AJALI: Basi la kampuni ya Jordan lapata ajali na kuua

AJALI: Basi la kampuni ya Jordan lapata ajali na kuua

Inawezekana madereva wengi wana ubongo sawa na wa mnyama Nyumbu. Namna ya uendeshaji na matokeo ya uendeshaji huo karibu yote yanaelekea. Itakuwa namna ya kuwaza na kuhitimisja/kutenda inafanana.
Suluhisho ni ushauri nasaha na mafundisho ili na wao wawaze na kuhitimisha sawa na binadam mwenye utashi wa kutambua uhusiano uliopo Kati yake na mazingira anayoyaishi na kuendesha maisha yake wakati wote.
 
Hii sio kawaida there is something spiritual behind these road accidents
 
Nchi iko kwenye Mapito Makubwa sana... siku hizi watu kufa kwa ajali imekuw ani kawaida..Tuliombee TAIFA Tanganyika
 
Mungu nakuomba uwalaze mahali pema marehemu na uwapatie speedy recovery majeruhi wote.
 
Inawezekana madereva wengi wana ubongo sawa na wa mnyama Nyumbu. Namna ya uendeshaji na matokeo ya uendeshaji huo karibu yote yanaelekea. Itakuwa namna ya kuwaza na kuhitimisja/kutenda inafanana.
Suluhisho ni ushauri nasaha na mafundisho ili na wao wawaze na kuhitimisha sawa na binadam mwenye utashi wa kutambua uhusiano uliopo Kati yake na mazingira anayoyaishi na kuendesha maisha yake wakati wote.

hawa madereva kweli wako kama nyumbu....tena wale ambao huwa wana-migrate to masai mara!! wanapita mto ule ule kila mwaka na wanaliwa na mamba life goes on! sasa hawa madereva wanapita njia hio hio nyembamba,ina mashimo na milima kila siku lakini wanakimbia na kuyaangusha hayo magari kwenye kona kali wanazozijua!!! labda wangekuwa ni wageni na barabara, lakini hata ukiwa mgeni na barabara kama una akili timamu huwezi kukimbia hovyo!
 
Sijui niseme nini sasa........RIP wote mliokufa ajalini..........
 
Basi la kampuni ya Jordan lenye namba za usajili T650 AQZ, linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Moshi limepata ajali maeneo ya Kitangiri, Nzega.Mpaka sasa mtu mmoja amepoteza maisha baada ya kulaliwa na basi hilo.

Basi hilo lililokuwa likitokea Mwanza kwenda Arusha, linaelezwa kuwa lilipinduka baada ya kumshinda dereva katika eneo lenye kona kali.
Eneo hili nalijua maana mimi mwenyewe nishakuwa muhanga.Kuna kona kali sana na mbaya zaidi hakuna kibao kinachoonesha kuwa mbele kuna kona kali na barabara ni nzuri sana inashawishi kuzidi kuchochea spidi.Mara nyingi mabasi huwa yanapinduka eneo lile kutokana na madereva kushindwa ku-control gari.

Sitapasahau Kitangiri,Nzega.
kitangiri.png
 
Basi la kampuni ya Jordan limepinduka na kuua watu 8 Kilometa 6 kutoka mji wa Nzega.

Lilikuwa likitokea Mwanza kwenda Moshi.

''Kutokana na ajali za barabarani ambazo watawala kama vile wameshindwa kusimamia au kuchukua hatua za dharura kunusuru maisha ya watu ambayo yanapotea kila siku;Ningekuwa kiongozi ningesema haya yafuatayo:

''Sitaki kusikia ajali zinatokea ,hivyo basi kamanda wa usalaama barabani wa eneo usika (eneo la ajari),mkuu wa wilaya wa eneo n.k , barua zao ziko tayari kufukuzwa kazi kama hayo yatatokea katika eneo lao ikiambatana na kutunga sheria ya kufungwa kwa miaka 1 jela kwa kushindwa kuweka mikakati ya kuzuia ajali'katika eneo lao''

MATOKEO:Wakuu hao wataweka mitakati ya kudhibiti ajari, hutasikia ajari za hovyo ovyo.

Mambo mengine
1.kama wauzaji wa madawa ya kulevya wamewekewa sheria kali,kwa nini madereva na wamiliki wa kampuni ya usafirishaji yasiwekewe sheria kali.''SHERIA ITUNGWE HARAKA''
Mfano🙁a)ikithibitika ni uzembe wa dereva;Dereva akisababisha ajari atalipa fidia ya TZS billion 10 Na kifungo cha maisha jela
(b) Wamiliki wa mabasi hayo pia watalipa fidia ya TZS billion 10 na kufungiwa kufanya shughuli za usafirishaji kwa miaka isiopungua 5.

2.Serikali kufuta vyuo vya mitaani ambavyo havina sifa za kufundisha udereva.

Je kama haya yakisimamiwa kutakuwa na ajalii ZA barabarani ?
 
Hii sasa inatisha maana kila siku ni ajali .Mungu tunusuru
 
dah tatizo nn dah harafu tochi ndo ivyo zimevutwa kila kitu siasa tu dah noma sana sheria za barabarani dah mwendo kasi dah madereva na pombe dah wanachoka sana dah hawana mda wa kupumzika dah wakipumzika wanaenda baa dah kesho wanaanza safari dah rushwa je dah barabara mbovu dah magari yanakaguliwa je dar service kabla ya kuondoka dar MUNGU TUSAIDIE
sheria aina macho wanayoiongoza vipofu

Tochi zipo palepale mkuu ilikuwa ni agizo la siku moja tu siku ile ya mgomo
 
Mmh! Mmh! hapana hii apana nasema hii hapana haikubaliki no no way! too much.
 
Inawezekana madereva wengi wana ubongo sawa na wa mnyama Nyumbu. Namna ya uendeshaji na matokeo ya uendeshaji huo karibu yote yanaelekea. Itakuwa namna ya kuwaza na kuhitimisja/kutenda inafanana.
Suluhisho ni ushauri nasaha na mafundisho ili na wao wawaze na kuhitimisha sawa na binadam mwenye utashi wa kutambua uhusiano uliopo Kati yake na mazingira anayoyaishi na kuendesha maisha yake wakati wote.

mwaka huu kampuni zimebadili madereva?
unamaanisha waliokua wanaendesha vipindi vya nyuma ni tofauti na waleo?
 
Jamani yule aliyetangaza mgomo kwa mbwembwe yuko wapi..suala sio viwango vya barabara bali ni uzembe wa madereva..kwa anaesafiri kwa mabasi atakubaliana na mimi. Hawa madereva wetu ajali zao ni kwenye kona kali,wakati wa ku over take na mwendo kasi katika maeneo hatarishi. Wakiambiwa warudi darasani kupigwa msasa wanagoma..Hembu nitafutieni yule muhamasisha mgomo nimpe nakozi shenzy taipuuu
 
Hapa dawa ni serikali kupiga marufuku kusafiri kwa mabasi mpaka uchaguzi upite raia wote wasafiri kwa miguu. Naona wamebanwa kwenye albino wamegeukia kwenye mabasi.

Ulichoongea ni kweli kabisa. Hata mimi niliwaza hivyohivyo. Kafara za Uchaguzi hizi!
 
Back
Top Bottom