Ukiona mtandao wa simu unakupa sms 10 kwenye kifurushi cha 1500 au 2000 ujue hali ni mbaya

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,729
2,082
Salam, mambo ni mengi kwa sasa tuendelee tu

Hii mitandao ya mawasiliano sàsa naona kama iko taabani. Inaonekana inapumulia mashine ya gesi ila yanajikaza kisabuni.

Yaani sms za kuhesabu sàsa hivi tofauti na zamani.

Huwa nikijiunga kifurushi huwa siangalii sms ziko ngapi, huwa najua zipo tu kwa sababu kifurushi huwa hakipungui buku jero cha wiki.

Sàsa jana nataka nimtumie mtu msg nashangaa inagoma.

Narudia narudia naresend naresend inarudi .Sàsa najiuliza mbona kifurushi nimeweka juzi tu cha wiki ina maana kimeisha.

Kuja kuangalia msg ya kifurushi kumbe nimepewa sms 10 tu. Sasa nimezitumia zimeisha.

Sàsa nashangaa ina maana sàsa hivi hali imekuwa ngumu namna hii kwa haya makampuni hadi sms tunapewa za mafungu kama ya nyanya halafu isitoshe tozo nasikia zimeondolewa ila sina uhakika maana sina taarifa rasmi sàsa inakuwaje kweli kampuni ya simu mnatoa sms 10 tu jamani huu kweli ni uungwana?

Mi najua siku zote kuwa sms sio dili kwenu kumbe sàsa hivi mteja unapewa kwa kuhesabiwa hatari sana.

Kama ndio hivyo basi hawa jamaa wa DP Welders wataingia sehemu nyingi sana yetu macho ngoja tusubiri tuone.
 
Kuna vifurushi maalumu vya meseji kwa mwezi mzima kwa shilingi 1000 tu unapata meseji 5000 za kutumia siku 30

Kuna vifurushi havina kikomo cha muda wa matumizi kupiga simu mitandao yote.

Mimi naona ni namna ya wewe kufanya uchaguzi wa vifurushi kuendana na matumizi yako.

Wanaumiza kwenye bando za intaneti,huku kwakweli mambo magumu sana .wanatuumiza mno.
 
Kuna vifurushi maalumu vya meseji kwa mwezi mzima kwa shilingi 1000 tu unapata meseji 5000 za kutumia siku 30

Kuna vifurushi havina kikomo cha muda wa matumizi kupiga simu mitandao yote.

Mimi naona ni namna ya wewe kufanya uchaguzi wa vifushushi kuendana na matumizi yako.

Wanaumiza kwenye bando za intaneti,huku kwakweli mambo magumu sana .wanatuinia mno.
Tigo hawa
 
Back
Top Bottom