DOKEZO Aina mpya ya mianya ya rushwa na upigaji ya watendaji wa TANESCO

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Wakuu , heshima mbele.

Niende moja kwa moja kwenye mada.

Kiukweli TANESCO hili shirika unaweza kudhani pengine tukibadili viongozi wa juu ndio inaweza kuwa mwisho wa matatizo ila pengine naona labda tuanzie kwenye "grassroots"

Ipo hivi, baada ya kufanya ombi la umeme kupitia mfumo surveryor alifika japo kwa mizengwe akafanya makisio yake na akaondoka.

Ikapita takribani mwezi mzima na juma moja kamili , huku surveryor akiwa hapokei simu kabisa hata ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) hakuwa akijibu.

Jukumu la kutinga ofisini kwao ndio lilifuata, ajabu ni kuwa surveyor alipopigiwa na boss wake mmoja pale alipokea na kusema "amepoteza daftari alilokuwa amewaandikia wateja hivyo atafanya mpango wa control number baadaye"

Hiyo ikapita , control number ikaja yenye malipo ya 320,960/= ambayo nililipa siku hiyo hiyo.

Ikapita tena wiki nikaona nitinge ofisini, huku hapo ninaelekea miezi 2 tangu zoezi la surveying lifanywe , zikapita siku 3 mafundi walikuja na zana zao ,walipoangalia mchoro wakasema hapa inahitajika nguzo wakawa wameondoka.

Zoezi lililofuata ni kutinga tena ofisini nikafika pale huduma ni mbovu sana unakaa kwenye waiting bench watu wanajipitisha ofisini na kupiga soga zisizo na tija, nikasogelea meza moja kuuliza na kuelezea tatizo akapelekewa mtaalam mmoja akasema kiukweli hapa ilihitajika nguzo na sijui surveyor huyu alijisahau vipi nikasema sema je gharama itakuwa kiasi gani katika ongezeko la pesa niliyolipa awali?

Nikajibiwa itakuwa 515,617.62 hivyo ukitoa 320,960 utapata 194,657.62, nikawaambia sawa malipo yatafanyikaje?

Nikaambiwa hii haitolipwa kwa control namba, nikabaki na mshangao nilipouliza sana kwanini isilipwe kwa control number pia kama awali?

Nikajibiwa hata hivyo huwezi kupata nguzo hivi karibuni hatujui nguzo zitakuja lini maana "material za kutengenezea nguzo zimeisha"

Nilikuta watu 4 na mimi nikaongezeka kuwa 5 kwenye kadhia hii ya uzembe na kutengeneza mianya ya rushwa ya wazi wazi.

Niliondoka ofisini na baada ya kupata safari za kikazi hapa sijaweza kufuatilia tena, sasa najiuliza kwenye ngazi huku ya chini kupo namna hii je hata tukiweka waziri malaika kuna nafuu tutapata?

Nani muhusika wa kutoa nguzo na pesa za malipo ya nguzo?

Hawa masurveyor wanapatikana vipi , ni miongoni mwa wafanyakazi wa TANESCO au ni day worker?

Mwenzangu mmoja alidai hata mafundi walipokuwa wanakuja site walitaka awalipie usafiri , je shrikika limeacha kutoa posho za kazi ya siku hadi mtu achangie karibu 10, 000 ili mafundi waje wamuunganishie umeme?

Hawa watu iwe ni surveyors na mafundi wanawajibishwa/wanawajibika kwa nani kwa kulikosesha shirika mapato waziwazi hivi?

Pendekezo: Nadhani mfumo wa kuunganishwa umeme wa Nikonekt uboreshwe na kila hatua ya kuanzia ombi la umeme, kutolewa control number, siku ya mafundi kuja sehemu husika , na rekodi ya malipo yote iwe inatunzwa kule kule.
 
Hakuna shirika hovyo Tanzania kama TANESCO, hata sielewi Kwanini serikali hailibinafsishi? Kuna sehemu walismika nguzo Msongo mkubwa, wakaweka na umeme lakini huu ni mwaka wa tatu watu hawajasambaziwa umeme kwenye eneo Hilo, upepo ukija au matawi ya miti yakidondokea zile nyaya zikagongana ni mwendo wa kugonga shoti tu. TANESCO hovyo kabisa. Mbunge wa eneo Hilo alikuja akaelezwa tatizo Hilo lakini alipoodoka hakurudi.
 
Back
Top Bottom