Pongezi kwa TANESCO Dodoma

Steph JK

Senior Member
Sep 14, 2018
103
106
Habari,

Achana na tatizo la umeme hilo lipo nchi nzima. Hapa natoa pongezi kwa maboresho yaliyofanyika kwenye suala la kuomba kuunganishiwa huduma ya umeme. Inawezekana maboresho yapo nchi nzima lakini mi naomba nizumngumzie na niwapongezi wale walionihudumia na nikarishika.

Niliomba kuunganishiwa huduma ya umeme kupitia mfumo wa Nikonekti, baada ya kujaza taarifa zangu binafsi na mtaalamu wangu wa umeme kuingiza taarifa za jengo na wiring na kuziwasilisha Tanesco ilinichukua siku tano za kazi hadi kuunganishiwa huduma ya umeme.

Ilinichukua siku moja mafundi kufanya survey, katika hatua hii nilipogiwa simu na fundi bahati mbaya nilikuwa mbali nikatafuta mtu anayepajua akampeleka surveyor , alifika na akafanya kazi. Nilijaribu kutafuta mazingira ya kutoa chochote ili jamaa akimbize kazi yangu lkn haikuwa hivyo, jamaa alichomoa.

Baada ya kufanya survey mfumo Nikonekti ulikuwa unanionesha status zote zilizofikiwa kwamba survey imefanyika sasa inaandaliwa bill na control namba. Baada ya siku moja nikapewa bill na control namba, nikalipia na siku ya tatu baada ya kulipia nilifunguwa hudama ya umeme.

Hivyo ndani ya siku 5 niliunganishiwa na huduma ya umeme bila kutoa rushwa ya aina yoyote aidha nilipata huduma kama hiyo kwa mkoa mwingine na kwa miaka iliyopita nilitoa sana hela na kumbembeleza surveyor kuja kufanya survey, mtoa control number alikuwa kama Mungu mtu, safari za kutosha katika ofisi za Tanesco na bado nikaunganishiwa ndani ya miezi miwili ila sasa sijawahifika tanesco, status ya application yangu nilikuwa naipata muda wote, sikutoa hata shilingo moja na bado nimeunganishiwa umeme ndani ya siku tano za kazi.

Hongera sana Tanesco boresheni na upatikanaji wa umeme sasa
 
Nimelipia kupitia nikonnect mwezi umepita hakuna kitu
Habari ya wakati huu ndugu mteja Tunafurahia kukuhudumia, tafadhali tunaomba namba yako ya ombi la kuunganishiwa umeme (Application number) kwa ufatiliaji na hatua zaidi.^EB
 
Habari ya wakati huu ndugu mteja Tunafurahia kukuhudumia, tafadhali tunaomba namba yako ya ombi la kuunganishiwa umeme (Application number) kwa ufatiliaji na hatua zaidi.^EB
Ahsante sana, jambo la msingi ni Tanesco kuwa na KPI mteja akilipa afungiwe baada ya siku ngapi?
Sio jambo la msingi kila mtu aje aseme nimelipia lini au kutoa namba wakati system inaonyesha. Kama kuna shida toeni taarifa sasa hatupokei pesa hatuna vifaa sio kuwafanyia utapeli wananchi mwishoni mnaanza kuwaomba rushwa.
 
Back
Top Bottom