AJALI: Basi la kampuni ya Jordan lapata ajali na kuua

AJALI: Basi la kampuni ya Jordan lapata ajali na kuua

hivi chanzo haswa cha ajali kufululiza ni nini haswa

bange + petroli + viroba + tochi za kujificha vichakani + usingizi kwa dereva + sifa za kijinga + abiria + sumatra + tanroads + israeli.
 
Mungu aturehemu tu. Yani ikipita siku bila ajali ni jambo la kushukuru Mungu. A
 
poleni wafiwa.Maombi nayo muhimu,Maana shetani ni muuaji.

ujinga na upumbavu wetu wenyewe sisi wanadamu usitupeleke kuanza kumshutumu illuminati ( shetani ) kuwa yeye ndiyo chanzo cha mara kwa mara za hizi ajali. siyo kweli hata kidogo na nakupinga tena kwa 100%. shetani ndiyo anawaambia abiria " oya wewe dereva hebu nyoosha mguu wako bhana alah " au " dereva tukiwahi kufika tunakokwenda kuna zawadi yako hapa " au " dereva tuwahishe bhana kama huwezi sema tukusaidie " au " dereva usipowahi sikupi dada yangu au sikupi nanihiiii yangu tukifika ". kwa kauli kama hizi unadhani hatutajipanga kweli kila siku kununua majeneza ya mazishi ya wahanga wa hizi ajali.
 
Serikali haikutakiwa kusalimu amri kwa madereva na wenye mabasi krahisi .

Kova kusema "Madereva Hoyeee" Ubungo amekosea sana!.

Hakupaswa kuwafagillia. Eti hakuna tochi tena kwamaderva/ mabasi wala...... Amefanya kisiasa zaidi

Naisikitikia nchi yangu. Hili lawezekana TZ tuu!

kova yuko bizy na gwajima
 
Sawa asante sana. Sikuwa na muda wa kupiga picha ila nilifanya kazi ya kutoa taarifa husika sehemu sahihi na ndio maana polisi na ambulance walifika na kutoa msaada, we unaongea kwakuwa una bundle ila mie ndio nimetoka hosp muda huu saa 4. Ila asante sana kwa mtazamo wako. Kuona picha za watu waliojeruhiwa ndio furaha yako! Well umejiuliza hao majeruhi wametokaje hapo na kufika hosp? Umeona picha ya watu wawili, mbona unajiaminisha rafiki? Mtu kulala chini ni amekufa? Nikwambie nimetoka hosp na nimefanya jitihada nyingi tu ambazo sihitaji kujitangaza ila Mungu anajua. Sio kila hero unamjua, kuna watu ambao wapo wanamchango mkubwa tu na hawafahamiki na hao ndio wanamake change. Haya asante sana kwa mtazamo wako. Nikutakie usk mwema

asante the unsung hero wetu jamvini na i think you're missing a point mkuu na unatafuta tu sympathy ya kitoto sana kwa maelezo yako mengi na sijui umeyatoa wapi. na naomba futa kauli yako kuwa nimefurahi watu kufa wakati huna pengine hata uhakika kuwa labda na mimi pia hapo nimefiliwa na mpendwa wangu au wapendwa zangu! hivi ajali zina mwenyewe?
 
Dah! uwiii Mungu Baba tusamehe waja wako. Tuliende na utunusuru na hizi ajari.
Poleni sana ndugu zangu mliopatwa na huu mkasa. Mungu Baba wa mbiguni awatie nguvu na faraja katika magumu mnayopitia.
 
Mpaka sasa sijafahamu kwanini ajali zimekuwa nyingi hivi, kwa kiasi ninaamini kuna kilichojificha nyuma ya hizi ajali. As most pple are saying kuna mambo ya nguvu za giza hapa. Tuombe Mungu kwa kweli atunusuru. Chanzo kilicholipotiwa kwa ajali hii ni Mwendo kasi na utelezi jamani! Tusali kwakweli.
 
Hali zao zinaendelea vizuri. Tuwaweke kwenye maombi.
 
Hawa watoa kafara sijui wanataka kupitia kila jimbo la uchaguzi!!!

Mungu wape uzima waliojeruhiwa na faraja waliofiwa...
 
Imetosha sasa Tanzania ni yetu sote na wasafiri ni ndugu zetu.
 
Hapa dawa ni kuacha mashimo barabarani ili mabasi yapunguze mwendo kipande Dar..Moro siku mbili hiviii..
Ile ajalii ya Majinja ilikuwa sehemu yenye mahandaki kwa hiyo hata hilo sidhani kama ni suluhisho mkuu.
 
ujinga na upumbavu wetu wenyewe sisi wanadamu usitupeleke kuanza kumshutumu illuminati ( shetani ) kuwa yeye ndiyo chanzo cha mara kwa mara za hizi ajali. siyo kweli hata kidogo na nakupinga tena kwa 100%. shetani ndiyo anawaambia abiria " oya wewe dereva hebu nyoosha mguu wako bhana alah " au " dereva tukiwahi kufika tunakokwenda kuna zawadi yako hapa " au " dereva tuwahishe bhana kama huwezi sema tukusaidie " au " dereva usipowahi sikupi dada yangu au sikupi nanihiiii yangu tukifika ". kwa kauli kama hizi unadhani hatutajipanga kweli kila siku kununua majeneza ya mazishi ya wahanga wa hizi ajali.

shetani ni pepo mchafu ambayo humungia mtu yeyote na kuchochea ajali yeyote.
 
Back
Top Bottom