Aibu hii huyu mume ataiweka wapi?

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,832
NDANI YA CHUMBA CHA BINTI WA KAZI [house girl]

Baba anavamiwa na pepo wa ngono anajikuta anawaka tamaa kwa binti wa kazi ambaye ni kama mtoto wake wa kumzaa.

Baada ya hiyo hali kumchosha house girl akaona isiwe tabu wacha akae na mama amueleze yote yanayoendelea baina yake na baba ili kunusuru ndoa ya huyu mama.

Ilikuwa ni jioni kama ya saa 9 alasiri
mama akijianda kwenda kwenye ibada,binti akatoka chumbani akamwambia mama

"Samahani mama naweza kuongea nawewe kitu sasa?"

"Ndiyo ondoa shaka japo niko na ratiba ya kwenda ibadani"alijibu mama

"Mama,baba ananitongoza ananitaka kimapenzi,sasa ni kama mwezi mzima sasa,

Siku ya kwanza nilidhani amepitiwa tu lakini inavyoonekana amedhamilia....

naumia nakosa amani hasa nikimwangalia baba na mimi naona kabisa ni kama baba kwangu,au babu yangu kabisa.nisaidie mama nakosa sana amani nikiona SMS zake kwenye simu yangu,

nakuheshimu na namuheshimu sana baba,sitaki tuje kuingia ugonvi na wewe mama mimi nafanya kazi hapa kwa malengo makubwa,sitaki nije nipoteze kazi kwa mambo ya kipumbavu......

na isitoshe pia mimi nina mchumba ambaye nilishamwambia ikiwa yuko sirious aje nyumbani awaone ninyi kama wazazi wangu mnaonilea.....na tangu nipoteze wazazi wangu naona kama majeraha yangu yameshapona kwa sababu Mungu amenipa wazazi wanaonijari na kunitimizia mahitaji yangu muhimu.....

"Binti alimweleza mama kwa hisia kali sana huku akionyesha kulengwa na machozi....."Naomba usinifukuze mama nakuomba!"

Mama alijikuta anampenda sana yule binti

Na yeye akajikuta analengwa na machozi akachukua muda wa kufkir kama dakika 10 pasipo kusema chochote

Binti akamwonyesha kila kitu kwenye simu yake

Mama akaona msg za ajabu na za aibu toka kwa mumewe.....akamhurumia,akajisemea moyoni

" hivi hawa wanaume wanataka nini jamani?"
Ni kitu gani kakikosa kwangu ambacho msichana wangu anavyo?
Nimemkosea nini hasa??

Basi kwa unyonge mama akaona hana hata hamu ya kwenda ibadani, akamjibu yule binti "ntaanzaje kukufukuza Mwanangu! Nakuhakikishia kwamba siwezi kukuondoa,mpaka pale utakapotimiza malengo yako.....

Baada ya muda mama akaona hakuna haja ya kwenda hata ibadani wakati tayari ako na shida moyoni mwake,akaingia chumbani kwake akawa amejipumzisha akifikiria mambo mengi yahusuyo ndoa yake......akajisemea " kwanini shetani anataka tumalize vibaya kwenye ndoa yetu?"

SAA za jioni msichana akapokea message toka kwa mzee:

"usiku nitachelewa kuingia na kabla sijaingia chumbani ntakuja kwako usifunge mlango sawa!"

Ilikuwa ni text iliyoingia kwenye simu ya binti

Moja kwa moja akampelekea mama kumwonyesha ili wajue wanafanyaje maana ni mtihani mzito kwa house girl.......

Lkn mama akamuuliza kama anaweza kumwachia ile simu kwa muda ule akae nayo chumbani kwake, binti akasema hakuna shida na mama akaingia nayo kuchat na mumewe.

Ile SMS iliyotoka kwa mumewe akaijibu akasema
[Hakuna shida]

Mzee akajibu;
{Ngoja nimwandikie wife sms kama ntachelewa,nikuletee zawadi gani mwanangu?}

Mama akijibu;
[Niletee skin tite]

{Size gani?}

[Kama anazovaa mama tunavaa size moja]

{Sifahamu anavaa size gani sijawahi kumnunulia}
[Haaaaaa!baba hujui size ya mkeoooo are you sure?]

Kukawa na ukimya kidogo mzee nafkir akashtuka kuona zile chatting utafkir ni mkewe akaruka hewani ili ajiridhishe.........

mama haraka akamwita binti akamwambia pokea mwambie mama yupo saizi tuendelee kuchat.....akafanya hivyo na mzee akakata.

Akamwendea Whatsap mkewe akamwandikia ujumbe

"Ntachelewa kurudi Leo kuna mpira wa Manchester na arsenal unaisha saa 6:45 mkewe akaijibu haraka akasema"sawa mume wangu"

Akarudi kuchat na house girl fake na hajui kama simu zote ziko na mkewe

{"Ndio sijui size ya mke wangu kwani lazima?}

Mama akamtajia size yake ya tait.

Usiku saa 4 na nusu,jamaa akamwandikia message anaedhani ni msichana wake wa kazi akisema
"Dakika 10 ntakuwa hapo acha mlango wazi"

Mama akajibu "poa" akaenda kufungua mlango akaingia chumbani kwa msichana wake kulala akimsubiri kwa hamu kubwa mumewe akazima taa akaingia ndani ya neti akajifunika shuka........wakati huo binti usiku huo amelala chumba cha wageni.

Saa tano kasoro dakika 20 mzee akafika,akafungua mlango wa nje taratiibuuu akaanza kunyata akiingia chumbani kwa house girl kuvunja amri ya 6 {usizini}

Alipofungua mlango kwa taratibu sana,akaufunga kwà ndani akachojoa nguo zote akitumia mwanga wa simu akaingia ndani ya neti akazima simu yake akaingia ndani ya shuka.....

Haraka haraka akatua mkono wake kwenye kiuno cha mkewe

Mh!ni kama alishtuka kidogo baada ya kuona matuta fulani kiunoni,akaanza kupapasa mkono wake ukatua kwenye maziwa ya mkewe.....hapo ndipo alipochoka.....maana aliona yale maziwa yamelala kabisa kama ya mkewe.......alikuwa ameshajua tayari kwamba amewekewa tego,stim zote zikawa zimekata ni mdogoo kama piliton......

Na mkewe baada ya kuona jamaa kashtukia ishu
Akaanza nae ukorofi wa kumpapasa mumewe huyo halali......jamaa alikuwa ameshanyong'onyea kila kiungo kimelala hakuna ushirikiano wowote!

Sikiliza neno la mzee kwa mkewe "habari za leo mke wangu?

"Salama mume wangu kuwa huru,hapa huibi uko na mkeo halali twende kazi".alijibu mama kwa sauti ya mahaba.....vp mpira umeisha,nani kaibuka kidedea?au ulikuwa unamaanisha mechi ya kitandani?

Hahaaaaa mwandishi anacheeka!!!

Unaambiwa mzee alinyong'onyea akajigeuza akaangalia juu hajui atatoka kwa njia gani,mama akatoa mkono wake nje ya neti akawasha taa akamgeukia mumewe akaanza kumwimbia kwa sauti ya chini

Kabla hajaanza kusema mzee akasema " samahani mke wangu..... Mama akajibu "usijari,bila hata samahani nimekusamehe,lakini naomba kukuuliza mwenzangu;-

Ulikuwa unataka nini kwa msichana ambacho mimi sina?

Najua kitu cha kwanza ulichotambua kama ni mimi mkeo,ni matiti yangu yalivyolala......

lakini umesahau kama na mimi wakati wa ujana wangu nilikuwa kama huyu binti nilikuwa mzuri nilikuwa nang'ang'aniwa na vijana wengi lakini miongoni mwao nikakuchagua wewe uwe mume wangu,

siku hazigandi mwenzangu!

Umri umesogea,kubaliana na hali iliyopo!!

Unataka nini kwa house girl?
Wenzio wakina Ibrahim walikuwa wanataka watoto......Mbona nimekuzalia watoto watano wote unataka nini kwa house girl??

Mwache Mtoto wa watu usimvurugie malengo yake
Nakuomba nakuombea kwa Mungu tuumalize uzee wetu vzur tafadhari.......mzee hakuna na neno lingine zaidi ya samahani mke wangu".

Nimekusamehe, naomba zawadi yangu....akamwonyesha kwa ishara rambo iliyokuwa chini.......mama akafungua akakuta skin title 12 akamwambia asante sana....sasa nimekusamehe tumalizie usingizi hapa hapa si ndio?

Mzee akasema twende kwetu wakatoka kwenda kulala

House girl anasema ilipita miezi mitatu hawakuwahi kuonana na dadii ijapokuwa wako wote ndani na sasa yupo kwake alishaolewa.

Wanaume mpone kwa kweli
 
Japo hii ni Shigongo style, ila Mama alitumia busara ya hali ya juu sana. Walio wengi wangemtimua huyo HG haraka sana maana kuepuka competition iliyoibuka. A good lesson kwa wamama (na wababa?) wote.

Joseverest akitia mguu tu, mimi ntatoka hapa. I am out of my comfort zone:)
 
Daaaa hakika huyo mama alikuwa shupavu Na muelewa.. Hakutaka kuanzisha gubu na dada wa kazi icho nazani ndicho kilicho nusuru ndoa yake... Busara ni kitu cha muhimu sana katika maamuzi..
 
Japo hii ni Shigongo style, ila Mama alitumia busara ya hali ya juu sana. Walio wengi wangemtimua huyo HG haraka sana maana kuepuka competition iliyoibuka. A good lesson kwa wamama (na wababa?) wote.

Joseverest akitia mguu tu, mimi ntatoka hapa. I am out of my confort zone:)
Huyo mama wa sampuli hiyo niadim sana
 
Busara sana mamy katumia wengine wanakuwa wakali ndio maana Housegrl huwa wanaogopa kusema chochote
 
Huyo mzee anawinda tetere kwenye pori ambalo mkewe naye yupo...!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom