Aibu jeshi la polisi kuwa na virungu vya kunyanyasa CHADEMA-Deo Fulikunjombe

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mbunge wa Njombe Deo Fulikunjombe ameshangazwa na jeshi la polisi kutokuwa na vifaa vya kisasa na kulikejeli kwamba jeshi hilo sasa lina virungu tu ambavyo vinatumika kukandamiza Chama cha Demokrasia na maendeleo-CDM.
Nanukuu maneno ya Fulikunjombe aliyotamka:
''Aliitaka Serikali kuongeza fedha zaidi ili kuliwezesha Jeshi la Polisi kununua silaha za kisasa: “Polisi hawana silaha zozote kuwawezesha kupambana na uhalifu na badala yake limeachiwa virungu ambavyo huvitumia kupigia wanafunzi, wakati wa migomo na maandamano ya Chadema,” alisema Filikunjombe.

Source:Mwananchi
 
Kweli huyu mwanamama aliichamba sana serikali na zaidi nilimuona kama anajipendekeza kwa jeshi la polisi ,ila aelewe polisi bado ni chombo cha CCM ,hivyo kama anataka kulilipapatua jeshi hili liachane na CCM ni bora akalikandia nakuonyesha sehemu ambazo polisi wametumika kama nguzo ya CCM,na sivinginevyo.Awambie polisi wajitahidi kuikimbia CCM au wakati utakuja kuwakumu ,wakati ambao CCM watakuwa benchi au haipo ,kesi za kuwashitaki polisi zitakapofumka.
 
Tanzania kuna Genge la vilaza walioajiriwa kulinda usalama wa CCM na makuwadi wao. Lifie mbali.
 
Mmomonyoko sio mmomonyoko kama hakuna athari kwenye ardhi, Je mmomonyoko wa kisiasa utakosa athari?
 
Kichaa mmoja aliziwasha nyiti zote za kiberiti, moja baada ya moja, ili kuhakikisha kama ziko katika hali nzuri. Alipomaliza akasema, "Barabara!, zote ni nzima."

Kwa hivyo mimi nashauri bora wabakiwe na hivyo hivyo virungu, wakiununuliwa silaha mpya watataka kuzijaribu juu ya miili yetu.
 
Mbunge wa Njombe Deo Fulikunjombe ameshangazwa na jeshi la polisi kutokuwa na vifaa vya kisasa na kulikejeli kwamba jeshi hilo sasa lina virungu tu ambavyo vinatumika kukandamiza Chama cha Demokrasia na maendeleo-CDM.
Nanukuu maneno ya Fulikunjombe aliyotamka:
''Aliitaka Serikali kuongeza fedha zaidi ili kuliwezesha Jeshi la Polisi kununua silaha za kisasa: "Polisi hawana silaha zozote kuwawezesha kupambana na uhalifu na badala yake limeachiwa virungu ambavyo huvitumia kupigia wanafunzi, wakati wa migomo na maandamano ya Chadema," alisema Filikunjombe.

Source:Mwananchi
Naona ana hamu ya kung'olewa meno bila ganzi....
 
Kweli huyu mwanamama aliichamba sana serikali na zaidi nilimuona kama anajipendekeza kwa jeshi la polisi ,ila aelewe polisi bado ni chombo cha CCM ,hivyo kama anataka kulilipapatua jeshi hili liachane na CCM ni bora akalikandia nakuonyesha sehemu ambazo polisi wametumika kama nguzo ya CCM,na sivinginevyo.Awambie polisi wajitahidi kuikimbia CCM au wakati utakuja kuwakumu ,wakati ambao CCM watakuwa benchi au haipo ,kesi za kuwashitaki polisi zitakapofumka.
Deo Filikunjombe sio mwanamama!
 
Kichaa mmoja aliziwasha nyiti zote za kiberiti, moja baada ya moja, ili kuhakikisha kama ziko katika hali nzuri. Alipomaliza akasema, "Barabara!, zote ni nzima."

Kwa hivyo mimi nashauri bora wabakiwe na hivyo hivyo virungu, wakiununuliwa silaha mpya watataka kuzijaribu juu ya miili yetu.
Kama gongo la mboto.
 
Kawapa live za uso!ni vile alikuwa polisi anajua vema namna wanavotumika kudhibiti wanasiasa tu wa upinzani
 
Deo mwanasiasa makini hataki kuingia kwenye historia ya siasa za majitaka ya chama cha mabwepande.
 
Kweli huyu mwanamama aliichamba sana serikali na zaidi nilimuona kama anajipendekeza kwa jeshi la polisi ,ila aelewe polisi bado ni chombo cha CCM ,hivyo kama anataka kulilipapatua jeshi hili liachane na CCM ni bora akalikandia nakuonyesha sehemu ambazo polisi wametumika kama nguzo ya CCM,na sivinginevyo.Awambie polisi wajitahidi kuikimbia CCM au wakati utakuja kuwakumu ,wakati ambao CCM watakuwa benchi au haipo ,kesi za kuwashitaki polisi zitakapofumka.

mbona unamtukana mwanaume mwenzio kwa kumuita mwanamama?

Kumbe jeshi la polisi ni mali ya ccm,asante kwa taharifa hii nzuri!
 
Back
Top Bottom