Ah.. Sijui wenzangu...ila kwa sisi tuliowahi kutumia usafiri huu tuli-enjoy sana!!

Pole mama ila usijali na wala hujachelewa, nenda pale stesheni ya dar, chukua tkt ya kwenda makambako by kitu TAZARA.

Hata afike boda la Tunduma kabisa ashuke ageuke.. Ndiyo utalli wa ndani huo! Tena ya Tazara ana rails pana kuliko ya ya kati,na nakumbuka mabehewa yake yalikuwa ni bora kuliko ya reli ya kati,na njiani unapita maselous,wanyama kibao wa porini...

Raha tu..
 
enzi hizo kutoka dar tulikuwa tunapanda train moja na wanaokwenda kigoma mpaka tabora, tufika tabora mabehewa yanatenganishwa tulikuwa tunalala pale tabora. Ukitaka kuuona uzuri wa tz panda train kupitia reli ya kati. Mwanza tulikuwa tunafika asubuhi halafu kutoka mwanza train ilikuwa inaondoka jioni.
 
Kweli kabisa..
Hata Dar inaanzia jioni kama saa12...

Wahaya walikuwa wanaweza kutumia tiketi hiyohiyo kupanda meli jioni (MV Victoria,MV Bukoba) hadi Kemondo,na hadi Bukoba.

Na tiketi zake zilikuwa ndogo kama kipande cha kiboksi kigumu,hakikunjiki.. Na inakuwa imechapwa kama vile imechapwa na mhuri wa moto au kama yale maandishi yamekuwa "engraved"..
 
Aisey Gamba, uliwaza nini kutukumbusha hii maneno ? Inasisimua kiaina yake!
Unamkumbuka yule Mz. Kipofu wa kigogo, alikua anatembea sana na Train akipuliza filimbi ?
Unamlipa sh 50 (sungura) au sh 1 ya (mwenge) au sent 20 ya (mbuni) kisha unachagua wimbo.

Mkuu naomba nikurekebishe kidogo hiyo ni senti 50 (sungura).
 
Nimepanda TAZARA . TRC ni mara mbili DAR --to MOSHI na MOSHI to DAR.
Wakati nipo Sekondari MTWARA usafiri wa MELI MV mapinduzi, MV Lindi, MS Mtwara, na ( MV Kilindoni hii sikuwahi kuipanda).
 
Back
Top Bottom