Nimemfuma mke wangu akicheza kwenye kigodoro. Nimeumia sana

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Mke wangu anaelekea kuivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe. Najuta sana kuoa mwanamke kutoka mwambao wa pwani. Sijui ni kwanini nilimkimbilia nikijua nitafaidi mauno feni pekee, kalio skonzi nililolitegemea leo hii limepatiwa majukumu ya kutikiswa tikiswa kwenye vigodoro.

Usiku wa jana mida ya saa nne wakati natoka kazini nikiwa maeneo jirani na mitaa yetu, nilifuata njia kuelekea mahali sauti ya mdundo wa kigodoro inakotokea kwa lengo la kusuuza macho pamoja na kutengeneza hisia za kumuadhibu mke wangu kwa fimbo yangu ya nyama, au nipate namba ya mwanamke mmojawapo mwenye uno feni kwa ajili ya kujiburudisha naye siku ya leo jioni.

Kwa bahati mbaya wakati nawasili eneo la tukio, nimemkuta mke wangu wa ndoa ya miaka 14 sasa akilizungusha uno mithili ya panga boi za Dubai huku akifuatisha mapigo ya ngoma zile tukufu.

Mpiga kigoma mmojawapo alikuwa mbele ya kichwa cha mke wangu akijaribu kumpasulia sauti ile karibu na ngoma yake ya sikio, huku mwanaume mwenye kitambi mbinuko na kaptula ya kitamba iliyochongwa na chupa kwa chini akilikamatia trako la mke wangu na kuufyonza utamu wote. Kisha angesogea nyuma kidogo na kulimwagia maji kisha kulirudia tena baada ya kuwa ndembe ndembe.

Mke wangu angeliinua juu mithili ya mtu aliyepiga magoti huku kichwa chake akikilaza kwenye mkeka ule pasi na huruma huku mikono yake ikielekezwa mbele kuikamatilia miguu ya mpiga kigoma mithili ya mtumwa anayemuomba Mfalme msamaha. Kisha zigo alilonalo lingekunjwa kushoto kulia, juu chini kufuata mapigo ya "mbala🪘 mbala🪘 mbala🪘"

Nilijikuta nikibubujikwa na machozi mazito ya uchungu yaliyoambatana na udenda mwepesi wa aina yake nikiyatazama na kuyafurahia maajabu ya uumbaji ya Mola baada ya kumuona mke wangu akiwa ndani ya mdera akifanya maajabu.

Nilichukua hatua ya kurekodi ngoma za kigoma kile kwenye simu yangu ili kuzifaidi nikiwa na mke wangu nyumbani muda huo simu iko connected na bluetooth kwenye spika ya chumbani

Baada ya hapo niliamua kurudi nyumbani nikiwa na hasira kali nikimngoja mke wangu arejee nyumbani ili nimuadhibu kibinadamu, baada ya hapo nimuadhibu pia kiutu uzima. Nilifika nyumbani na K Vant yangu pamoja na tembe tatu za diklopa na kuwafosi wanangu wakalale mapema

Ni hayo tu wapendwa.

UPDATES:
NILIMWAMBIA KAMA HATAKI KUNIPATIA UTELEZI, BASI ATAFUTE PA KULALA
Baada ya kipigo kizito tulichokipata mimi na mke wangu siku ya jana usiku baada ya mke wangu kurudi kutoka kwenye kigodoro, mke wangu aliamua kuninyima unyumba, alilala sebureni.

Itoshe kusema kuwa tulipata kipigo kitakatifu kutokana na ngumi tulizokuwa tukitandikana na kubamizana vichwa kwenye kabati la nguo. Siyo siri, niseme tu, mbali na kuoa mwanamke, pia nimeoa komando ambalo halikubali kushindwa.

Mwanaume ni mwanaume tu. Vidonda vyangu havijachomoza kwa nje, ni maumivu ndani kwa ndani huku maumivu makubwa yakitokea kwenye moyo, tofauti na mke wangu ambaye vidonda vyake vimeshamili kwa nje.

Mida ya saa saba nimejaribu kusuluhisha tatizo, hii ni baada ya kuona jiko limenuna ilihali kila kitu kipo ndani. Hatukufikia muafaka lakini itoshe kusema mke wangu aliamua kuingia jikoni na kunipikia ugali japo ulikuwa na mabonge mabonge.

Baada ya kula nikaamua kumsogelea karibu kisha kuvuta hisia ya kile nilichokiona jana kwenye kigodoro, nimejikuta nikisoma 6G+. Nilishtushwa na sauti ya "Niache huko, we ni mume gani unayeninyima uhuru? Usiniguse, em niache huko, hujanizaa hadi uniendeshe unavyotaka".

"Utatoa Utoi", ilisikika sauti nene yenye mikwaruzo kutoka kwenye koromeo la shingo yangu. "Sifanyiiiiiii", ndiyo sauti niliyoiskia ikipenya dirishani kuelekea kwenye nyumba za majirani. Nikajikuta napatwa na aibu za ghafla kwa kuwa nimeonesha kuomba tendo mchana kweupe huku joto la jua likiwa linashamili kwa nje.

Ilinitoka sauti moja tu ya "kama hutaki tafuta pa kulala usiku wa leo, na ukienda, tokomea jumla usirudi tena kwangu".

Mke wangu huwa ana kawaida moja ya ikitokea tumegombana, basi mtamaliza wiki hata tatu bila kuzagamuana. Muda huo domo kalivuta, nyumba haitamaniki.

Jibu alilonipatia ni eti hapa ni pa kwetu sote, la sivyo tugawane. Nimepatwa na mshtuko wa moyo nikaamua kuondoka kwenda kumwagilia moyo mchana kweupe licha ya kuwa siku ya leo sikuenda kazini kutokana na songombingo la jana jioni. Uzuri wanetu wako boarding, hivyo hawajui vituko hivi tunavyoendelea kufanyiana mimi na mama yao.

Issue ya kugawana imenifanya nitandike bia jioni nzima, hadi sasa hivi nipo hapa bar napata vyombo. Samahanini kama mwandiko huu umekuwa wa ulevi maake niko tungi ndugu zangu.

Unyumba ni haki yangu mimi kama kichwa cha familia.

Ni mimi Chandra Gupta, mtoto wa Murya

UPDATES:
MKE WANGU ALIAMUA KUWATEGA MAJIRANI NA KANGA MOKO KWA LENGO LA KUNIKOMOA

Baada ya mke wangu kutia ugumu suala la kunipatia utelezi kutokana na mgogoro wa hapa na pale, niliona ni vyema sheria ya kale ya jino kwa jino itumike ipasavyo. Nilichukua simu yangu kisha kumpigia mchepuko wangu mpya aitwaye Rahma.

Niliyaanza mazungumzo nikiwa pembezoni mwa mke wangu, ili kukoleza wino nikaenda kujibanza pembezoni mwa ukuta wa korido ya sebule, muda huo simu ishakatwa kitaambo.

Nilisikika nikisema, "Poa baby, usiniangushe basi, leo nipatie ile style inayoitwa "Mama mkanye mwanao". Nilikuwa sawa na kile nilichokuwa nakifikiria kwa kuwa mke wangu kipenzi Mwa J alikuwa kabana kwenye kuta akiyasikiliza yale maongezi.

Nilivaa buti langu kisha nikamuonesha mke wangu tabasamu la kinafiki kisha kuwapatia wanangu hela ya kula shule, taratiibu nikatoka ndani na kuingia barabarani huku nimeikunja sura mithili ya mtu anayetaka kukojoa.

Tayari tayari, nshalizwa mwenzenu, ni bora nisingempigia simu Rahma. Nilikuwa nikikisaka kibanda cha M Pesa kilicho wazi ili nimtumie 30k aliyoniomba ghafla bin vuu.

Baada ya kumtumia, nilizama kwenye bar moja hapa karibu na kuanza kupiga vyombo vya kila rangi nikiwa na mtoto mmoja niliyetegemea kuzimalizia hasira zangu kwake, lakini kwa bahati mbaya wakati napanga mipango ya kupata chumba na mhudumu, tayari nshalipia 10k nilikuta tayari murembo kashatokomea kusikojulikana, ikabidi nikubali kurudishiwa 5k kama ilivyo ada.

Nikaona isiwe soo, nikaamua kuweka miguu yangu kwenye kiti kingine cha ile meza ya bar, nikatega masikio yangu vizuri kusikiliza muziki ule wa msondo ngoma kwa lengo la kufidishia upotevu wa pesa yangu

Mida ya saa sita usiku nilikuwa tayari nishafika mlangoni na kuanza kubisha hodi pasipo dalili ya kufunguliwa mlango. Kama masihara imefika saa nane kasoro nikaamua kupiga ukunga wa mtu anayevamiwa na vibaka, kidogo hii ilisaidia, kwa kuwa dakika ishilini baada ya mimi kuacha kupiga ukunga nilishangaa geti likifunguliwa taratibu na kwa hofu kubwa

Baada ya kuingia ndani nilimnasa kibao mke wangu kilichofuatiwa na mpasuko wa sukumio la chapati mgongoni. Nilibaki nikijikunja mgongo kwa maumivu makali niliyoyapata. Nilipiga glass tatu za maji kisha kulala palepale sebuleni nilipokuwa

Kawaida ya mke wangu, Mwa J, akiamka na kuoga, huchagua dera lake swaafi jepesi na kulitupia mwilini, kisha huvaa viatu vyake vya manyoya na kuanza majukumu ya hapa na pale.

Mwa J kaamka saa moja hivi na kuvaa kanga nyepesi sana na kwenda kuogea bafu la nje. Wakati anatoka bafuni, khanga ile imemng'ang'ania mwilini na kumchora kabisa, full HD, akiwa kalowa hivyo hivyo kaingia ndani na kutoa nguo zake safi kabatini kisha kutoka nazo nje na kuinama pale kisha kuanza kufua.

Muuza vyombo vya udongo na glass mmoja alikuwa akikatisha maeneo ya nyumbani kwangu, dakika chache nilishtushwa na mlio wa mpasuko wa vyombo. Maskini! Kumbe katika harakati ya kuyafaidisha macho yake alijikuta akikosea njia na kuuvaa mfereji wenye mawe mawe. Ndo hivyo basi, hasara juu ya hasara.

Mke wangu ameona hii ni njia bora ya kulipa kisasi cha tukio la jana usiku, tokea saa moja hadi sasa hivi eti anafua huku zigo hilo akilielekezea kwenye vyumba vya wapangaji jirani na nyumba yangu ambavyo wapangaji wake wengi huwa ni mabachela.

Licha ya kuwa tayari nimeshaomba ruhusa ya wiki nzima kazini, ninaona ni vyema tu niende somewhere nikatulize mawazo mpaka jioni.
 
.
Mkuu umefeli sana hapo uliposema unajutia kuoa mwanamke wa pwani. Ulijua kama angekuwa kubadilika mbelen? Asingebadilika bado ungejuta?
.
Siku zote, kamwe usijutie maamuzi uliyoyafanya kwa sababu wakati ule yalikuwa maamuzi sahihi.
 
Wewe pia una matatizo why uende kwenye kigodoro then unamkuta mkeo anacheza unamlaumu. Unamwoea bure mwache mkeo afanye yaliyofuraha kwake
Mwanamke anapofanya uasherati ama kujiingiza keenye mazingira kama hayo jua wazi kuwa ana kitu cha kupoteza. Ila mwanaume hana anachopoteza

Yaani ni sawa na kinu na mwichi katika matumizi, kinu ndicho husagika haraka kwa kutwangwa twangwa na mwichi

Mi sina ninachopoteza
 
Aisee! Hadi nimeshangaa.

Yaani mbali na hayo unayoita machungu uliyonayo lakini umeweza kuelezea vyote tena kwa bashasha kabisa. Lol.
Ni kwa kuwa tayari kichwa kimeshapumzika na kutafakari kwa kina, lakini kama huu uzi ningeuandika baada ya tukio ningeandika kwa ghazabu na hasira sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom