Ahsante Sana.........juma Reli

Engineer Mohamed

JF-Expert Member
Jul 27, 2007
451
9
Wawakilishi Zanzibar wadai Benki Kuu Tanzania inawalinda mafisadi Na Salma Said, Zanzibar

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wamesema Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inawalinda watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi wa kuchota mabilioni ya fedha katika Akaunti Madeni ya Nje (EPA).

Wakichangia mada katika semina iliyoandaliwa na BoT kuhusu Awamu ya pili ya Mageuzi ya sekta ya fedha wawakilishi hao walisema kwa sasa kinachofanyika ni kuwahadhaa wananchi, lakini hakuna nia ya kuwashugulikia.

Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi, Abubakar Khamis Bakari alidai kuwa kama mafisadi wa EPA angekuwa miongoni mwao wamo Wazanzibari wangekuwa wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani.

"Hawa wezi ni jamaa zao hakuna mtu wa Zanzibar katika ufisadi wa EPA, kama angelikuwemo ungeona namna anavyoshungulikiwa" alisema Abubakar ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni.

Kiongozi huyo wa Upinzani ambaye kitaaluma ni Mwanasheria na aliyewahi kuwa Mwanasheria wa Zanzibar, alisema anashangaa kuona mwizi aliyechukua fedha za umma anapotakiwa kuzirejesha, anazurudisha bila ya wasi wasi.

"Kuna suala la EPA jamani, ni mwizi gani anayeiba fedha anachukua na baadaye anazirudisha ni sheria ya Benki gani hiyo, ambayo mtu anaiba fedha na kuzirudisha bila kuskukamatwa," Alihoji Abubakar.

Wawakilishi wengine waliochangia mjadala huo walimuomba Naibu Gavana na BoT, Juma Reli kufanya utaratibu wa kuwachotea fedha za EPA kwa kuwa fedha hizo zinaonekana kutokuwa na mwenyewe.

"Naibu Gavana, kama watu wanaiba fedha za EPA huko BoT na baadaye wanazirudisha, basi na sisi tunaomba tupewe halafu tutazirudisha" alisema kwa kejeli Mwakilishi wa Jimbo la Ole, Hamad Masoud Hamad.

Alisema wizi uliofanywa katika akaunti ya EPA ni mkubwa na haupaswi kupuuuzwa na wahusika wanastahili kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka.

Wawakilishi wengine waliochangia mjadala huo, pia walionesha masikitiko yao dhidi ya ufisadi katika BoT, hatua ya kuchota pesa imezidi kuwafanya Watanzania masikini zaidi.

Hata hivyo, wakati wa kutoa majumuisho Naibu Gavana pamoja na wakurugenzi wengine walishindwa kutoa majibu ya ufafanuzi waliokuwa wameulizwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusiana na suala zima la ufisadi katika BoT.

Habari zaidi zinasema kwamba BoT haikutaka vyombo vya habari kuwepo kwenye semina hiyo, kwa hofu kuwa vinaweza vikawapotosha wananchi juu ya suala zima la benki hiyo.

Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Ibrahim Mzee walisema waandaaji wa semina hiyo (BoT), walimtaarifu kwamba wasingelipenda waandishi wa habari kushiriki katika kwa kuhofia kuripotiwa vibaya.

Hata hivyo, waandishi wa vyombo mbalimbali walionekana kutupilia mbali agizo hilo na kupenya kwenye semina hiyo ambayo ilikuwa na mjadala mkali kuhusiana na masuala ya EPA na maslahi ya Zanzibar katika BoT.

Wakichangia kwenye semina hiyo wajumbe mbalimbali walilalamikia nafasi za ajira hasa za kati na za juu BoT zimechukuliwa na upande mmoja wa Muungano (Tanzania Bara), wakidai kuwa jambo ambalo haonyeshi umoja wa muungano

Akijibu madai hayo, Reli alisema nafasi ambazo Wazanzibari wanaweza kupewa zisizokuwa na ushindani wa sifa ni zile za kupika chai, ulinzi na udereva, lakini nafasi nyengine zote za kitaalamu zinatakiwa kuombwa na watu wenye sifa na hakuna nafasi maalumu zilizotengwa kwa ajili ya Wazanzibari.

"Waheshimiwa wajumbe nafasi za ajira ya kupika chai, ulinzi na udereva hizi Wazanzibari wanaweza kuzifanya na ni zao hatuna sababu ya kumchukua mpika chai au mlinzi ama dereva kutoka Tanzania Bara, lakini zile za kitaalamu kama uhasibu, IT na nyinginezo, hizo ni lazima watu waombe na kushindaniwa na Watanzania wote wenye sifa," alisema Naibu Gavana.

Majibu hayo yaliwachukiza karibu wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi ambao wasisitiza kwamba Zanzibar wapo watu wenye sifa ambao wanaweza kufanya kazi za kitaalamu.

Hata hivyo, mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi wa Baraza la Wawakilishi, Salmin Awadh Salmin alikiri kuwa ni kweli vijana wengi wa Zanzibar hawana sifa za kuwawezesha kuajiriwa katika kazi za kitaalamu BoT.

mkuu sasa umeanza kuleta dharau kibri na unafiki.kuteuliwa nafasi ya naibu gavana imeanza kukufanya utoje mafuta sio na kuanza kutudharau wa-znz????? kama kupika chai na waliNZI getini mbona wewe hukuajiriwa kazi hiyo.

TAFADHALI TUOMBE RADHI

http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=5520
 
?Hawa wezi ni jamaa zao hakuna mtu wa Zanzibar katika ufisadi wa EPA, kama angelikuwemo ungeona namna anavyoshungulikiwa,? alisema Abubakar ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni.
Hata humu namo wanaingiza uzanzibari? Mimi nazidi kuamini kuwa hawa tunaodhani ni wenzetu watatufikisha pabaya. Siasa kwao ni jazba na chuki. Wanasahau kuwa Babu angekuwa Zanziba wakati wa kifo cha Karume wangemnyonga! Leo wanaona watanzania bara wana kisasi na wazanzibari?

Alichokosea nini Juma Reli katika kuwaambia kuwa nafasi za juu ni competitive? Suala si kuwa kuna mtu anaqualifications, ni jee aliomba na wakati anaomba alikuwa the BEST qualified? Hatuwezi kufanya mashara na nafasi za menejimenti kama tunavyoweza kufanya na hizo za kupika chai na udereva. Ingawa hata huko ingebidi watu wachaguliwe kwa ushindani lakini kuna nafasi za kuweza kufanya upendeleo. Wao wawaambie hao wanaowaona wame'qualify' waombe hizo nafasi za menejimenti. sitashangaa kama hivi karibuni hata kufa kwa People's Bank itasemwa kuwa ni kwa sababu machogo waliifisadi!

Hii ni kweli tupu, sasa kakosea nini?

Hiyo referendum iunganishe swala la Muungano.
 
Muungano wa Julius huo jamani,watu bado wanalalama!!! Kumbe Karume yuko sahihi kutaka kura za maoni
 
"Waheshimiwa wajumbe nafasi za ajira ya kupika chai, ulinzi na udereva hizi Wazanzibari wanaweza kuzifanya na ni zao hatuna sababu ya kumchukua mpika chai au mlinzi ama dereva kutoka Tanzania Bara, lakini zile za kitaalamu kama uhasibu, IT na nyinginezo, hizo ni lazima watu waombe na kushindaniwa na Watanzania wote wenye sifa," alisema Naibu Gavana.
][/B]

http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=5520

Haya majibu ni MAZITO SANA
 
mkuu sasa umeanza kuleta dharau kibri na unafiki.kuteuliwa nafasi ya naibu gavana imeanza kukufanya utoje mafuta sio na kuanza kutudharau wa-znz????? kama kupika chai na waliNZI getini mbona wewe hukuajiriwa kazi hiyo.

TAFADHALI TUOMBE RADHI

http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=5520

Ah vipi Balahau. Usimsubu Bw. Juma. Alichosema ni cha Kweli. Tukaze kamba tufikie madaraja ili tuweze ku-compete. Usiwe mlalamishi kama hao watu, yakhe.
 
...reli amewapa ukweli...nafasi za casuals ndizo unazoweza kugawa kwa upendeleo....lakini hata mlinzi anayekula urojo hafai...labda niongeze kuwa nafasi nyingine ya upendeleo ni za kiSIASA....
 
Ingawa Juma Reli alichosema ni ukweli lakini amekiframe vibaya that was too harsh ....Ila nimecheka sana anasema kupika chai na ulinzi wanaweza kupata bila matatizo
 
Engeneer Mohamed unaposema akuombe radhi , akuombe kama nani, kama engeener ama kama Mlinzi na mpika chai? Inaonekana wazi kuwa Wazanzibar hawapendi kuambiwa ukweli. Bro Call spade , spade and not otherwise.
 
Stark reality.The same applies for UN and its organizations and international organizations.Wafanyakazi wa mashrika hayo casual laborers, walizni wapika chai,wafagizi wote ni watz ila nafasi za kiaalamu kuna waghana,wazungu,wamarekani.etc.

Reali kasema ukweli.
 
..ukimlinganisha Juma Reli na wakurugenzi wa Bara walioko BOT, utaona kuwa shule yake ni nyepesi mno.

..hata huo Wadhifa wake wa Unaibu Gavana umetokana na fadhila ya Muungano.

..hivi hakuna Wazanzibari waliobobea katika Uchumi au Finance kum-replace Juma Reli?
 
Engeneer Mohamed unaposema akuombe radhi , akuombe kama nani, kama engeener ama kama Mlinzi na mpika chai? Inaonekana wazi kuwa Wazanzibar hawapendi kuambiwa ukweli. Bro Call spade , spade and not otherwise.

sio kama zanzibar hakuna watu wenye ujuzi, lakini tatizo la ZNZ siasa mbele, mara nyingi wanachaguliwa watu kwa utashi wa kisiasa wewe tizama baraza letu la wawakilishi (CCM) aibu tupu wawakilishi wanashindwa hata kujieleza , tunadhalilika sana ZNZ kwa upuuzi huu wa kila kitu siasa mbele.

nakumbuka kuna mara moja katika vikao vya EAC kule Arusha, ilikuwa zamu ya watu wa TZ kuchair kikao kwa bahati mbaya wawakilishi wa Mainland walikuwa hawajafika na ikaamuliwa muwakilishi kutoka ZNZ awe chair basi jamaa (jina namuhifadhi) aliingia mitini nadhani aliondoka na basi la alfajiri mana wakati wa kikao anatafutwa hakuonekana.....ilikuwa aibu ...we acha tu
 
Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Wawakilishi, Abubakar Khamis Bakari alidai kuwa kama mafisadi wa EPA angekuwa miongoni mwao wamo Wazanzibari wangekuwa wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani.

"Hawa wezi ni jamaa zao hakuna mtu wa Zanzibar katika ufisadi wa EPA, kama angelikuwemo ungeona namna anavyoshungulikiwa" alisema Abubakar ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni.

Huyu kiongozi wa upinzani ana maana gani anaposema hivi? ana ushahidi ambapo wazanzibari wameshughulikiwa kwa sababu tu ni wazanzabari? Huyu ana tofauti gani na yule aliyedai watu wa Monduli wanaonewa? Nimesoma na kufanya kazi na wazanzibari na sijaona mahali ambapo wamenyanyaswa kutokana na uzanzibari. Wenzetu walikuwa hata wakimaliza kidatu cha sita hawahusiki na JKT na hakuna aliyelalamika. huyu bwana kwa sababu huko wana hisia za kukomoana kati ya waunguja na wapemba anataka kutuletea sisi? Kwa vile avaae kiatu ndiye anayejua kinapombana, atutajie majina ya hao waliopatwa na hiyo dhoruba ili wote tutambue kuwa serikali ya Muungano ni ya kibaguzi. Kama hawezi, anyamaze na awaombe msamaha wale wanaowaita machogo wote! Ni vijineno kama hivi vya uchonganishi ndiyo mwanzo wa matatizo mengi katika jamii zetu.
 
The story is convoluted, there is a lot of history, mudslinging, bickering and all that.

Nikiona haya yanatoka kwa vibabu wala sishangai.Naibu Gavana anaposhindwa kutoa kauli iliyopigwa pasi hapo ndipo nashangaa na nitafocus kwenye hilo.

Akijibu madai hayo, Reli alisema nafasi ambazo Wazanzibari wanaweza kupewa zisizokuwa na ushindani wa sifa ni zile za kupika chai, ulinzi na udereva, lakini nafasi nyengine zote za kitaalamu zinatakiwa kuombwa na watu wenye sifa na hakuna nafasi maalumu zilizotengwa kwa ajili ya Wazanzibari.

"Waheshimiwa wajumbe nafasi za ajira ya kupika chai, ulinzi na udereva hizi Wazanzibari wanaweza kuzifanya na ni zao hatuna sababu ya kumchukua mpika chai au mlinzi ama dereva kutoka Tanzania Bara, lakini zile za kitaalamu kama uhasibu, IT na nyinginezo, hizo ni lazima watu waombe na kushindaniwa na Watanzania wote wenye sifa," alisema Naibu Gavana.

Essentially Naibu Gavana anaweza kabisa kujitetea kwa kusema alichotaka kumaanisha ni kuwa Wazanzibari hawatapewa preferential treatment.Lakini ikiwa kutoa kauli kama hiyo tu ni mzigo kwa Naibu Gavana sitaki kufikiri itakuwaje atapaokuwa anapitia ma balance sheet ya mabenki yote pamoja na kuangalia ma terms of trade ya nchi.

Hata kama alitaka kumaanisha kuwa Wazanzibar hawatapewa preferential treatment au quota katika kazi za kitaalam,jambo ambalo ni murua kabisa katika ulimwengu huu wa soko huria, Naibu Gavana Juma Reli kakosea kusema kuwa nafasi za wapika chai ni za Wazanzibar, na za utaalamu inabidi wenye sifa washindanie.

"Nafasi za wapika chai ni za Wazanzibar" ni kauli tata na inaweza kuwa na maana mbili.

1.Nafasi hizi ni maalum kwa ajili ya Wazanzibar

2.Nafasi hizi ziko wazi kwa watu wote, wakiwemo wazanzibar

Sasa katika kanuni za kufanya kisicho habari kuwa habari, waandishi wa habari huchukua maana iliyo most controversial, hata kama msemaji hakumaanisha hivyo.

Papa alivyofika NY aliulizwa na waandishi wa habari, "Baba Mtakatifu hivi unafahamu kuwa kuna malaya New York? Na yeye bila kujua, almost by reflex akauliza rhetorically "Kuna umalaya New York? Kesho yake New York Post ikaweka headline, Papa auliza "Kuna malaya New York? Subheading "Je anatafuta ndogondogo kama Eliot Spitzer?

Kwa hiyo mara nyingine siyo unachokisema, ni jinsi unavyokisema.Jinsi unavyokisema kitu inaweza kubadilisha kile unachokisema kikawa kitu tofauti kabisa na ulichotaka kusema.

Kauli hiyo ya Naibu Gavana moja kwa moja inaweza kuchukulika kumaanisha kuwa Wazanzibar ni watu goi goi wanaoweza kufanya kazi zisizohitaji akili sana, usomi na kipaji.

Katika dunia yetu ya leo ya kuheshimu kila mtu anatakiwa kuwaomba radhi Wazanzibar, kwani kuna Wazanzibar wa kila hali na kuwalundika wote katika kapu moja ni makosa makubwa.

Haya mambo ya kuwalundika watu wa nchi/race/religious affiliation pamoja ndiyo yaliyopingwa katika civil right movement USA,ndiyo yaliyopingwa katika apartheid system South Africa.Hizi bias ndiyo zilileta genocide Rwanda Burundi na ndiyo zilisababisha watu karibu 2000 kufa Kenya juzi juzi hapa.Ndiyo bias hizi hizi zilizosababisha KKK waseme "Niggers are lazy" and some rubbish like that.

You can't just lump an entire island together just like that.If you want a scientifically qualified dialogue produce data and lets discuss.
 
..kama miaka yote hii Wazanzibari wameshindwa kujichanganya na Watanzania, basi hii experiment inayoitwa Muungano bora isitishwe.

..kila mtu achukue 50 zake. Huu Muungano ni wa kulazimishana kama ule wa Yugoslavia.
 
..ukimlinganisha Juma Reli na wakurugenzi wa Bara walioko BOT, utaona kuwa shule yake ni nyepesi mno.

..hata huo Wadhifa wake wa Unaibu Gavana umetokana na fadhila ya Muungano.

..hivi hakuna Wazanzibari waliobobea katika Uchumi au Finance kum-replace Juma Reli?

Aste aste yakhe. Kwa wakati huu afaa huyo. Tumesema tumo tunakaza kamba, na kama ushindani tutashindania hizo nafasi. Usiandikie mate, nakupa miaka mitano tu..the task is challenging , and we are ready for that- honestly.
 
..kama miaka yote hii Wazanzibari wameshindwa kujichanganya na Watanzania, basi hii experiment inayoitwa Muungano bora isitishwe.

..kila mtu achukue 50 zake. Huu Muungano ni wa kulazimishana kama ule wa Yugoslavia.

Yakhe wataka kuchafua hali ya hewa. Mheshimiwa Jumbe yupo Mji Mwema anapumzika kwenye mizimu ya kwao. Baba wa Taifa amefariki, lakini mizimu yake itakuchapa Mheshimiwa.
 
Hivi Baraza la mitiani wameanza kuwapelekea mitiani tofauti na ya Bara maana hata ili it was issue, je Universities zile nafasi za wazanzibar bado zipo wawe na sifa wasiwe nazo lazima hizo nafasi zijazwe na wazanzibar, wanapendelewa sana ndo maana wanafika sehemu wanaona kila kitu kwao lazima kiwe easy.
Amkeni maana wakati tulionao mtaachwa bila kujua.
 
The story is convoluted, there is a lot of history, mudslinging, bickering and all that.

Nikiona haya yanatoka kwa vibabu wala sishangai.Naibu Gavana anaposhindwa kutoa kauli iliyopigwa pasi hapo ndipo nashangaa na nitafocus kwenye hilo.

Hata kama alitaka kumaanisha kuwa Wazanzibar hawatapewa preferential treatment au quota katika kazi za kitaalam,jambo ambalo ni murua kabisa katika ulimwengu huu wa soko huria, Naibu Gavana Juma Reli kakosea kusema kuwa nafasi za wapika chai ni za Wazanzibar, na za utaalamu inabidi wenye sifa washindanie.

Kauli hiyo moja kwa moja inachukulika kumaanisha kuwa Wazanzibar ni watu goi goi wanaoweza kufanya kazi zisizohitaji akili sana, usomi na kipaji.
Naweza kumkingia kifua Bw. Juma hapo. Wewe hukuwepo katika hiyo semina, naamini ungemuelewa vizuri kutokana na upeo wako, na Wawakilishi waliokuwa wakimsikiliza najuwa wamemuelewa vizuri. Tatizo la sisi kuelewa vibaya limechangiwa na uandishi mbovu wa Mwandishi aliyeandika habari hiyo. Ni mwanagenzi na amefanya "quotations" visivyo hivyo amepotosha badala ya kupasha habari. Taaluma hiyo Mzee -imekwenda kombo hapo.
 
Kwa uwelewa wangu wapo wa Zanzibar wengi tu ambao wamebobea katika kila fani unayo ijua wewe.

Mimi binafsi naamini kuwa Wazanzibar ni miongoni mwa watu waliosoma sana na ni jamii inayoelewa vile vile. Lakini tatizo limeshaelezwa kuwa ni lazima watu waangalie huyo msomi anatoka upande gani . Jee ni mwenzao akina Eng. Mohamed ama vipi.

Na ndio maana hadi leo wanahisi ni wao tu ndio wanao haki ya kufanya kazi katika kila taasisi iwe ya kimataifa, ya Muungano ama ya wapi.

Iwapo wazenj hawatabadilika wataendelea kulalamika kila siku.

Tatizo wanalo wenyewe. Ni juavyo Mimi Zanzibar Hakuna Jina la Juma Reli ,sasa eng ulitegemea nini KAKAAAAA.....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom