AJALI: Basi la kampuni ya Jordan lapata ajali na kuua

AJALI: Basi la kampuni ya Jordan lapata ajali na kuua

Mgomo wa abiria kusafiri utasaidia yule aliyeitisha wa madereva aitishe na wa abiria sasa!! au anafurahia hao madereva wanavyoua watu maana yupo kimyaa mashauzi yote yamemuisha!

Laiti hili lingewezekana labda ingesaidia..kugomea kupanda mabasi kwa wiki mbili mfululizo....Mambo gani haya jamani? Imezidi sasa.
 
Waziri mhusika anafanya nini ofisini❓❔❕❗
 
Baadhi ya picha za ajali
 
Attachments

  • 1429094315212.jpg
    1429094315212.jpg
    107.1 KB · Views: 547
Hali kama hii viongozi wa miundombinu wa usafirishaji sumatra na hata raisi wamekaa kimya .... Nashindwa kuelewa. Hata kutafakari haya inakua ngumu

kwa nini hawana tamko? Kwa nini hawachukui hatua? Kwa nini kwa nini?
 
Basi la kampuni ya Jordan limepinduka na kuua watu 8 Kilometa 6 kutoka mji wa Nzega.

Lilikuwa likitokea Mwanza kwenda Moshi.

Wimbi hili la ajali linaashiria nchi hii iko chini ya laana kutokana na mauaji na uovu wa kila namna kukithiri.Serikali ikae na viongozi wa dini iwasikilize.Tatizo la ajali za kila itwapo leo hazitokani na uzembe tu wa madereva
 
Hapa dawa ni serikali kupiga marufuku kusafiri kwa mabasi mpaka uchaguzi upite raia wote wasafiri kwa miguu. Naona wamebanwa kwenye albino wamegeukia kwenye mabasi.

Inawezekana kiungo kimoja cha albino = watu kumi wa kawaida! , hivyo viungo ndio mana dau lake kubwa. Hili ni janga la kitaifa, hapa mpaka nchi za magharibi ziseme ndio utasikia wakuu wetu watalisemea, wapo wepesi kukanusha.

Mungu ibariki Tanzania
 
Poleni sana waliotangulia mbele ya haki serikali inatakiwa kutoa tamko kuhusu hawa madereva wazembe wanaoendelea kumaliza abiria kwa nini kipindi hiki kuna nini?
 
NAISHAURI SERIKALI IFANYE YAFUATAYO HARAKA:

1. IUNDE TUME KUCHUNGUZA KAMA HIZI YOUTONG/HIGER ZINA VIWANGO VYA KUWA MABASI YA ABIRIA.
2. MABASI YOTE YAKAGULIWE TAIRI ZOTE NA WATAALAMU KABLA HAYAJAANZA SAFARI MIKOANI KOTE.
3. MADEREVA WOTE WATEMBEE NA KADI MAALUM ITAKAYOKUWA INAJAZWA KILA WANAPOFIKA STENDI KUU ZA
WILAYA/MKOA VIPIMO KAMA WAMETUMIA KILEVI CHOCHOTE AU LA.
4. KABLA YA SAFARI ABIRIA WAMCHAGUE ABIRIA MMOJAWAPO KATI YAO AMBAYE ATAKUWA NA JUKUMU LA
KUMSIMAMIA DEREVA MPAKA MWISHO WA SAFARI. IWAPO ATAFANYA MAMBO AMBAYO YANAHATARISHA MAISHA
YAO KIONGOZI HUYO AWE AWE ANAWATAARIFU ABIRIA WENZAKE WAWEZE KUCHUKUA HATUA MAPEMA
(IKIWEZEKANa HATA KUMTANDIKA DEREVA VIBOKO) KABLA MAMBO HAYAJAARIBIKA.
 
Sijui tusemeje sasa, hii inatosha jamani!
Je, na matokeo ya design za barabara zinazoendana na viwango vya BRN - matokeo makubwa sasa au ni harakati za wanasiasa wa Kitanzania kuelekea 2015!?

Hapa rafiki naona kuna zaidi ya barabara. Jiulize; kwa nini tunasikia ajali nyingi mwaka wa uchaguzi? Ni ajali za barabarani kweli au makafara? Inauma sana kuona watanzania tunatoana sadaka kwa ajili ya uongozi tu (iwapo ni makafar ya uchaguzi)
 
Sipandi basi mpaka uchaguzi upite!
Mkuu kwani uchaguzi mkuu una uhusiano gani na ajali za mabasi barabarani?

Au ina connection na zile tafiti zilizofanywa na yale mashirika ya kimataifa, ambapo tafiti zao ziligundua kuwa kila unapofika mwaka wa uchaguzi mkuu, mauaji ya albino yanaongezeka kwa kasi ya kutisha sana!
 
Nimepita eneo la tukio, mtu mmoja ndio amefariki papo hapo wengine majeruhi
Mtu mmoja kivipi wakati hapo juu naona kama wawili,huyu aliyebanwa na gari kapona (Tshirt ya light blue) na huyu mwenye shati jeupe barabarani?Au ni majeruhi?
 
NAISHAURI SERIKALI IFANYE YAFUATAYO HARAKA:

1. IUNDE TUME KUCHUNGUZA KAMA HIZI YOUTONG/HIGER ZINA VIWANGO VYA KUWA MABASI YA ABIRIA.
2. MABASI YOTE YAKAGULIWE TAIRI ZOTE NA WATAALAMU KABLA HAYAJAANZA SAFARI MIKOANI KOTE.
3. MADEREVA WOTE WATEMBEE NA KADI MAALUM ITAKAYOKUWA INAJAZWA KILA WANAPOFIKA STENDI KUU ZA
WILAYA/MKOA VIPIMO KAMA WAMETUMIA KILEVI CHOCHOTE AU LA.
4. KABLA YA SAFARI ABIRIA WAMCHAGUE ABIRIA MMOJAWAPO KATI YAO AMBAYE ATAKUWA NA JUKUMU LA
KUMSIMAMIA DEREVA MPAKA MWISHO WA SAFARI. IWAPO ATAFANYA MAMBO AMBAYO YANAHATARISHA MAISHA
YAO KIONGOZI HUYO AWE AWE ANAWATAARIFU ABIRIA WENZAKE WAWEZE KUCHUKUA HATUA MAPEMA
(IKIWEZEKANa HATA KUMTANDIKA DEREVA VIBOKO) KABLA MAMBO HAYAJAARIBIKA.

Hapa naona unajaribu kutwanga maji kwenye kinu. Ni jambo lipi liliwahi kuanzishwa likafanikiwa na sirikiali ya awamu hii? Ukisema hayo yote unatengeneza mlango mwingine wa rushwa kwa sababu hakuna kitakachofanyika bila ya rushwa
 
Back
Top Bottom