Rum 3:23-26
kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake, ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa; apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu.
Maoni yangu.
Anayejua akina nani wataenda na akina nani hawaendi Mbinguni ni Mungu mwenyewe.
Sisi jukumu letu ni kumuamini Mungu na Yesu Kristo huku tukitenda yaliyo mema na kuishi kwa mapenzi na mwongozo wa Roho Mtakatifu.