Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 780
- 1,831
Mwaka jana, Serikali ya Tanzania ilitangaza mpango wa kujenga barabara ya Usagara – Mwanza Mjini (KM 25) kwa kiwango cha njia nne (dual carriageway) ili kupunguza msongamano na ajali zinazoendelea katika lango kuu la kuingia Jiji la Mwanza
Lakini leo, zaidi ya mwaka mmoja baadaye, wananchi wanauliza:
Mbona hatuoni maendeleo ya kile kilichoahidiwa?
Kupitia hotuba za bajeti na maelezo ya mipango ya maendeleo ya sekta ya ujenzi, kipande hiki kilitajwa kama sehemu ya kuboresha miundombinu ya Jiji la Mwanza linalokua kwa kasi.
Eneo la Usagara limekuwa:
Kitovu cha makazi mapya.
Njia kuu ya malori yanayoingia na kutoka Mwanza.
Sehemu yenye msongamano mkubwa nyakati za asubuhi na jioni.
Kwa mantiki ya mipango miji, upanuzi wa KM 25 kuwa njia nne ungekuwa suluhisho la muda mrefu.