Aiseeh! Washkaji pigeni simu kabla hamjaja maghettoni

Walafi buana yaani swala zima la uchovu wangu na privacy hujaona umeona msosi tu? Watu wa uswazi mna shida sana
Privacy ipo,,ila kwa jinsi ulivyoandika soda ilikuwa moja afu baridi,,,utani bro mwambie msela siku nyingine hasitimbe maghetoni kimya kimya
 
Maana ya neno "Ghetto" ni sehemu wanapo kutana vijana wa kila aina na wasio na uelekeo wa maisha,Ungekuwa unaishi nyumbani kwako usingeona mtu kuja kwako bila taarifa labda iwe emergency.
Nazani ungesikiliza wimbo wa mangwair "ghetto langu tu, linalowazingua madem" ungeondokana na ushuzi wa kuangaika google kutafuta tafsiri za kiitalian mafia. Wakati kila mtu humu kashaelewa ghetto ni nini. Hata kamusi huwa ina badilika tafsiri ya maneno kulingana na wakati na matumizi ya kizazi na kizazi usiwe conservative kila neno unalitafsiri enzi za babu zako.
 
Privacy ipo,,ila kwa jinsi ulivyoandika soda ilikuwa moja afu baridi,,,utani bro mwambie msela siku nyingine hasitimbe maghetoni kimya kimya
Soda siyo ishu nimeiweka tu kuongelea nilivyojiandaa kupumzika zangu watu mmeshadadia msosi mbona mna mawazo ya kimaskini? Sijasema kama msela kafata msosi au hana hela ya kula nimeongelea appointment na privacy
 
instagram,

Pole sana. Naona budget imebana hadi msosi unakuondolea imani/utu. Maelezo yako yanaonesha huna shida na wageni ila tatizo limetokea kwenye chakula. Sasa ili ushinde ilo jaribu, weka chakula mezani tu.
 
Huwa napenda kujiachia nikiwa private sipendi mtu anakuja bila appointment mida nataka kupumzika
duuh kweli jitahidi sana ubadilishe fikra zako mkuu,linapokuja suala la msosi hata kama ni adui yako mkaribishe kwanza mmalize kula ndio mengine yaendelee,kuna siri kubwa sana unapomlisha au kumkirimu mgeni..kuna watu wanaomba wapate mgeni wa kuwakirimu hivo na hawawapati,jitahidi kubadili fikra hizo utaona manufaa yake
 
Marafiki ndiyo watakao kupa michongo ya maisha siyo hiyo loneliness yako.

Washikaji ndiyo watakaochimba kaburi lako na kukuzika siyo hiyo tv na movie yako.

Washikaji hao hao ndiyo watakubeba utakaposhindwa kutembea siyo hiyo tv na movie yako.

Kuchukua kutembelewa na marafiki na washikaji zako ni dalili za uchoyo, kiburi na kujikweza.
Hamna kitu kinakera kama hicho.. Mi ukija kwangu kibwege bwege hata huo mlango sifungui..
 
Wanaokupinga ni waswahili kama huyo mshikaji wako...

Unaanzaje tu kwenda kwa mtu bila kutoa taarifa!!!

Siku ntakuja bila taarofa baada ya kuhakikisha Uko nyumbani kwako mwenyewe. Na hivi nna copy ya ufunguo na password ya kuingia na mahali alarm button ilipo, utastukia niko kwenye kochi, maana ntavizia ukiwa bafuni mie huyoo natoma ndani aahahahahaa
Halafu hapo ndo tutapata majibu kama niwe natoa taarifa au najileta tuu aahahahhaa
Shkamoo Msafiri.

Matata the K.
 
Nakutoa nduki tu...

Thubutuu yaakoooo aahahahhaaa ubavu huo hunaaa, utajikuta wewee ndo umetoka nduki na taulo kiunoni umeniachia crib eehehehehheheee ukirudi unakuta mazagazaga kibao na mie nshasepa.....

Vurugu tuu za Kasinde
 
Kasinde wewe ndio wa kunitoa nduki mimi?

Over my dead body walah
Thubutuu yaakoooo aahahahhaaa ubavu huo hunaaa, utajikuta wewee ndo umetoka nduki na taulo kiunoni umeniachia crib eehehehehheheee ukirudi unakuta mazagazaga kibao na mie nshasepa.....

Vurugu tuu za Kasinde
 
Back
Top Bottom