DOKEZO Rushwa kwa Watumishi wa TANESCO (surveyors) Kongwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Ukiniambia hapa hakuna mazingira ya RUSHWA BASI NASTAHILI KUWEKWA HOSPITALI YA AKILI MIREMBE.

Iko hivi:

Niliomba kupatiwa huduma ya umeme mara mbili na kupewa nambali hizi kama rejea ya maombi hayo 1. 2907220637 ambayo mpaka leo haijarejesha majibu na 2. ikawa 2112220335 ambayo nayo hadi sasa haina matokeo yoyote.

Surveyor mwenye namb ya simu 062.....80 aliyetumwa mara zote alitamka kuwa TANESCO INAANDAA MPANGO WA WATEJA WA REA WATACHANGIA AMA NGUZO AU WIRE jambo hili nilimwambia HALIKO KATIKA NCHI HII labda uniambie kitu kingine.

Niliwasiliana na TANESCO wakati ule kwenye ukurasa wa TWITTER na nikaambiwa eti Bado TANESCO haijapata miundo mbinu ya kupeleka umeme mahali ilipo nyumba yangu
pamoja na kuwa meter 25 toka ilipo nyumba yangu ipo nguzo inayo-supply umeme kwa jirani.

KAMA maombi haya ni ya kutoka 2021 na hadi sasa hakujapatikana huduma ya umeme kwangu na si kuwa nanyimwa huduma ili nitoe MLUNGULA basi nitakuwa mgonjwa wa Mirembe.
 
siwatetei TANESCO lakini mimi nilitumia nikonekt kutuma maombi na ndani ya siku 9 nilishaunganishwa na huduma.
Ni kweli kabisa Tanesco kwa namna fulani wamerekebisha sana mifumo yao. Mimi kwangu zilihitajika nguzo mbili na ndani ya mwezi mmoja nikaunganishiwa umeme na hapo nilichelewa mwenyewe kufanya malipo kutokana na changamoto zangu binafsi.

Sijajua mazingira alipo mdau huyu mpaka mizunguuko inakuwa mingi hivyo!.
 
KAMA maombi haya ni ya kutoka 2021 na hadi sasa hakujapatikana huduma ya umeme kwangu na si kuwa nanyimwa huduma ili nitoe MLUNGULA basi nitakuwa mgonjwa wa Mirembe
Na hilo ni jimbo la spika aliyeng'atuliwa fikiria majimbo yasiyo na spika kutakuwaje
 
Nliambiwa nguzo hakuna kwa miezi4 siku moja nikaenda nikiwa nimepiga simu kwa kiongozi na imeshuka simu kutoka hq tanesco bila wao kujua wakaniambia tena hakuna nguzo wakati jirani yangu opp na mm alijenga nyumba nyuma yangu alikuwa keshawasha umeme.

Kwa rushwa ya laiki moja. Ile ntoka getini niondoke nikapigiwa simu kujulishwa niwepo nyumban8 wanakuja kufunga umeme. Nliwacheka sana walivokuwa wanafunga.
 
Labda sio sehemu zote. Mimi niliutumia NIKONECT hazikuisha wiki mbili nguzo ipo mlangoni. Ni hapa Moshi mjini lakini kwa msaada wa afisa mmoja mstaarabu sana anaitwa Godfrei.Alinipa maelekezo hatua za kufuata kupitia huo mfumo. Ni rahisi sana na unapunguza urasimu.
 
Tanesco wakuda.

Mwaka 2018. Walimgomea kufungua umeme mama x. Na wale vibarua wakamtamkia maneno ya shombo walipomuomba laki mbili.

Mama x akampigia simu x, x ni mke wa mdogo wake magu. Mdogo wake magu akamuwakia kalemani na kalemani akamuwakia meneja wa mkoa.

Ndani ya nusu saa zilikuja gari tatu zinafukuzana. Fuso limebeba nguzo mbili, kluza la emergency na lingine la meneja wa mkoa.

Walipofika wakafanya wayaringi upya na kumuwashia umeme chini ya usimamizi wa RM.

Majirani wote waliwashiwa umeme siku hiyo na nguzo zilipopelea zilifuatwa wilaya jirani.
 
Back
Top Bottom