Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
- Thread starter
- #21
Gamba,
Azimio la Arusha ni mali ya Taifa na si chama. Chama kilitumika kama chombo kutangaza na kulitekeleza.
Katiba na Sheria zote tunazo na tulizirithi kutoka kwa mkoloni na kwa kiasi kikubwa bado tunazitumia kama zilivyokuwa. Azimio ni Manifesto ya Taifa kuatika kulijenga Taifa letu.
Kwa nini nasema Azimio ni mali ya Taifa na si TANU au CCM? Ni kwa kuwa wakati wa mfumo wa chama kimoja, kila Mwananchi alikuwa ni lazima awe mwanachama wa TANU na hata CCM. Mashuleni, makazini, viwandani, biashara, mashambani, vijijini na mijini, kutokuwa mwanachama wa TANU au CCM ilikuwa ni usaliti kwa Taifa. Hivyo basi, kimsingi hata TANU na CCM ni mali za wananchi.
Kilichotungwa na TANU na kumilikiwa na TANU ni mali ya wananchi. Same goes with CCM. Yaliyoandikwa ndani ya Azimio si lazima yawe katika Katiba au kuundiwa sheria. Bali ni dira, mfano wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi, Sera ya Chadema au Utajirisho wa UDP.
Hatuwezi kuendelea kudai eti Azimio ni maliya CCM na si ya Taifa. Kusema hivyo kuna maana kuwa kila kilichofanywa na CCM basi ni mali yao hivyo mwingine akiingia basi atengue kila kitu.
Naomba ulipitie Azimio tena ujisomee na utabaini kuwa Azimio, limetumia Katiba na Sheria zilizokuwepo wakati huo. Ukija kwenye suala la miiko ya uongozi, hata Sheira ilikuwa imelizungumzia hilo, ila tuu Azimio lilitoa msisitizo zaidi.
Sisi Wakristo, tuna Biblia, Amri Kumi, kisha tuna Sala ya Bwana na baadaye ni Imani ya Mitume. Kama Biblia ni Katiba, Amri Kumi (kumi na mbili)ni Sheria, Sala ya Bwana na Imani ya Mitume ndio Manifesto yetu na si lazima ibadilishwe kuwa sheria au katiba.