insp pangane 11.Pf.17691 insp Peter 12.Pf.18719 insp Ohusso 13.Pf.17321 insp Ilomo 14.Pf.18616 insp Anthony 15.Pf.17674 insp Zongho 16.H.1659 pc gift (×) majeruhi wote wameumia sehemu mbalimbali za mwili na kutibiwa kituo cha afya Kabuku na kuruhusiwa (×) chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari no.T.131 dvu how yenye tela no.T.329 dmr kujalibu kulipita gari iliyokuwa mbele yake pasipo kuchukuwa tahadhali (×) dereva amekamatwa yupo mahabusu kituo cha polisi Kabuku kwa ajili ya mahojiano (×) eneo la tukio limekaguliwa na acp. Sofia jongo rpc Tanga akisaidiwa na ssp leopord .N. Fungu rto tanga , sp. Elias Rwambano ocs Kabuku, a/insp Rajabu kaimu DTO Handeni pamoja na g.3191 cpl Mussa ambaye ndiye amechora na kupima eneo la tukio (×)///////////

Taarifa kwa maandishi inafuata //////////


Toka rto tanga ///////////

IMG-20211116-WA0119.jpg

Picha nyingine hizi hapa

IMG-20211116-WA0100.jpg


IMG-20211116-WA0089.jpg


IMG-20211116-WA0104.jpg


IMG-20211116-WA0093.jpg


IMG-20211116-WA0103.jpg


IMG-20211116-WA0091.jpg


IMG-20211116-WA0096.jpg


IMG-20211116-WA0105.jpg


IMG-20211116-WA0087.jpg
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,448
2,000
Nimejaribu kusoma kwa utulivu kisha nikaangalia picha, naona kama yanapingana na uhalisia, anyway Wajuvi nisaidieni, lory HOwo ame-ovrtake kweli hapo??

AFANDE TAARIFA YA AJALI:
KAB/TR/AR/16/2021(×)AJALI YA MAGARI MANANE KUGONGANA NA KUSABABISHA MAJERUHI NA UHARIBIFU WA MAGARI (×) MNAMO TAR 14/11/2021 MAJIRA YA SAA 18:30 HUKO KATIKA KIJIJI CHA KWEDILOMBA KATA YA KWEDIBOMBA TARAFA YA MZUNDU WILAYA YA HANDENI

Serikali ni kikundi cha watu kilichojitwalia madaraka kutoka kwa wananchi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom