Aibu Kubwa Baada ya Moto Kuzuka Kwenye Danguro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aibu Kubwa Baada ya Moto Kuzuka Kwenye Danguro

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Msharika, Mar 22, 2010.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  [​IMG]
  Memeth J akificha sura yake baada ya moto kwenye danguro alilokuwemoSunday, March 21, 2010 7:06 PM
  Moto uliozuka kwenye danguro la mashoga nchini Uswizi ulisababisha wateja wa danguro hilo wakimbie uchi kunusuru maisha yao.Mmoja wa wateja wa danguro hilo aliyetajwa na gazeti la Blick la Uswizi kuwa jina lake ni Memeth J, alilazimika kuning'inia kwenye dirisha akiwa uchi huku akificha sura yake wakati akisubiri zimamoto waje kumuokoa.

  Tukio hilo lilitokea kwenye danguro moja mjini Basel nchini Uswizi ambapo mashoga hujiuza.

  Memeth ambaye anakataa kuwa yeye pia alikuwa mteja wa danguro, alijitetea kuwa alienda kwenye danguro hilo kumtembelea rafiki yake wa miaka 10, Tamilo H ambaye ni shoga anayefanya kazi kwenye danguro hilo.

  Memeth aliliambia gazeti la Blick kuwa alikuwa akijirusha na shoga huyo kwenye danguro hilo kabla ya kupitiwa na usingizi na kuzinduka danguro hilo likiwa limeshika moto.

  Memeth alilazimika kukimbilia kwenye korido ya danguro hilo huko akiwa uchi lakini huko alikutana na kundi la waandishi wa habari na wapiga picha wakiwa pamoja na zimamoto.

  Hali hiyo ilimfanya Memeth akimbilie kwenye dirisha na kuacha makalio yake nje huku akificha sura yake kwa kutumia pazia. Alikubali kuondoka kwenye dirisha hilo baada ya zimamoto kumhakikishia kuwa wataendelea kuificha sura yake.

  "Nafikiri ndugu zangu hawatanitambua kwa kuangalia makalio yangu", alisema Memeth akiliambia gazeti hilo.

  "Familia yangu haijui kuhusiana na tabia yangu hii ndio maana nimelazimika kuificha sura yangu", alisema Memeth ambaye alisema ana umri wa miaka 33.
   
 2. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kazi kweli kweli.
   
 3. Jerome

  Jerome Senior Member

  #3
  Mar 22, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii inaonyesha wazi siku za mwisho zimekaribia na ahera nyingine inaanzia hapahapa duniani
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,468
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha ha
  mungu bana,anajua jinsi ya kuwaumbua watu
   
 5. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Na sijui huyo mkewe akiyaona hayo makalio itakuwaje.
   
 6. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  [​IMG] sawa ila hii avatar yako, na wewe duh sijui una umri gani,
   
Loading...