Kuna vitu viongozi wetu wa dini wanavijua lakini hawawafundishi nyinyi!, miongoni mwa vitu hivyo ni Mungu alipotuumba binadamu wote, na kutupulizia ile pumzi ya uzima, kwa kufanya hivyo, umetugawia 'Umungu" ndani yetu, hivyo Mungu yuko ndani yetu watu wote, wanaomwamini na hata wasio mwamini!. Hivyo hata kabla hao wazungu walipoleta dini zao huku, waliwakuta mababu tayari wanaye Mungu!, hivyo kitendo cha kudismiss everything katika imani zao za asili in totality, its not fair!. Ndio hao wametuletea huu ujinga wa mume mmoja mke mmoja!. Hakuna popote Bibilia Takatifu imetamka mume mmoja mke mmoja!, hii ni just the making ya wazungu na mauongo yao!. Mimi binafsi ningetamani sana kuwa kama Mfalme Suleiman!. Unaijua idadi ya wake zake?!.
Dini, mila na desturi zetu za asili, zilikuwa zina mazuri yake na mabaya yake!, na dini hizi za wazungu, zina mazuri yake na mabaya yake!, mimi nimechukua mazuri from both, na kuyaacha mabaya from both!, hili la mume mmoja na wanawake kadri ya uwezo wao ndilo moja ya mazuri ya mambo yetu ya asili!, na hilo la mume mmoja, mke mmoja ni miongoni mwa mabaya ya dini za wazungu!, nimeachana nayo na marafiki zangu kibao, wana nyumba ndogo!, cha ajabu zaidi wengine ni makasisi wetu!.
Pasco