Airtel rekebisheni haraka hii changamoto ya vifurushi vya SMS

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
24,037
71,271
Nianze na hili, Kwa shilingi elfu Moja unapata SMS za Wiki zipatazo 5000 na Kwa elfu 2 unapata SMS za mwezi 9000.

Maajabu, Mmeweka Ukomo wa Kutumia SMS hizo, yaan Kwa siku Mteja wenu atumie SMS 300 tu, kiwe ni kifurushi cha wiki au mwezi.

Tafasiri yake Kwa Mteja wa Kifurushi Cha wiki Sms 300* siku 7=2,100 SMS..... Yaan kifurushi Cha Mteja kitaisha akiwa bado na SMS 2900 kibindoni. Anyway sio inshu sana.

Nije kwa kiini cha Andiko langu kwenu ambalo ndio changamoto Kwa wateja wa vifurushi vyote vya SMS Kwa wiki na mwezi.

Binafsi, nimechaguliwa kua Mwenyekiti wa Kamati ya Harusi ya Rafiki yangu wa Damu, Pilau tunalila miezi michache ijayo.

Hivo nina lazimika kuwasiliana na watu wengi sana.

Kama mjuavyo, Kitanzania Tanzania Pesa inatoka kwa ushawishi, na JUMBE hizi za Harusi Huwa ni gazeti yaani Ndefu.

Nyinyi mnaweka Ukomo wa SMS 300 kwenye kifurushi unachokua umejiunga.

Ninashindwa kufanya kazi yangu ipasavyo, nalazimika kutumia Salio la kawaida.

MAAJABU SASA, hata ukiamua kujiunga Kifurushi kingine Cha SMS, huruhusiwi kukitumia kifurushi hicho mpaka Masaa 24 yapite.

Hii kitu inalazimisha , Nitumie Salio la kawaida Kwa kitu ambacho haikupaswa kuwa hivo.

Yaan Ndani ya Masaa 3 tu, nimeshatumia Vocha ya 6000? Hii ni sahihi?

NAJUA, na inawezekana mmefanya hivi ili kupambana na wazee wa "Ile pesa tuma humu"

Lakini hii sio njia sahihi, na sio jukumu lenu, wajibu wenu ni kutoa Ushirikiano Kwa Wahusika, matokeo ya njia hii kwanza inamuumiza Mteja kifedha, pili, Ukomo wa SMS 300 unamuondolea Mteja uhuru na ni sawa na kuingilia uhuru wa Mteja kimawasiliano, tatu.

Basi hata kama mnaweka Ukomo huo wa SMS 300, mfumo wenu uruhusu Mteja, kujiunga Kifurushi kipya Cha SMS na aweze kukitumia kama alivyotumia kifurushi cha Awali.

WAKUU, Mtandao gani mzuri naoweza kuforward SMS Kwa watu kuanzia 70 Kwa pamoja bila kadhia kama hii ya Airtel?
 
Airtel ni bomu linaloekea kubutuka. Sijui wameelemewa na wateja ama wameshiba lakini wamekuwa na kila aina ya kero.

Si jambo la ajabu mtandao kukata ghafla bila sababu maalum.

Ni kawaida kuwa na MB za kutosha lakini kushindwa ku browse.

Sasa hivi wamekuja na mtindo wa kutotoa taarifa ya matumizi ya 75% ya kifurushi chako kupelekea kupata msg ya ukomo wa kifurushi tu, nikiamini ni mbinu mpya ya wizi wa vifurushi vya watu. Airtel ni mtandao wa ovyo kabisa Tanzania.
 
Mkuu Matatizo unayopitia ndo nayopitia, ila najipa Moyo nikiamin ni changamoto za kieneo.

Kumbe hamna!
 
Acha Uwongo, sawa? SMS 10,000 za Airtel kwa Mwezi ( Siku 30 ) ni Tsh 1,000/= na siyo Tsh 2,000/= kama Ulivyodanganya hapa.
 
Umesahau hili mtandao hauko smooth yaani ukipiga simu kuazia satatu usiku kwakweli nikero tupo unagoma
 
Halotel.

Buku 1 kwa mwezi napewa SMS 6,000.

Nikiweza ata kuzimaliza siku 1 fresh tu.

Usiende TTCL wana mchezo huo huo.
Kwahiyo unataka kusema HALOTEL ni mtandao madhubuti?

Kama jibu ni Yes, kesho nahamia.
 
Airtel ni bomu linaloekea kubutuka. Sijui wameelemewa na wateja ama wameshiba lakini wamekuwa na kila aina ya kero.

Si jambo la ajabu mtandao kukata ghafla bila sababu maalum.

Ni kawaida kuwa na MB za kutosha lakini kushindwa ku browse.

Sasa hivi wamekuja na mtindo wa kutotoa taarifa ya matumizi ya 75% ya kifurushi chako kupelekea kupata msg ya ukomo wa kifurushi tu, nikiamini ni mbinu mpya ya wizi wa vifurushi vya watu. Airtel ni mtandao wa ovyo kabisa Tanzania.
Unawajua tigo wewe?
 
Serikali imeruhusu tuibiwe na kila mtandao unajitahidi kumkamua mteja kadiri ya uwezo wake.
 
Back
Top Bottom