Kamanda miye umekumbusha machungu na raha, machungu ni msiba wa baba yangu mdogo ambaye alikuw akifanya kazi stesheni Tabora, nilikuwa sipandi kajamba nani, nimeshuka sana daraja la pili, nilikuwa sijui kabisa adha za daraja la tatu wakati nikitoka Dar kwenda shule ya Uyui pale Tabora, raha nakumbuka nilipata mademu wawili mmoja wa Kigoma alikuwa akiitwa Kidifa.... sijui yuko wapi na mwingine Mchaga alikuwa akiitwa Haika.... hata huyu sijui yuko wapi. Treni ulikuwa bonge la usafari jamani.
i missed this!..sijapanda mpaka leo...nahisi mlikula happy sana wakubwa!..
Ah ilikuwa tunakula ma-happy kwa sana tu!
Namkumbuka TT Simba alikuwa mkali huyo.
Nakumbuka mkifika Korogwe mnabadilisha mabehewa yale ya kwenda tanga na ya kuelekea Moshi yanaunganishwa na kuendelea na safari!!
mweeh enzi hizo nipo sangu secondary mbeya huko.
Nilikuwa bingwa wa kula nauli ya kupandia basi.
Shule ikifunga tunashinda disko mount au soweto complex unatumia nauli ya basi kesho mchana iyunga moja mmebakiwa na hela ya treni tu mnanunua karata mnachukua draft then mdogo mdogo mpk kitu mzizima.
Ha ha ha .... We ni kiboko Kapala...
Kipind hicho ilikuwa inahusika, nan apande scandinavia atoe 8000 mpk chalinze au dar wakati tazara ni wewe na id yako.
Ni noma! hasa ukute behewa wamekata wajeda hukatishi kwenda behewa jingine, au mmetoka Mwz na kufika Tbr kumbe hilo behewa wamepangiwa Tbr boys mtapigwa mikanda hadi muhame
Yaani raha nyingine mnapokutana lile la bara na la kutoka dar maeneo with majina ya shule yalivyobandikwa ubavuni na basi vifijo na kelele wapeleke wa bara hao !!Na kweli ujasiriamali wa kipindi kile jamani,we acha tu!
I miss kile chombo kwa sana..
Mnakutana hadi watu mliopoteana muda mrefu,mnaungana hata na kufahamiana na watu wapya,it was fun pia..
Nataman siku nikibahatika kupanda tren sijawahi tangu kuzaliwa lol!
Yaani raha nyingine mnapokutana lile la bara na la kutoka dar maeneo with majina ya shule yalivyobandikwa ubavuni na basi vifijo na kelele wapeleke wa bara hao !!
poleh sana dear,mimi nilipanda mara moja tu.
Dah umenikumbusha mbali sana....yan enzi zileeeee nasoma zangu Kigoma.....Usafiri wa treni...
Ah... Tuliowahi tukumbushane,mabehewa marefu kama nyoka,hekaheka za ma-TT, mambo ya "buffet car",enhe...
Tukumbushane jamani..