Meli ya mafuta yawaka moto baada ya shambulio la kombora Houthi

Didododi

JF-Expert Member
Jul 21, 2023
321
426
Meli ya mafuta inawaka moto katika Ghuba ya Aden, mwendeshaji wake anasema, baada ya wapiganaji wa Houthis kusema waliishambulia kwa kombora.

Kundi hilo la Yemeni lilisema lililenga meli hiyo kwa jina Marlin Luanda siku ya Ijumaa jioni.

Opereta Trafigura aliambia BBC kwamba mashambulizi yalisababisha moto katika tangi moja la mizigo la meli hiyo na vifaa vya kuzima moto vilikuwa vikitumiwa kuuzuia.

Jeshi la Marekani lilisema kuwa Wahouthi waliipiga meli hiyo kwa kombora la balestiki .

Hakuna majeruhi walioripotiwa, Kamanda Mkuu wa Marekani alisema katika taarifa.

Ni shambulio la hivi punde zaidi dhidi ya meli za kibiashara na Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran ndani na karibu na Bahari ya shamu.

Kundi hilo linasema kuwa linalenga meli katika eneo hilo kuwaunga mkono Wapalestina huko Gaza, ambako Israel inapambana na Hamas.

Marekani na Uingereza zimeanzisha mashambulizi ya angani dhidi ya wahouthi kujibu, Katika taarifa yake, msemaji wa Houthi alidai kuwa Marlin Luanda ilikuwa meli ya Uingereza na ililengwa kujibu "uchokozi wa Marekani na Uingereza dhidi ya nchi yetu".

Meli hiyo ya mafuta inapepea chini ya bendera ya Visiwa vya Marshall na inaendeshwa na Trafigura - kampuni ya biashara yenye kampuni katika maeneo 50 duniani kote ikiwa ni pamoja na London.

Serikali ya Uingereza ilisema mashambulizi dhidi ya meli za kibiashara "hayakubaliki kabisa" na kwamba Uingereza na washirika wake "wanahifadhi haki ya kujibu ipasavyo".
#BBC
 
Back
Top Bottom