Aina hii ya Wanawake ni kama Kutafuta Nyoka mwenye Miguu

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,744
Mwanamke
1. Mzuri wa Sura
2. Mzuri wa Umbo
3. MWENYE AKILI?

Ni nadra sana hasa miaka yetu hii. Nahangaika sana nipate mwanamke wa namna hiyo. Inakuwa changamoto.

Unakuta dada mzuri wa umbo na sura lakini kichwani.... Empty. Unaumia sana kuwa huyu si anaweza hata kukuambukiza upumbavu?

Miaka hii.. sijui ni kutokana na aina ya vyakula tulavyo...watoto wanazaliwa wazuri sana hasa mabinti. Lakini kichwani kumejaa tu mayonnaise hamna kitu.

Sisi wengine tunabaki tu tunaumia. Maana pia shida inakuwa kubwa wenye akili nao hawazaani sana ukilinganisha na hawa wengine...

NIMPATE WAPI MWANAMKE MZURI WA SURA,UMBO NA MWENYE AKILI (MZURI WA TABIA)? Nimpate wapi mimi Chizi Maarifa?
 
Nashukuru me ninae wa hivyo vigezo hata yule aliopita alikuwa na hivyo hivyo vigezo tulishwandwana kitu moja tu ikapelekea mahusiano yetu kuvunjika ni kwenye upande wa dini Wazazi wake walikuwa na vikwazo Sana kwasababu nilikuwa ni mkristo baba yake alinitisha niachane na mtoto wao wa kislamu ila kabla ya huyu wasasa na aliyopita nilikutana na mabinti wasiokuwa na akili wengi ambao wapo kimaslahi Sana kama unaowalalamikia.

Nakushauri ndugu yangu we endelea na kubahatisha hivyo hivyo ipo siku utampata huyo demu mwenye mahitaji unayotaka
 
Wapo ila kukutana naye na kumpata inahitajika neema!

Halafu huwa ni wagumu sana kuridhia kuingia kwenye mahusiano!

Lakini akikuridhia na kukupa nafasi moyoni mbona utafurahi
Mwenyewe!

Kuwapata inahitajika subira yakutosha.
 
Wa hivyo huwa hawaji expose kuwatega wanaume ili wawatake.

Sio watu wa tamaa na kunia makubwa kuliko wawezavyo.

Ni watu wa kuridhika na hali zao kuliko tamaa ambao huzani inaweza kuwaweka under high risks.

Hupenda kujiweka at low profile.
 
Wapo kibao kama unapenda wenye sifa hizo na umri mdogo nenda katege udbs pale udsm

Kama unapenda wakubwa wenye sifa hizo nenda katege kampuni za auditing big 4.. uone pisi kali zenye akilii kubwaaa..

Ila mpaka uwapate uwe na wewe akiliii kubwaa na pesaa mingiiii
 
🤣🤣🤣usipokuwa makini utaambukizwa upumbavu,uwe makini mkuu!

Ila wanawake wameumbwa kwa ajili ya kutuzalia watoto tu mkuu na Wala siyo Mambo mengine,kwa hiyo Mambo Kama umbo na sura achilia mbali akili ambazo wanawake wote hawana,tuwaheshimu Ni mama zetu,Wana mchango mkubwa Sana katika kuifanya dunia ikamilike.
 
Hao ni aina ya wanawake ambao kutokana na altitudes za misingi ya malezi na makuzi yao hawawezi kumuomba Mwanaume hela hata kidogo.

Ni kitu kigumu kwao kumuomba hela Mwanaume yeyote labda baba yake mzazi ikiwa anahaja ya mahitaji yake.

Wanawake wa aina hiyo huamini kuwa kumuomba hela Mwanaume ni tabia ya kimalaya.
 
Back
Top Bottom