Ahsante sana January

Rohombaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
13,055
10,337
Usiku wa kuamkia leo mida ya saa 6 hivi niliangukiwa na bahati ya mtende baada ya January kufanya yake.

Hapa mtaani Kuna pisi moja Kali kutoka kwa mzee PK inafundisha lugha za kigeni kwenye shule hizi za kishua.Ina nyodo sana ukimpa salamu anakujibu kifaransa Ila jana ndiyo nimejua kumbe anajua kiswahili vizuri tu.

Usiku wa Jana huku kwetu kulikuwa na Joto la nyuzi 30°C hivi baada ya umeme kukatika sauti za vilio na matusi vilitawala anga, milango ikaanza kufunguliwa wanaume wakitoka vifua wazi wakinusuru na Joto Kali la ndani huku wakitoa lawama nyingi kwa January.

Tuliojiandaa haikuwa tabu nikaunganisha betri zangu kwenye feni nikaendelea kujipepea ndipo ghafla ikaingia pisi ya kinywarwanda ikiwa ndani ya nguo za kulalia zinatirika jasho akiniomba angalau akae kwenye feni dakika 10 tu huku naye eti akimlaumu mwezi January nikashangaa.

Kuna mistari mingi tu kwenye vitabu vya dini inayozungumzia majirani, kwa sababu feni ninayo moja hivyo ikabidi tushee huku nikiomba January asije akaahirisha ishu zake na kweli Hadi jua linachomoza January alibaki na msimamo wake uleule na ulikuwa usiku mwema sana kwangu. Asante January

Siyo kila kitu kinachotokea ni cha kulalamika, subiri bahati ikudondokee au geuza kuwa fursa. Kuna mzee mstaafu jirani yangu alifunga shule yake ya mafunzo ya namma ya kujiokoa ukiwa ndani ya roba ya mbao. Leo naiona inapakwa rangi huku raia wakijasili kwa wingi. Asante January..

Naomba January iendelee hivyo hivyo kila saa6 usiku ufanye yako Hadi nimg'oe huyu binti wa mwenye nyumba kwa kutumia feni yangu hiihii ya betri mbili.

Asante January
 
Back
Top Bottom