Aiseeh! Washkaji pigeni simu kabla hamjaja maghettoni

Unatakiwa kujua while wew unahitaji privacy kuna rafiki ako anahitaji kampagn yako. Usiruhusu kuwa mbinafsi hebu Vuta subra akiridhika uwepo wako utaona tu mwenyewe anaondoka.
 
Sio poa kuibuka tu kwa wana. Nimemuelewa mleta mada. Kila mtu na utaratibu wake.
 
Maana ya neno "Ghetto" ni sehemu wanapo kutana vijana wa kila aina na wasio na uelekeo wa maisha,Ungekuwa unaishi nyumbani kwako usingeona mtu kuja kwako bila taarifa labda iwe emergency.
 
Sometimes inabidi ujitolee tu kwa mshikaji. Namaanisha hata kama hauma mood ya story na mtu kwa wakati huo, basi unaitengeneza mood na mtapiga story, then ataondoka basi.

Jua hata wewe kuna siku unampigia mshikaji kwamba unaenda getoni kwake na yeye anaweza kuwa hana mood vile vile ila anakuambia njoo tu, anapiga story na wewe, unaondoka anatulia.
 
Back
Top Bottom