Jeshi la Polisi, JWZ na Usalama wa Taifa huu ni muda wa kuiamini CHADEMA

Poa 2

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
1,294
1,288
Nawasalimu wote

Leo nitawasilisha hoja yangu kwa njia ya shairi.

CHORUS
Tunakushukuru wananchi wanatuamini,
Jeshi la polisi tunaomba mtuamini
Usalama wa taifa tunaomba mtuamini
Ohoo ohooo CHADEMA

Wadau wa maendeleo mtuamini
Taasisi za kimataifa mtuamini
Taasisi za kidini na NG'Os mtuamini
Ohoo ohooo CHADEMA

VERSE 1
Tutajali utu, haki pamoja na maendeleo
Utawala Bora,uwajibikaji na demokrasia
Tutatoa fursa za kiuchumi bila upendeleo
Ajira kwa vijana kwa nguvu tutalipigania
Amani haitovunjika kamwe
Visasi havitakuwepo kamwe
Hatutauana sababu ya kukosoana
Tutajenga nchi yenye umoja na mshikamano
Tutaudumisha upendo na wetu muungano
Kero tutatatua kwa maelewano na mapatano

CHORUS
Tunashukuru Wananchi wanatuamini
Jeshi la polisi tunaomba mtuamini
Usalama wa taifa tunaomba mtuamini
Ohoo ohooo CHADEMA

Wadau wa maendeleo mtuamini
Taasisi za kimataifa mtuamini
Taasisi za kidini na NG'Os mtuamini
Ohooo ohooo CHADEMA

VERSE 2
Tanzania si kisiwa inaihitaji dunia
Kuliko Dunia inavyoihitaji Tanzania
Tutashirikiana na yeyote Mwenye Nia njema
Miradi yenu itakuwa salama enyi wakezaji
Zaidi tutaboresha sera Ili ziwavutie wengi
Tutaupinga ubaguzi wa dini ama rangi
Tutailinda katiba na kuheshimu mikataba
Kupambana na ugaidi mabadiliko ya hali ya nchi
Haki za binadamu tutazilinda kama pochi

NB. CHADEMA ni watanzania ikiingia madarakani itawahitaji polisi itawahitiji wanausalama na jumla Kila mtanzania na fani yake. Amani, upendo na furaha vitajaa mioyoni mwa wananchi.

2025, Tunaomba ridhaa yenu wananchi tubalishe maisha yenu Hawa wenzetu ccm wanatupeka kwenye maendeleo madogo kwa mwendo wa kinyonga na wametuchelewesha saana.
 
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikiamua mabadiliko yatokee na siasa safi na uongozi bora unakuwepo YAWEZEKANA.
Wao ni kuwakatalia CCM kutumika kwenye siasa maana madhila ya matatizo ya nchi hii hata wao, familia zao na ndugu na jamaa yanawagusa.
 
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikiamua mabadiliko yatokee na siasa safi na uongozi bora unakuwepo YAWEZEKANA.
Wao ni kuwakatalia CCM kutumika kwenye siasa maana madhila ya matatizo ya nchi hii hata wao, familia zao na ndugu na jamaa yanawagusa.
Ni kweli tupu umeandika nakushukuru sana
 
Back
Top Bottom