Engineer Mohamed
JF-Expert Member
- Jul 27, 2007
- 451
- 11
Wawakilishi Zanzibar wadai Benki Kuu Tanzania inawalinda mafisadi Na Salma Said, Zanzibar
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wamesema Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inawalinda watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi wa kuchota mabilioni ya fedha katika Akaunti Madeni ya Nje (EPA).
Wakichangia mada katika semina iliyoandaliwa na BoT kuhusu Awamu ya pili ya Mageuzi ya sekta ya fedha wawakilishi hao walisema kwa sasa kinachofanyika ni kuwahadhaa wananchi, lakini hakuna nia ya kuwashugulikia.
Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi, Abubakar Khamis Bakari alidai kuwa kama mafisadi wa EPA angekuwa miongoni mwao wamo Wazanzibari wangekuwa wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani.
"Hawa wezi ni jamaa zao hakuna mtu wa Zanzibar katika ufisadi wa EPA, kama angelikuwemo ungeona namna anavyoshungulikiwa" alisema Abubakar ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni.
Kiongozi huyo wa Upinzani ambaye kitaaluma ni Mwanasheria na aliyewahi kuwa Mwanasheria wa Zanzibar, alisema anashangaa kuona mwizi aliyechukua fedha za umma anapotakiwa kuzirejesha, anazurudisha bila ya wasi wasi.
"Kuna suala la EPA jamani, ni mwizi gani anayeiba fedha anachukua na baadaye anazirudisha ni sheria ya Benki gani hiyo, ambayo mtu anaiba fedha na kuzirudisha bila kuskukamatwa," Alihoji Abubakar.
Wawakilishi wengine waliochangia mjadala huo walimuomba Naibu Gavana na BoT, Juma Reli kufanya utaratibu wa kuwachotea fedha za EPA kwa kuwa fedha hizo zinaonekana kutokuwa na mwenyewe.
"Naibu Gavana, kama watu wanaiba fedha za EPA huko BoT na baadaye wanazirudisha, basi na sisi tunaomba tupewe halafu tutazirudisha" alisema kwa kejeli Mwakilishi wa Jimbo la Ole, Hamad Masoud Hamad.
Alisema wizi uliofanywa katika akaunti ya EPA ni mkubwa na haupaswi kupuuuzwa na wahusika wanastahili kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka.
Wawakilishi wengine waliochangia mjadala huo, pia walionesha masikitiko yao dhidi ya ufisadi katika BoT, hatua ya kuchota pesa imezidi kuwafanya Watanzania masikini zaidi.
Hata hivyo, wakati wa kutoa majumuisho Naibu Gavana pamoja na wakurugenzi wengine walishindwa kutoa majibu ya ufafanuzi waliokuwa wameulizwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusiana na suala zima la ufisadi katika BoT.
Habari zaidi zinasema kwamba BoT haikutaka vyombo vya habari kuwepo kwenye semina hiyo, kwa hofu kuwa vinaweza vikawapotosha wananchi juu ya suala zima la benki hiyo.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Ibrahim Mzee walisema waandaaji wa semina hiyo (BoT), walimtaarifu kwamba wasingelipenda waandishi wa habari kushiriki katika kwa kuhofia kuripotiwa vibaya.
Hata hivyo, waandishi wa vyombo mbalimbali walionekana kutupilia mbali agizo hilo na kupenya kwenye semina hiyo ambayo ilikuwa na mjadala mkali kuhusiana na masuala ya EPA na maslahi ya Zanzibar katika BoT.
Wakichangia kwenye semina hiyo wajumbe mbalimbali walilalamikia nafasi za ajira hasa za kati na za juu BoT zimechukuliwa na upande mmoja wa Muungano (Tanzania Bara), wakidai kuwa jambo ambalo haonyeshi umoja wa muungano
Akijibu madai hayo, Reli alisema nafasi ambazo Wazanzibari wanaweza kupewa zisizokuwa na ushindani wa sifa ni zile za kupika chai, ulinzi na udereva, lakini nafasi nyengine zote za kitaalamu zinatakiwa kuombwa na watu wenye sifa na hakuna nafasi maalumu zilizotengwa kwa ajili ya Wazanzibari.
"Waheshimiwa wajumbe nafasi za ajira ya kupika chai, ulinzi na udereva hizi Wazanzibari wanaweza kuzifanya na ni zao hatuna sababu ya kumchukua mpika chai au mlinzi ama dereva kutoka Tanzania Bara, lakini zile za kitaalamu kama uhasibu, IT na nyinginezo, hizo ni lazima watu waombe na kushindaniwa na Watanzania wote wenye sifa," alisema Naibu Gavana.
Majibu hayo yaliwachukiza karibu wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi ambao wasisitiza kwamba Zanzibar wapo watu wenye sifa ambao wanaweza kufanya kazi za kitaalamu.
Hata hivyo, mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi wa Baraza la Wawakilishi, Salmin Awadh Salmin alikiri kuwa ni kweli vijana wengi wa Zanzibar hawana sifa za kuwawezesha kuajiriwa katika kazi za kitaalamu BoT.
mkuu sasa umeanza kuleta dharau kibri na unafiki.kuteuliwa nafasi ya naibu gavana imeanza kukufanya utoje mafuta sio na kuanza kutudharau wa-znz????? kama kupika chai na waliNZI getini mbona wewe hukuajiriwa kazi hiyo.
TAFADHALI TUOMBE RADHI
http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=5520