Agano Jipya

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,531
Yeah, hata mimi nina imani na kudumu kwa kijiwe hiki cha udaku na rumours. Lakini let us be honest with ourselves, this is just a frickin' message board let us not make it like some Lenin Square where a revolution ya wanyonge wa Bongo itaendeshwa. If you believe so, then you are so naive and out of touch. Revolution will never happen through an internet forum as long as less than 1 percent of wananchi are connected and only 3 percent read newspapers. So, kama mnataka kututoa mafisadi, tafuteni mbinu nyingine.


Dear Lord,

I have tried to restrain myself from exploding and advocate milltancy for a while, but Lord, forgive thy servant for I am to go postal!

Lord, the absurdity of the comments above tells me that we have people in our community and society as whole who see no evil in their wrong doings.

Lord, JF is collection of minds and souls of Tanzanians all over the world. These are the people like me who could opt to use a remote control with their relationship with motherland by keeping silent enjoying cheese, chocolate and champaigne or they could be activists voicing concerns for the sake of our nation.

Lord, just like how you did it in old times with Joshua, David or Solomon, allow thy servant to advocate for civil uprising that will bring true revolution to rescue Mtanzania from being deprived of his freedom and natural resources that you have granted us O Lord the day we were concieved.

Lord, I announce, "Death to Mafisadi" "Death to Wahujumu" "Death to Wasaliti". Please forgive me for seeking blood and take life to correct the wrongs and ills in our society created and managed with people like the quoted fellow.

If civil means to make right what has been done wrong are going to fail, I will not heed to your Son and our Savior Jesus Christ to turn the other cheek to the enemy, to forgive him on seventieth time or even love my enemy. For he, my enemy has vowed to destroy me and my offspring and I shall stand tall with my clan to fight oppression. Our march to Calvary has started and no one will take our pride and freedom away.

In thy hands, I rest my case and seek thy blessings,strength, courage, peace, wisdom and happiness. As for patience, that was long lost away.

As in swahili we would say, Nimechoka kungojea.

Amen
 
Pumping up my fist like Sarafina, listening to Zombie by Fela after my prayer above, I have made pact with myslef for a new convenant to rescue Tanzania from the hands of killers who are lyinching us on day light.

As you most of you have seen I started the topic for Focus 2010 and Chadema must Reform as to create a dialogue of great minds (both for and opposing) in searching for means and way to bring true changes for our country and not dwelling on costmetic appearance.

I am calling for all those who are ready to join me in my journey to save our nation to be active participants of several innitiatives that I will be working on to empower Tanzanians (some of you we have already spoke about this).

Yes, my emotions on my prayer above are true, my anger is deeper than Lake Tanganyika, I am tired to be played like a yo-yo or some toy, while I have all the blessings from the Mighty God.

Some of innitiatives that I would like to work on are New Constitution for URT, Muungano, revisiting Azimio la Arusha,Freedom of press, revisiting MKUKUTA and VISION 2025 and Volunteerism.

The priority is on Katiba. For those who will be interested, please send me a PM and we will pick it up from there. The door is open for serious folks of all minds, whether is CCM, Chadema, CUF or Independents.

This project will be for the benefit of Mtanzania and taifa and not tied to one political party.

This is my new convenant in fighting Ujinga, Maradhi na Umasikini. Ni agano jipya la kumrudishia kila Mtanzania matumaini kuwa hatujakwama Jangwani tukisubiri Mana kutoka mbinguni.

Sitaacha mapambano dhidi ya Ufisadi, Uhujumu, Usaliti au Ubadhirifu wa mali na hazina ya Taifa.

Aluta Continua!
 
Kishoka huyo jamaa ni kawaida yake,naona anatafuta attention tuu...pitia post zake za nyuma utajua unajibu mtu wa namna gani,usipteze muda wako
 
Hi Rev! We r keeping it up. We hav thousands coming behind us.. We go 100% from o%..1% etc etc! We have to have the starting point!!
Nafikiri analysis ya koba ni valid! Tukumbuke kuwa bila a reasonable resistance hata kama ni very blind .. we have no going foward!! Hivyo Kwa kweli Kwa hoja tuliyoletwa hakuna jipya ambalo halikutegemewa!
 
Pastor Kishoka!

Nilidhani unaanzisha Agano Jipya kutoka ndani ya Biblia kumbe ni agano jipaya la kuleta namna mpya ya kufikiri na kuchukua na kutenda.

Wazungu hapa UESIEI wanasema.

Talk Change and Walk the Talk.

Kwa hiyo kama Talk ni Tough naamini hata Walk itakuwa Tough vile vile.
 
Kishoka huyo jamaa ni kawaida yake,naona anatafuta attention tuu...pitia post zake za nyuma utajua unajibu mtu wa namna gani,usipteze muda wako


Koba, nimemnukuu huyu bwana si kwa matusi yake ili nimjue kwa maandishi. Najua yeye ni mpuuzi wa siku nyingi. Kilichoharakisha hasira yangu na kutangaza hili Agano jipya ni majivuno yake kama ya CCM.

Yeye anaona kuwa 1% ya Watanzania wenye internet na 3% wanaosoma magazeti hawana haki yeyote wala msukumo kudai haki zao, hivyo sauti zetu ni batili. Hii ni dhana ya CCM kudai eti 80% waliridhia na uongozi wa CCM ndio maana wakashinda Tsunami.

Naam, walishinda Tsunami kutokana na ulaghai, udhalimu na kusaliti Taifa. Leo hii twajutia kura zetu na hivyo tunapotaka kufurukuta mfano kama suala la Katiba, basi kina Nagu na wenzake wa 80% wanasema nyie wa 20% hamna haki.

Katiba ni lazima ipitiwe na kuandikwa upya kukidhi mahitaji ya Taifa na nyakati tulizoko na si kuweka viraka au kuridhia kuwa midhali Katiba ina kimu mahitaji ya CCM (Vigogo wake) basi mazungumzo hata kuichambua Katiba ni Batili.

Azimio la Arusha labidi kuelimishwa na kupitiwa. Kama Mwalimu Nyerere alisema lahitaji mabadiliko kadhaa na kuhamasisha utekelezaji wake.

Watanzania tumepotoka kufikiri kuwa Azimio lilituletea Umasikini. La hasha! Ni sehemu moja ya Azimio ambayo ilitafsiriwa vibaya na kushindwa kufanyika vizuri ni kwenye kupambanua suala la Kujitegemea na haswa kuhusu kutegemea Umilikajji wa Uzalishaji mali kupitia mikono binafsi na hasa ile ya Wageni.

Azimio bado lipo hai, kinadharia na hata kivitendo. Tusipotoshwe na danganya toto ya Zanzibar 1992 ambayo ilifuta miiko ya Uongozi kuhusiana na kujilimbikizia mali!

So my anger is due to the fact that, my place in my nation and my well being are being belittle by idiots like Fisadist, who represents those who we have been fighting day and night!

Msikatee tamaa. Kazi ya Kujenga Taifa bado haijaisha, mapambano ndio kwanza yanapata nguvu mpya!
 
Pastor Kishoka!

Nilidhani unaanzisha Agano Jipya kutoka ndani ya Biblia kumbe ni agano jipaya la kuleta namna mpya ya kufikiri na kuchukua na kutenda.

Wazungu hapa UESIEI wanasema.



Kwa hiyo kama Talk ni Tough naamini hata Walk itakuwa Tough vile vile.

Madela,

Fear not the fight. Nikitumia msaafu, hata Utume wa Kristo ulikuwa na Ugumu wake ambao uliishia kutundikwa Msalabani ili wale wamwaminio Mungu wakombolewe.

Daudi aliimba, "Bwana ndiye Mchungai wangu...Naam nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya"

Time for soft conversation over cup of tea or Chibuku has to come to an end if one side continues to deceive the other side. We need to be tough and not only on our talk but even in the way we walkl!

THe tough talk on Ufisadi has started reaping fruits of our sweats. now Mafisadi wanahangaika kama panya pangoni anapoona nyoka kaingia.

Same has to be done opn Katiba. We can not allow Nagu and CCM to be dismissive as they have done in the past. They have neglected the Muafaka talks and a lesson has been learnt from Kenya, uprising is the only solution!
 
Mandela: Hebu sema tena kwa kufafanua na upana kidogo... naona umesema kimethali zaidi

Mkikaa kikao cha kumwinda simba mla watu( Fisadi) kwa kutumia silaha za jadi mazungumzo yanakuwa makali sana. Tough Talk.

Saa ya kupambana na Simba mla watu ikifika ni wakati wa Ku Walk Talk. Kwa sababu shughuli yenyewe ni ya kumwua Simba ni ngangalii, si lelemama kama kuweka maji kwenye Gilasi, vishindo vyake siku zote huzua patashika( Tough Walk).
Na msipo jiangalia mnaweza toboana wenyewe kwa mishale na mikuki na kuuana badala ya kumchoma na kumwua simba mlawatu( Fisadi)
 
Koba, nimemnukuu huyu bwana si kwa matusi yake ili nimjue kwa maandishi. Najua yeye ni mpuuzi wa siku nyingi. Kilichoharakisha hasira yangu na kutangaza hili Agano jipya ni majivuno yake kama ya CCM.

Yeye anaona kuwa 1% ya Watanzania wenye internet na 3% wanaosoma magazeti hawana haki yeyote wala msukumo kudai haki zao, hivyo sauti zetu ni batili. Hii ni dhana ya CCM kudai eti 80% waliridhia na uongozi wa CCM ndio maana wakashinda Tsunami.

Naam, walishinda Tsunami kutokana na ulaghai, udhalimu na kusaliti Taifa. Leo hii twajutia kura zetu na hivyo tunapotaka kufurukuta mfano kama suala la Katiba, basi kina Nagu na wenzake wa 80% wanasema nyie wa 20% hamna haki.

Katiba ni lazima ipitiwe na kuandikwa upya kukidhi mahitaji ya Taifa na nyakati tulizoko na si kuweka viraka au kuridhia kuwa midhali Katiba ina kimu mahitaji ya CCM (Vigogo wake) basi mazungumzo hata kuichambua Katiba ni Batili.

Azimio la Arusha labidi kuelimishwa na kupitiwa. Kama Mwalimu Nyerere alisema lahitaji mabadiliko kadhaa na kuhamasisha utekelezaji wake.

Watanzania tumepotoka kufikiri kuwa Azimio lilituletea Umasikini. La hasha! Ni sehemu moja ya Azimio ambayo ilitafsiriwa vibaya na kushindwa kufanyika vizuri ni kwenye kupambanua suala la Kujitegemea na haswa kuhusu kutegemea Umilikajji wa Uzalishaji mali kupitia mikono binafsi na hasa ile ya Wageni.

Azimio bado lipo hai, kinadharia na hata kivitendo. Tusipotoshwe na danganya toto ya Zanzibar 1992 ambayo ilifuta miiko ya Uongozi kuhusiana na kujilimbikizia mali!

So my anger is due to the fact that, my place in my nation and my well being are being belittle by idiots like Fisadist, who represents those who we have been fighting day and night!

Msikatee tamaa. Kazi ya Kujenga Taifa bado haijaisha, mapambano ndio kwanza yanapata nguvu mpya!

Rev: You have just touched the realy core of the matter:
hebu soma link hii, ina a simple example of what I want to say..nisirudie hapa : http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=8950

Then pita hii:

Mzee Msekwa hebu tuongee kidogo
dk. gideon shoo​

SUALA la Azimio la Arusha kuwa hai au mfu limekuwa likijadiliwa kwa muda sasa. Mjadala huo haukuibuka tu bila sababu yoyote ile ya msingi. Ni wazi kwamba kulikuwapo na kichocheo cha mwibuko huo.

Na ni hicho hicho kichocheo ndicho ambacho hadi leo bado kinaufanya mjadala huo ufoke na kutulia kama ilivyo volcano ya Oldoinyo le Ngai.

Mjadala kuhusu uhai au umauti wa Azimio la Arusha ni matokeo ya uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana Zanzibar mwaka 1992 kunyofoa moja ya sehemu kuu za Azimio hilo inayohusu Miiko ya Uongozi kwa sababu ambazo hadi sasa hakuna mshiriki yeyote yule aliyefikia mahali pa kutoa sababu za hatua hiyo zikaingia akilini.

Jambo moja ambalo limejidhihirisha ni kwamba, hakuna aliye tayari kujitokeza hadharani na kutoa sababu za msingi za hatua hiyo ya Halmshauri Kuu ya Taifa. Kumekuwapo na ama ukimya kabisa kutoka kwa baadhi ya wajumbe na hata viongozi wa ngazi za juu za Chama au sababu zimekuwa za ubabaishaji ambazo hazijitoshelezi hata kidogo.

Pengine ni katika kuendeleza utamaduni ule ule wa kutokuwa tayari kusema ni kitu gani hasa kiliwasukuma wajumbe wa Halmashauri Kuu kukimbilia kile kipengele bila hata kutaka kushauriana na wanachama, ndiyo sababu Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa naye amejikuta katika wakati mgumu na kutoa majibu ambayo yanalazimisha kupatiwa majibu na kurushiwa maswali mengine ya kutaka ufafanuzi.

Mzee Msekwa si tu kwamba aliwahi kukiongoza chama mzazi wa CCM yaani chama cha TANU (Tanganyika African National Union), bali ni msomi mzuri wa sayansi ya siasa ambaye ameandika vitabu na kuwasilisha mada lukuki kuhusu masuala ya chama, chama kushika hatamu na nafasi ya chama katika utawala n.k.

Katika muda mfupi wa chini ya siku tatu, Mzee Msekwa amesikika na kunukuliwa akijaribu kujenga hoja kwamba Azimio la Arusha halijauawa (gazeti la Mzalendo la Novemba 18, 2007 uk.1).

“Kilichotokea Zanzibar si kuua Azimio la Arusha bali ilikuwa ni kufanya marekebisho madogo katika azimio hilo….

Mzee Msekwa anaendelea kutoa ufafanuzi kuhusu hayo marekebisho madogo kwamba ni “kuondoa kifungu kimoja cha Azimio hilo na kukihamishia mahali pengine kwenye Sheria ya Maadili ya Viongozi…”

Sasa wakati mwingine pamoja na kujiepusha kuingia katika kuumbuana, unaweza kujikuta ukilazimika kupiga yowe la ukunga kama uliyeshambuliwa na chui. Mzee Msekwa ananilazimisha kupiga yowe la ukunga.

Bila shaka hapana ubishi kwamba Azimio la Arusha ni waraka wa Dira ya Taifa ulioainisha sera na ambao kamwe haujawahi kuwa sheria kama zilivyo sheria za nchi.

Aidha, itakumbukwa kwamba yaliyoainishwa kwenye buku hilo ni makubaliano ya msingi ya wana-TANU kuhusu nini kinachotakiwa kufanyika na kutokufanyika katika jitihada za ujenzi wa ujamaa.

Ujenzi wa ujamaa unahitaji wananchi, na hao wananchi wanahitaji viongozi. Viongozi nao ni lazima waongozwe na dira na sera ambayo wanaikubali. Ni lazima kiongozi awatumikie wananchi na ili afanye hivyo ni lazima kuondoa aina yoyote ile ya mazingira yanayoweza kusababisha mgongano wa maslahi hata kama ni wa kudhaniwa tu.

Maadili ya uongozi katika Azimio la Arusha yaliwekwa makusudi kabisa kuhakikisha kwamba kiongozi anapochukua nafasi ajue kwamba hiyo ni dhamana na akubali kutumikia na kamwe asitumie nafasi ile kwa ajili ya manufaa binafsi.

Miiko ya uongozi ilisema wazi kwamba kiongozi wa Chama asiwe na hisa katika kampuni yoyote, asiwe mkurugenzi katika kampuni yoyote ile ya binafsi, asiwe na mishahara miwili au zaidi na pia asiwe na nyumba ya kupangisha.

Mzee Msekwa anadai kwamba miiko hiyo haikufutwa moja kwa moja. Lakini anakiri kwamba iliondolewa katika Azimio la Arusha na eti kuihamishia kwenye sheria mpya iliyotungwa maalumu kwa ajili hiyo – inayoitwa Sheria ya Maadili ya Viongozi.

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ulifanyika mwaka 1992 na wakati huo sheria ilikuwa jikoni na wala haikuwa imekaribia kuwasilishwa bungeni. Hiyo Mzee Msekwa anaikumbuka na anakumbuka kwamba hata muswada huo ulipopelekwa Bungeni mwaka 1994 ulikuwa na matundu na udhaifu mkubwa, ambao hadi leo madhara yake ni jinamizi letu la maisha.

Sasa ni sheria gani hiyo ambayo iliwafanya wajumbe wa Halmashauri Kuu kufikia uamuzi wa kunyofoa kipengele hicho cha maadili ya viongozi? Au kuna sheria nyingine ambayo hatuijui?

Hata kama kwa minajili ya kuendeleza mjadala huu tutakubali kwamba sheria ilikuwapo (ingawa tunajua kwamba haikuwapo) kwa nini ni kipengele hicho tu kilichoonekana kuwa ni kero katika Azimio la Arusha na hivyo kikastahili kunyofolewa haraka haraka?

Mantiki ya uendeshaji wa masuala ya chama na hasa katika nyaraka zake za msingi na muhimu kama lilivyokuwa Azimio la Arusha kwa CCM, inadai kwamba marekebisho yoyote yale ya msingi yanapofanyika katika dira na sera ni lazima yafanywe machapisho mapya ya waraka husika na kusambazwa kwa wanachama ili waweze kujielimisha kuhusu mwelekeo mpya wa chama chao.

Hilo halikufanyika hadi leo. Sasa tueleweje kwamba maamuzi ya Zanzibar yalifanyika bila kuwapo kwa uchukuaji wa kumbukumbu wa aina yoyote ile?

Mzee Msekwa anakubalika ndani na nje ya chama chake. Ni wazi kwamba kwa kuingia katika uongozi wa juu wa Chama wanachama na wasio wanachama wanatarajia na wanatumaini kupata msukumo mpya wa kuhuisha chama na kusaidia katika kuisukuma Serikali itekeleze ipasavyo Ilani ya Chama.

Kitendo cha Mzee Msekwa kutaka kutufanya tuamini kwamba hatua ya kunyofoa miiko ya viongozi kutoka katika Azimio la Arusha “ilichukuliwa kwa sababu maalumu ya kuwezesha viongozi wanaovunja miiko hiyo, waweze kushitakiwa mahakamani kwa kuvunja sheria ya nchi…” si tu kwamba hakina mantiki yoyote, ile bali ni cha ubabaishaji na pengine ingelikuwa vyema akajinyamazia tu kama alikuwa akiona taabu sana kutamka hadharani kwamba kilichofanyika Zanzibar ni kulisaliti Azimio la Arusha na kutoa mwanya kwa baadhi ya viongozi kuhalalisha fedha na mali ambazo tayari walikuwa wamejilimbikizia katika nyadhifa zao.

Kwamba katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja tulishuhudia baadhi ya watu ambao tulikuwa tumefanywa tuamini kwamba walikuwa ni watumishi wa umma wasiokuwa na mali za kutangaza wakichomoza mali kama uyoga.

Mzee Msekwa anatambua wazi kwamba miiko ya viongozi haina maana kwamba kiongozi awe masikini, la hasha. Kinachozungumziwa ni kwamba kiongozi aonyeshe uhalali wa kile alichokuwa nacho na kamwe asije kuitumia nafasi yake ya uongozi kwa ajili ya kujinufaisha.

Kwamba kwa kuondoa miiko ile badala ya kuifanyia marekebisho yaendane na wakati, CCM ilitoa mwanya kwa kila aina ya ufisadi katika uongozi ndani ya Chama na Serikali kwa kukifutilia mbali kipengele hicho na kujifanya kwamba kimehamishwa, inasikitisha sana.

Lakini pengine jambo baya zaidi ni kwamba Mzee Msekwa ametoa maelezo hayo mbele ya wanafunzi wa vyuo 13 vya elimu ya juu na walimu wao walio wanachama wa CCM. Nisingependa kuamini kwamba si wanafunzi wala walimu wao walioona udhaifu wa maelezo ya Mzee Msekwa ambayo alianza kuyatoa katika kipindi cha kila wiki cha Mzee mwenzake Simbeye cha ‘This Week in Perspective’ kilichorushwa na Televisheni ya Taifa (TvT) mwishoni mwa wiki.

Jambo moja ambalo linatatiza wengi ni kwamba ni kwa nini Halmashauri Kuu ilikimbilia kunyofoa hiyo miiko badala ya kufanya marekebisho yanayoendana na zama hizo?

Hivi Mzee Msekwa na wengine wanaotaka kuhalalisha kitendo hicho cha Zanzibar hawaoni kwamba kiongozi wa umma kuwa na hisa katika kampuni kunaweza kwa kiasi kikubwa kukazua mgongano wa maslahi katika utumishi wake?

Kwa nini kabla ya kujitumbukiza katika mtego huo hatari haukufanyika utafiti wa kina wa jinsi wenzetu wanavyoendesha mambo, hasa katika zile nchi ambazo zimepiga hatua katika demokrasia ya vyama na serikali ili kujua ni njia zipi zinazotumika katika kuweka mipaka ya maslahi ya umma na maslahi binafsi katika uongozi?

Katika kujaribu kukwepa uhalali wa maswali yanayoibuliwa na uamuzi wa Zanzibar, akina Mzee Msekwa wanakimbilia kusema kwamba si haramu kiongozi kuwa tajiri. Nami pia nakubali kabisa kwamba si haramu kiongozi kuwa tajiri na pengine ni jambo jema akiwa tajiri.

Lakini niseme kwamba ni haramu kabisa kwa kiongozi kutumia nafasi yake ya uongozi kujitajirisha, hata kama ni kuhalalisha utajiri ambao aliupata kwingine na si kwenye uongozi.

Ni lazima kuwa na mfumo ambao utamzuia kiongozi aliye tajiri kutumia nafasi yake ya uongozi kuimarisha utajiri wake. Kuwa tajiri si kosa hata kidogo. Na chama kizuri ni kile ambacho ndani yake kuna matajiri na masikini, ili mradi wote itikadi yao inashabihiana na malengo yao ni yale yale, kama ni kujenga ubepari basi wote wanajenga ubepari kwa sababu ndiyo dira ya chama chao.

Kama wanajenga ujamaa, basi na wajenge ujamaa, kwani ndiyo itikadi ya chama chao, dira na sera zinaelekeza huko.

Azimio la Arusha ni waraka wa sera. Ndani yake kuna dira ya chama ambayo inaelezwa kwa msingi wa itikadi iliyojumuishwa na siasa ya ujamaa na kujitegemea. Kiongozi wa chama hicho anatakiwa kuwa mstari wa mbele, si tu katika uelewa wa sera bali katika kutekeleza yaliyomo ndani ya waraka huo.

Utekelezaji wa yaliyomo ndani ya Azimio la Arusha ni sera ambayo inapewa nguvu na sheria mbalimbali. Sasa kama kuna mabadiliko ya sera ni lazima sheria nazo zitabadilika.

Kwa mantiki hiyo basi, Mzee Msekwa kudai kwamba kipengele husika kilinyofolewa ili kuwezesha viongozi kushitakiwa ni utani wa hali ya juu.

Sheria inatungwa ili kufanikisha utekelezaji wa sera, sasa haiyumkiniki ung’oe kifungu katika sera eti kwa ajili ya kutoa nafasi ya kuigeuza kuwa sheria, eti ili ifanye kazi. Hiyo si kweli. Ukishang’oa kipengele katika waraka wa sera ndilo hitimisho la sera hiyo na kamwe haiwezi kutungiwa sheria.

Ndio sababu baada ya Zanzibar ilitokea kila aina ya vurugu katika duru za uongozi na kila mmoja na waliomhusu aligeuka kuwa bingwa wa biashara, uwekezaji, ujasiriamali na kadhalika. Ili mradi kulikuwapo mbio katika kuzika miiko yote ile ya uongozi iliyokuwa katika Azimio la Arusha.

Ruksa iligeuka kuwa ruksa kwa kila mmoja kutoka juu kabisa hadi chini kabisa. Na hiyo ruksa haikutumiwa kwa uadilifu na baadhi ya watu waliokuwa katika uongozi na wale waliokuwa pembeni nao udenda ukaanza kuwavuja na haishangazi kwamba baada ya hapo nafasi za uongozi zikageuka dili.

Katika kuhitimisha hoja yangu, ni vyema swali la nini kilichofanyika Zanzibar likajibiwa kwa uwazi zaidi na pengine si vibaya kutamka bayana kwamba kuna hitilafu iliyotokea na pengine kiwewe cha mageuzi kilitukumba na hivyo kufanya uamuzi ambao umegeuka kuwa jinamizi letu la kudumu na jinsi ya kumrudisha jini ndani ya chupa imekuwa vigumu mno.

Hapana ubishi kwamba vurugu yote ya sasa ya kutoaminiana, vurugu katika uchaguzi, uhahaji wa kutafuta nafasi za uongozi tunaoushuhudia hivi sasa na madhambi yote ambayo tunayapigia kelele katika uchaguzi chimbuko lake la kwanza ni uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kunyofoa hicho kipengele muhimu katika Azimio la Arusha na halafu kujifanya kwamba hakuna lolote baya lililofanyika.

Hatutaki kusema ukweli kwamba kwa kuondoa miiko ya viongozi na bila kuiweka miiko mingine ndani ya waraka muhimu wa chama kama Azimio la Arusha, tulifungulia milango kila aina ya watu ndani ya uongozi wa chama na hatimaye Serikali.

Matokeo yake hata Mzee Msekwa anayajua. Pengine anachokifanya Mzee wetu Msekwa ni kujiandaa kutafuta jibu mwafaka litakalokidhi na kukata kiu ya wadadisi wa mambo; kwamba Azimio la Arusha li wapi?

© Habari Corporation Ltd
All rights reserved

Huchapishwa na Habari Corporation Ltd. P.O. Box 4793, Shekilango Road, Sinza Kijiweni, Dar es Salaam
raihcl@yahoo.com
22.11.2007 1046 EAT

THEN malizia na hiii:

Definetly you will see that there lots of people with same idea as yours. Wanaelimisha na kutoa Mwito wa kusonga mbele: Na utaona kuwa bado we have hope kama Tunataka.


RAIA MWEMA: NASAHA ZA MIHANGWA: Januari, 16, 2008 http://www.raiamwema.co.tz/08/01/16/11.php

Azimio la Zanzibar: Tunacheza Kibepari, tunaimba Ujamaa

NI miaka 16 sasa tangu kuanza kwa Azimio la Zanzibar mwaka 1992, lililobadili sera za uchumi kwa kulainisha au kuvunja kabisa misingi ya Azimio la Arusha la 1967.
Tangu hapo maji mengi ya mto yamepita chini ya daraja yakibeba viumbe hai vya majini, magogo na viumbe wengine na kuelekea baharanini.
Aazimio la Zanzibar limekaribisha mambo mengi sana, lakini makubwa na muhimu kati ya hayo ni kupokewa kichwa kichwa shinikizo la sera za Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha kimataifa (IFM) kama vile mfumo wa vyama vingi vya siasa, ubinafsishaji (usiojali) kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji kutoka nje na serikali kujitoa katika shughuli za kibiashara na utoaji wa huduma za jamii kwa maana ya kuachia nguvu ya soko ifanye kazi
Ilivyokuwa ni kwamba kama tungekataa kupokea na kutekeleza sera hizo nchi ingenyimwa misaada na mikopo na nchi tajiri na mashirika yake ya kimataifa.
Ingawa Katiba (ibara ya 3 na 9 ) bado inatamka kwamba nchi “inafuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea”, yanayotokea ni kinyume chake tunaimba “Ujamaa” huku tukicheza ngoma ya kibepari.
“Bongoland” ni jina iliyopewa nchi kwa maana ya utawala wa mwituni ambapo watu kutokana na ugumu wa maisha wanaishi kwa ujanja ujanja, ulaghai (utapeli) akili na viunganishi ili kujipatia riziki kwa njia yoyote ile.
Utapeli huo haukuishia kwa kiwango cha mtu binafsi tu, hata Serikali haikusalimika, huko uporaji wa rasilimali, ubinafsishaji na uwekezaji usiojali uuzaji wa nyumba za Serikali kwa “waliobarikiwa” kwa bei ya “chee” matumizi mabaya ya misaada na ufisadi mwingine vimetia fora katika nchi ambayo uwajibikaji na maadili yanamomonyoka kwa kasi.
Tulianza na sera za kurekebisha mifumo ya uchumi (SAPs na SRPs) zilizoandaliwa na kushinikizwa kwa utekelezaji na WB na IFM. Na katika kuvikwa kiremba cha ukoka baada ya ubepari wa kimataifa kuvunja uti wa mgongo wa sera na fikra za kiukombozi tulizozijengea tangu uhuru nchi yetu ikawa moja ya nchi zenye kupokea misaada mikubwa kutoka nchi zilizoendelea na hivyo kuongeza fikra za utegemezi miongoni mwa watu na watu.
Ni katika kuvikwwa kilemba hicho cha ukoka na kudumazwa kifikra kwamba rais wetu wa awamu ya tatu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Tume ya Utandawazi ya Dunia, ambayo ripoti yake haijasaidia kitu ila kuimarisha ukoloni mambo leo.
Zikafuatia warsha na makongamano juu ya sera huria za uchumi (lakini si juu ya demokrasia na utawala bora ili kuwaamsha watu wajue haki zao na misingi); fulana na vipeperushi vitachapishwa ambavyo pamoja na posho kubwa za vigogo vilitafuna sehemu kubwa ya misaada kwa nchi.
Miaka 16 ya Azimio la Zanzibar imeshuhudia kupwaya kwa demokrasia na mkataba kati ya watawala na watawaliwa unaotaka watawala watawale kwa ridhaa ya wanachi.
Kupwaya kwa mkataba huo kunathibitishwa na kauli za viongozi kama “wavivu wa kufikiri” au “wale majani” kwa sababu tu ya kuhoji hoja za viongozi na Bunge kukosa meno.
Miaka 16 ya azimio la Zanzibar limeshuhudia kutoweka kwa miiko ya uongozi na kufanya fedha na utajiri kuwa kigezo cha kupata au kubakia katika uongozi.
Sasa huwezi kutenganisha utajiri na uongozi kwa kuwa fedha inanunua uongozi na uongozi unanunua fedha na utajiri. Leo ni nadra kuwa na kiongozi asiyetajiri. Sasa wanasiasa ni kati ya matajiri wakubwa katika jamii.
Fungate kati ya fedha na siasa imehamisha utawala kutoka kwa watu kwenda kwa matajiri wenye fedha chafu, wanaoweza kufadhili uchaguzi na kuingiza viongozi madarakani kwa nguvu ya fedha badala ya ridhaa ya watu.
Miaka 16 ya Azimio la Zanzibar imeshuhudia Taifa kutekwa nyara na kikundi kidogo cha “wasomi” wajanja lakini wenye nguvu kutokana na kujishirikisha kwao na mitaji ya kimataifa na mafisadi mbalimbali.
Ni kikundi hiki kinachoingia mikataba mibovu ya uwekezaji kwa kutanguliza mbele maslahi binafsi. Ni kikundi hiki kilichopania kuangamiza uhuru wa vyombo vya habari ili kiweze kula kimya kimya bila kuanikwa hadharani.
Ni kikundi hiki kinacholigawa Bunge kuwa na “hoja ya wapinzani” na “hoja ya chama tawala” ili wabunge wasiseme kwa sauti moja katika kutetea maslahi ya wananchi au katika kutokomeza ufisadi.
Ni kikundi hiki kinachotuambia nchi yetu inafuata sera ya ujamaa na kujitegemea wakati kinatuchezesha ngoma kwa mdundo wa kibepari. Ni kikundi hiki kinachofurahia na kudumu katika kashfa kama kitendo cha “ushujaa”badala ya kuziona kuwa ni jambo la aibu.
Miaka 16 ya Azimio la Zanzibar imeshuhudia wabunge kuruhusiwa kuwa wenyeviti au wajumbe wa bodi za taasisi za umma. Zamani hawakuruhusiwa kwa dhana sahihi kwamba wasingeweza kuhoji bungeni utendaji kazi wa taasisi wanazoziongoza. Mtu huwezi kujichoma kisu mwenyewe.
Tumeshuhudia wabunge kuteuliwa kuwa wakuu wa mikoa, kinyume na dhana ya utawala bora juu ya “mgawanyo” wa madaraka kwa kuzingatia mihimili mitatu Bunge, Utawala na Mahakama.
Miaka 16 ya Azimio la Zanzibar imeshuhudia kuongezeka kwa baraza la mawaziri kufikia 63, likiwa ni kubwa kuliko yote tangu uhuru. Kimeshuhudia pia kuongezeka kwa majimbo ya uchaguzi, wilaya na mikoa kwa njia ya kutengeneza ajira zaidi kwa tabaka la wanasiasa, yote hayo yanatendeka katikati ya utamaduni uliozuka kwa wabunge kwenda likizo ndefu na kutoonekana kwa wananchi hadi unapokaribia uchaguzi mwingine wakiwa wamesheheni “takrima” ili wapate kura kwa nguvu ya fedha. Hakika demokrasia ya uwakilishi si uwakilishi tena bali ni “utatanishi”.
Miaka 16 ya azimio la Zanzibar limeshuhudia kuhama kwa zingatio la wanasiasa na watawala juu ya maendeleo vijijini kwenda maendeleo ya biashara ndogondogo mijini kwa njia ya mikopo ya dunduliza (Saccos) mithili ya wachuuzi wa Kishihili. Kwa mara ya kwanza tangu uhuru, hatuna wizara ya maendeleo vijijini mahsusi kwa ajili ya kumwendeleza mwananchi wa kijijini.
Magari ya vigogo wetu maarufu kama “shangingi” yanajieleza yenyewe kwamba watumiaji wake ni watu wenye mtazamo wa vijijini maana ni magari yasiyoshabihiana na barabara za vijijini waliko wapiga kura walalahoi.
Mkoloni na viongozi wa enzi hizo hawakuwa wajinga kuchagua “Landlover” kwa shughuli zenye mazingira magumu vijijini.
Miaka 16 ya Azimio la Zanzibar limeshuhudia kubezwa kwa sekta ya kilimo na kukumbatiwa kwa sekta ya madini. Mwanzo tuliambiwa “kilimo ni uti wa mgongo” wa uchumi, leo macho yetu yameelekezwa kwenye machimbo ambako, hata hivyo, tunaambiwa taifa halinufaiki na mikataba ya madini eti kwa sababu ya sheria za madini kuwa mbovu.
Ni nani anayetunga sera na sheria hizo kama si sisi wenyewe? Ni nani mwenye uwezo wa kuzibadili kama si sisi wenyewe? Kwa kulialia kwetu tunamdanganya nani wakati tunakula bila kufuta midomo?
Kabla ya sakata la mikataba mibovu ya madini halijaisha na “wawekezaji” (waporaji) kuanza kufukia mashimo kwa kuanzia Buhemba na kwingineko baada ya kukomba madini, makampuni ya mafuta kutoka nje nayo yameanza kumiminika kuvuna bidhaa hiyo chini ya mikataba tata na mibovu kama ile ya madini.
Kwa mfano, hivi karibuni Serikali imetiliana mkataba wa miaka 25 na kampuni ya Petrobras ya Brazil kwa shughuli ya kutafuta mafuta katika Bahari ya Hindi. Tunaelezwa kati ya miaka hiyo 25 minane ya kwanza itakuwa ni kwa ajiri ya kupata taarifa za kijiolojia, kifizikia na kikemia.
Miaka minane itakuwa kwa ajili ya kuendeleza utafiti na uchimbaji wa visima, kama kampuni hiyo itagundua mafuta itatengenezewa mkataba wa miaka 25 ya uzalishaji ya kuanza kulipa kodi.
Hatuhitaji kukumbushwa yaliyotokea kwa mikataba ya madini. Kipindi chote cha miaka nane ya utafiti na uchimbaji visima cha nini kama si historia ya mikataba ya kiporaji ya madini kujirudia? Nani atathibitisha kwamba hawavuni mafuta?
Kinachokera zaidi ni ule usiri katika mikataba hiyo kana kwamba wananchi hawana haki ya kuelewa jinsi utajiri wa nchi yao unavyotumika.
Taarifa zinasema tayari kuna mikataba mingine kama huo na makampuni mengine 18 ya utafiti wa mafuta nchini na wakati huo huo mazungumzo yamekamilika na kampuni nyingine mbili za Statoil ya Norway na Tullow Oil ya Uingereza.
Miaka 16 ya Azimio la Zanzibar imeshuhudia kuvunjwa kwa Katiba ya nchi ili kulinda na kutetea maslahi ya kitabaka kiuchumi, kisiasa na kijamii dhidi ya matakwa ya idara ya 9 kwamba “…… Mamlaka ya nchi na vyombo vyake vyote wanawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha …….. kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa (kwa uwazi) kwa njia mbazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa ujumla na pia kuzuia mtu kunyonya mwingine”. Mikataba mingi hasa kwenye sekta ya madini na ubinafsishaji ni kielelezo tosha juu ya kukiukwa kwa Katiba.
Lakini nani amfunge paka kengere wakati safu ya uongozi imejaa watu wenye uchafu?
Nani apige vita maovu wakati mhimili wa nne, kwa maana ya vyombo vya habari, umebanwa na sheria na ssa unamwagiwa tindikali?
Nani amsemee mwananchi wakati mhimili muhimu wenye dhamana ya kulinda maslahi ya umma, yaani Bunge, unasukwa sukwa?
Miaka 16 ya azimio la Zanzibar limeshuhudia kuporomoka kwa uzalendo. Wananchi wamekatishwa tama na tabia, mwenendo na vitendo vya wanaojiona wenye nchi zaidi, wenye meno zaidi ya kufaidi matunda ya uhuru.
Sasa wenzetu wanaandaa mswada na uraia wa nchi mbili (dual citizenship) ili kuunda Taifa la ma-popo. Muswada huo utatoa haki kwa mafisadi wasio na uchungu wa nchi kuvuna wasichopanda, wakirandranda mipakani na kutoshikika.
Muswada kama huo ulikataliwa na Bunge la uhuru mwaka 1962. Leo vipi unarejea? Miaka 16 ya Azimio la Zanzibar imeshuhudia nchi kuongozwa bila dira wala ramani.
Katiba inasema: “Jamhuri ya Muungano (ni) Taifa la watu sawa na huru, wanaofurahia uhuru, haki, undugu na amani kutokana na kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ambayo inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa…………”
Miaka 16 ya Azimio la Zanzibar imethibitisha kwamba sisi si Wajamaa na hatuna azma ya Kujitegemea, isipokuwa tumekubali kuwa tegemezi wa sera za WB na IFM.
Tumekosa dira na ramani kutuongoza tuendako. Wahenga walisema “mtu asiyejua bandari anayoelekea, hakuna upepo ulio mwafaka kwake” hiyo ndiyo hali tuliyomo sasa.

REV: Ninamaliza kwa kusema Nakubaliana kabisa na maneno yako::

Azimio la Arusha labidi kuelimishwa na kupitiwa. Kama Mwalimu Nyerere alisema lahitaji mabadiliko kadhaa na kuhamasisha utekelezaji wake.

Watanzania tumepotoka kufikiri kuwa Azimio lilituletea Umasikini. La hasha! Ni sehemu moja ya Azimio ambayo ilitafsiriwa vibaya na kushindwa kufanyika vizuri ni kwenye kupambanua suala la Kujitegemea na haswa kuhusu kutegemea Umilikajji wa Uzalishaji mali kupitia mikono binafsi na hasa ile ya Wageni.

Azimio bado lipo hai, kinadharia na hata kivitendo. Tusipotoshwe na danganya toto ya Zanzibar 1992 ambayo ilifuta miiko ya Uongozi kuhusiana na kujilimbikizia mali!
 
Bwana asifiwe! maana nilifikiri nipo peke yangu na wachache ninaowafahamu Nashukuru na nafurahi kuwa tupo wengi wenye mtazamo huo huo wa mapinduzi. hivyo vita hivi ni kutoka pande zote kumng'oa haramu mhujumu mbadhirifu.

Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyanyaswa kiasi cha kutosha, tumepuunzwa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha. Ni unyonge wetu ndio uliotufikisha hapo. ni unyonge tuliouendekeza na kufanya ushamiri na kutuacha Masikini, Wajinga na wenye Maradhi.

Naam sasa ni wakati wa kumkataa Shetani nia kazi zake ili tuondokane na Unyonge ulioleta Udhalimu, Ubadhirifu, Uhujumu na Usaliti!
 
Hii ni sehemu tu ya mahojiano ya Mwalimu na IB. unaweza kuyasoma yote hapa: MAHOJIANO NA MWALIMU

IB: Does the Arusha Declaration still stand up today?


MJN: I still travel around with it. I read it over and over to see what I would change. Maybe I would improve on the Kiswahili that was used but the Declaration is still valid: I would not change a thing. Tanzania had been independent for a short time before we began to see a growing gap between the haves and the have-nots in our country. A privileged group was emerging from the political leaders and bureaucrats who had been poor under colonial rule but were now beginning to use their positions in the Party and the Government to enrich themselves. This kind of development would alienate the leadership from the people. So we articulated a new national objective: we stressed that development is about all our people and not just a small and privileged minority.

The Arusha Declaration was what made Tanzania distinctly Tanzania. We stated what we stood for, we laid down a code of conduct for our leaders and we made an effort to achieve our goals. This was obvious to all, even if we made mistakes - and when one tries anything new and uncharted there are bound to be mistakes.

The Arusha Declaration and our democratic single-party system, together with our national language, Kiswahili, and a highly politicized and disciplined national army, transformed more than 126 different tribes into a cohesive and stable nation.

However, despite this achievement, they say we failed in Tanzania, that we floundered. But did we? We must say no. We can't deny everything we accomplished. There are some of my friends who we did not allow to get rich; now they are getting rich and they say `See, we are getting rich now, so you were wrong'. But what kind of answer is that?

The floundering of socialism has been global. This is what needs an explanation, not just the Tanzanian part of it. George Bernard Shaw, who was an atheist, said, `You cannot say Christianity has failed because it has never been tried.' It is the same with socialism: you cannot say it has failed because it has never been tried.
 
Hii ni sehemu tu ya mahojiano ya Mwalimu na IB. unaweza kuyasoma yote hapa: MAHOJIANO NA MWALIMU

IB: Does the Arusha Declaration still stand up today?

MJN: I still travel around with it. I read it over and over to see what I would change. Maybe I would improve on the Kiswahili that was used but the Declaration is still valid: I would not change a thing. Tanzania had been independent for a short time before we began to see a growing gap between the haves and the have-nots in our country. A privileged group was emerging from the political leaders and bureaucrats who had been poor under colonial rule but were now beginning to use their positions in the Party and the Government to enrich themselves. This kind of development would alienate the leadership from the people. So we articulated a new national objective: we stressed that development is about all our people and not just a small and privileged minority.

The Arusha Declaration was what made Tanzania distinctly Tanzania. We stated what we stood for, we laid down a code of conduct for our leaders and we made an effort to achieve our goals. This was obvious to all, even if we made mistakes - and when one tries anything new and uncharted there are bound to be mistakes.

The Arusha Declaration and our democratic single-party system, together with our national language, Kiswahili, and a highly politicized and disciplined national army, transformed more than 126 different tribes into a cohesive and stable nation.

However, despite this achievement, they say we failed in Tanzania, that we floundered. But did we? We must say no. We can't deny everything we accomplished. There are some of my friends who we did not allow to get rich; now they are getting rich and they say `See, we are getting rich now, so you were wrong'. But what kind of answer is that?

The floundering of socialism has been global. This is what needs an explanation, not just the Tanzanian part of it. George Bernard Shaw, who was an atheist, said, `You cannot say Christianity has failed because it has never been tried.' It is the same with socialism: you cannot say it has failed because it has never been tried.

Mwanakiji,

That is why I said, Azimio did not bring us Umasikini. Ulimbukeni na kudhani kutajirika na kuwa kama kina Rokafela,DuPont, Ford na koo nyingine za Kizungu ndio maendeleo.

Those people created wealth by working hard, they did not steal, they were thrifty, they did not squander.

Infact Azimio was creating a foundation for emergence of the likes of Dupont, hard working people who use their imagination and creativity to revolutionize our lives. (rejea kipengele cha juhudi na maarifa).

Now our ruling class instead of working hard to become like the likes of Ford, they rush like Marcos, Bokassa and Pinochet! Worse enough is supressing the mass and lead them into a Maze that has no ending or purpose!
 
Mzee MwanaKiji: Thanks so much for Links.

Sikuwahi kuiona while r in deep research kujaribu kuona what realy went wrong. Nimeshangaa kuona kuwa Kumbe Mwalimu JK ali_predict kurudi kwa Azimio la Arusha in a new verson :
"...But I still think that in the end Tanzania will return to the values and basic principles of the Arusha Declaration..."

Ona hoja ya msingi na key words hapo: Values + Basic Principles

Inabidi kutulia na kuondoa papara uchambuzi a kina unapobidi kufanywa: Inabidi kuangalia Taifa lilipo sasahivi. Inabdi kuona Ufisadi uanvyoliteketeza taifa mabalo linaitwa taifa huru la tanzania: Ndio utangamua maana ya maneno hayo; value and Basic principles

Wakati wa kupigania uhuru: lazima kuna kikundi cha watu kilikaa na KUAGANA kuwa Lazima kuupata Uhuru wa Taifa la Tanganyika wakati huo. Lazima Waliagana na kukubaliana mambo muhimu...(Basic values and Principles).

Ofcorse Uhuru wakati ule ilibidi uanzie kwenye UHURU WA BENDERA:
But Agano la Msingi la kupigania Uhuru lilikuwa Kila "Familia Ya Tanzania KUJITEGEMEA KIUCHUMI"

Harakati na mapambano ya kaanza: Uhuru ukapatikana. Kumbuka hilo halikuwezekena Bila kuwa Na viogozi. Viogozi wa kulifikisha "TAIFA KWENYE KUJITEGEMEA KIUCHUMI KWA KILA FAMILIA NA KILA MTANZANIA"

Baada Ya Uhuru wabendera kuelekea kujenga uhuru wa uchumi. Mambo kama yanoyotokea sasa kwnye serekali ya awamu ya nne yakaanza kujitokeza. Viogozi wakasahau na kutupilia mbali kuwafanyia kazi wananchi wakaanza kuwa MAFISADI wasio shikika. Walifanya kila kile kinachofanywa na Uongozi Uliopo sasa. Wananchi wakaanza kutoa kilio kama wanvyofaya sasa. Hali ilikuwa kama hii iliyoko sasa tuseme kwa VALUE NA PRINCIPLES.

DAWA:

Mkutano wa kamtikuu Ulikaa Arusha 1967; Waka pitisha "MIIKO" iliyowabana Viongozi kuwategemea wananchi kama watumwa wao. MIIKO hiyo ambayo ilikuwa SAHIHI kabisa kwa wakati ule.

Kilichofanyaka 1967 Kimsingiilikuwa Ni Kuunganisha AGANO LA UHURU(KUJITEGEMEA KIUCHUMI KWA KULA "FAMILIA" YA MTANZANIA) na AZIMIO LA ARUSHA(MIIKO YA UONGOZI). Hii ikwa ndio dira ya mulekeo wa Taifa.
Mtu mwenye link ya azimio la arusha atup. Unapo ondoa MIIKO YA UOGOZI taifa litayumba.

Azimio la Zanzibar? Lliliondoa MIIKO YA UONGOZI. LEO HII HAKUA MIIKO YA AINA YOYOTE..soma makala hapo juu ya Dr Shoo. NDIO MAANA LAZIMA MIIKO MIPYA ITUNGWE TENA HARAKA A HATA IKIBIDI IWEKWE KWENYE KATIBA MPYA!!! Bila hivyo UONGOZI utatumika kama Mradi (Nafikiri hiki ndicho kinamsuta MKAPA)na utanunuliwa hata kwa Gharama ANAZOZIJUA MWAIKIBAKI NA WAANACHI WAKE KWA SASA. "UOGOZI UTAKUWA NI DILI"Dr Shoo!!
 
http://www.ccmtz.org/nyaraka/azimiolaarusha.pdf

Nitasevu kopi ili CCM wasije lifuta au kumtuma Hasara na Fisadist walifute!

Mkuu REV; Nimepitia tena kwa makini doc. nzima; iko attached: nafikiri ni sawa kabisa Kusema kuwa Azimio La Arusha limejengwa na Nguzo Kuu mbili amabazo kila moja ilitokea Kwa wakati wake katika HISTORIA YA UUASISI WA TAIFA TANZANIA.

A: KUTIJTEGEMEA KIUCHUMI KWA KILA FAMILIA YA TANZANIA NA KILA MTANZANIA. = [ LENGO KUPIGANIWA UHURU ]

B: MIIKO YA UONGOZI.= [ KUZUIA VIONOZI KUWATEGEMEA WALE WANAOWAONGOZA ]

kwa hiyo narekebisha kidogo;

Kutoka:

Kilichofanyaka 1967 Kimsingiilikuwa Ni Kuunganisha AGANO LA UHURU(KUJITEGEMEA KIUCHUMI KWA KULA "FAMILIA" YA MTANZANIA) na AZIMIO LA ARUSHA(MIIKO YA UONGOZI). Hii ikwa ndio dira ya mulekeo wa Taifa.

Na kuwa:

Azimio la arusha KAMA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA = A: KUTIJTEGEMEA KIUCHUMI KWA KILA FAMILIA YA TANZANIA NA KILA MTANZANIA "kwa" [ LENGO LA KUPIGANIWA UHURU NA UTAIFA ]+ B: MIIKO YA UONGOZI "kwa" [ KUZUIA VIONGOZI KUWATEGEMEA WALE WANAOWAONGOZA,HUKU WAKIWAHUTUBIA WAO WAJITEGEMEE KWA JASHO LAO ]

VILIO VYA UFISADI NA KUKATA TAMAA KWA MTANZANIA LEO; Umetokana na kutikisika kwa nguzo moja ya Dira ya maendeleo ya Taifa. MIIKO YA UONGOZI. NGUZO HII IMESHIKILIWA NA GIZA NENE NA UKIWA MKUBWA.
Leo hakuna miiko, kikundi kidogo cha VIOGOZI kwa kisingizio cha azimio la zainzibar inaitikisa nchi kwa ufisadi. ONA MFANO MMOJA;WALIVYOCHEZEA JASHO LA WANANCHI HAPO BANK KUU:

HAKUNA MIIKO YENYE MENO SASAHIVI. Hata kama Pangekuwa na Misingi mizuri kiasi gani(UWEKEZAJI,MKUKUTA,MKUKUTA,MIKAKATI,M_CHOCHOTE!!) kwa nguzo ya kwanza ya Taifa kujitegemea, bila nguzo ya uhakika ya miiko YA UONGOZI : Dira ya maendeleo bado ingekuwa haitimiliki, viongozi mafisadi wangeharibu maendeleo ya Taifa tu, hasa ukitilia maanani nchi ya ulimwengu wa tatu. Miiko ya uongozi ni vigumu sana kuitunga na ikafanya kazi. Lakini tunasema hilo haifanyi isiwepo na isifanye kazi. Haiwezekani?? Basi lazima kitufulani kama hicho kiwezekane kuwadhibi mafisadi,Au?? Sasa Itakuwaje kama haitawezekana kuwabana mafisadi!!!?? Ona walivyosema kwa Nyerere, mara baada ya kuondoa MIIKO YA UONGOZI ::: "There are some of my friends who we did not allow to get rich; now they are getting rich and they say `See, we are getting rich now, so you were wrong'. But what kind of answer is that?::: Soma post ya MMMwanakiji.

Jana tumeona Wananchi wakivamia shamba la Gavana wa zamani. kila mmoja alisikia walichokuwa wanakidai(Tuwekeeni attachment) na ni nguvu gani imewasukuma kufanya vile. Ni Utovu wa Nidhamu na sio maadili mema ya Uongozi..blah.blah. etc. Lakini Tunaomba mtu mmoja afanye analisis ya kweli kabisa why that is happening na hata wawekaezaji wengine wenye mikataba mibovu wasijidangaye .. the same FORCE will fall upon them. Sio kweli?? hah ..hah.. Muulize kibaki kama aliwahi kuamini kuwa kinachotokea leo hii kwa Taifa lake kama kingetokea.

Mwenye uchugu sana. Ahamasishe na kuhakikisha Kurejea kwenye Maagano na Maazimio ya kimsingi, yaliyo asisi Taifa na kuacha kubabaisha na upofu usio saidia chochote zaidi ya kujiandaa kwa machafuko yasiyo kwepeka. LAKINI NI YA KUJITAKIA.

TUNAAMINI MUDA WA KUREJEA NA KUAFIKIANA UPO. HIMA HILO LIFANYIKE. HAKUNA SABABU YA KUSUBIRI MAMBO YAHARIBIKE ZAIDI YA YALIVYO SASA NDIPO MARIDHIANO YAANZE. Hatuhitaji kusikia viongozi wetu wanakimbilia mara sijui marekani, mara wamechupa wako sijui Malta, souz..etc..WHAT IS ALL THAT? Mifano ni mingi. Hatukatai kuwa Kenya hawatafikia Maridhiano lakini kwa Gharama Gani?

Tuache kujivuta vuta Tufungue macho turejee maagano na maazimio ya Msingi: JK nyrere tunamnukuu!

"...But I still think that in the end Tanzania will return to the values and basic principles of the Arusha Declaration..."


Kama hilo halitatokea Tunaomba tuonyeshwa Mbadala. Hasa kwenye NGUZO YA MIIKO YA VIONGOZI!
Mungu ibariki Tz.
 
Lakini azimio la Arusha lilikuwa ni sera ya Chama, na wala halikuwa kwenye katiba ya nchi, kwenye katiba ya nchi kulikuwa na sera ya Ujamaa tu(nampaka leo bado ipo)

kwa hiyo ukitaka kulirudisha azimio la arusha huna budi kulirudisha katika chama, au uunde chama kitakachokopa mawazo ya azimio la arusha. lakini usitegemee chama A,au B, kufuata sera hizo, kwa sababu na wao wana sera zao kuhusiana na mambo hayo hayo yanayozungumziwa na azimio la arusha.

sisi tunahitaji katiba bora, na sheria zilizowazi, sheria za haki, mambo ya mazimio ni mambo ya vyama na kila chama kikiingia madarakani kinaenda kutekeleza sera zake bila kuathiri sheria za nchi.

Kwa hiyo unless otherwise, ukitaka Azimio la Arusha lirudi halina budi kupitia katika mlango wa sheria na katiba,

lakini mbona sheria za uajiri na sheria za kazi zipo wazi tu?.lakini mafisadi bado wanazivunja, wanaiba kinyume cha sheria. kwa hiyo problem hapa siyo Azimio kutokuwepo ,problem ni law enforcement ,hata ukiwa na maazimio mia kama enforcement hakuna basi hakuna chochote kitakachofanyika.
 
Mimi pia nalikubali sana Azimio la Arusha. Ni kati ya vitabu vichache vya zamani nilivyonavyo. Kimsingi Azimio la Arusha ni falsafa ya TANU zaidi kuliko ya CCM. Kiitikadi, TANU ilikuwa kushoto mno, wakati CCM ilikwenda kulia sana wakati wa Mwinyi. Lakini leo hii, ideologically speaking, CCM is a bankrupt party now; they are just doing things without any reason other than to hold on power which is why any politician believing in ideological stance as a core part of a political party will find it hard to be a practical member of CCM.

In my view, to radically transform Tanzania from where it is now, we need a party that is a bit further away from the left of TANU but less to the right than CCM. This is where CHADEMA comes in very well. So, any movement of ideas that we will endeavour to undertake with a view to transforming our country we will eventually need a political party to put those ideas in practice. It is from this reality of the matter that I have always asked you guys to join CHADEMA massively and let's bring all those fantastic ideas at its disposal. We certainly don't need another moribund NGO in our country; we need a political party that will take us to the next step and for this,we need CHADEMA and CHADEMA needs us.
 
Lakini azimio la Arusha lilikuwa ni sera ya Chama, na wala halikuwa kwenye katiba ya nchi, kwenye katiba ya nchi kulikuwa na sera ya Ujamaa tu(nampaka leo bado ipo)

kwa hiyo ukitaka kulirudisha azimio la arusha huna budi kulirudisha katika chama, au uunde chama kitakachokopa mawazo ya azimio la arusha. lakini usitegemee chama A,au B, kufuata sera hizo, kwa sababu na wao wana sera zao kuhusiana na mambo hayo hayo yanayozungumziwa na azimio la arusha.

sisi tunahitaji katiba bora, na sheria zilizowazi, sheria za haki, mambo ya mazimio ni mambo ya vyama na kila chama kikiingia madarakani kinaenda kutekeleza sera zake bila kuathiri sheria za nchi.

Kwa hiyo unless otherwise, ukitaka Azimio la Arusha lirudi halina budi kupitia katika mlango wa sheria na katiba,

lakini mbona sheria za uajiri na sheria za kazi zipo wazi tu?.lakini mafisadi bado wanazivunja, wanaiba kinyume cha sheria. kwa hiyo problem hapa siyo Azimio kutokuwepo ,problem ni law enforcement ,hata ukiwa na maazimio mia kama enforcement hakuna basi hakuna chochote kitakachofanyika.

NAKUBALIANA NA HOJA ZAKO KIASI KIKUBWA:

KWANZA:

Tunapolichambua azimio la arusha kwa kinaganga ni kutaka kuwa onesha viogozi waliopo madarakani wapi wamepotoka na kwanini wamepotoka. Wapi wamesaliti kile walichosema wanakiamini, kukifuata NA KUKIFANYIA VIAPO. Tunawaonyesha kiundani NA OBJECTIVELY namna waliyoitumia kujisaliti wenyewe na wale waliosema wanawaongoza. Tunawaonyesha Maana ya kweli Ya Ujamaa, maana ya Kujitegemea, maana Ya UONGOZI na MIIKO yake.tuwawaonyesha madhara ya kukiukwa kwa hayo. Baada ya hayo, tunatoa mapendekezo bora zaidi tunayotegemea yatafuatwa na kutokuchezewa.

PILI;

DOC. iliyokuwa ni msingi wa maendeleo na ujenzi wa Taifa hili so far ilikuwa azimio la arusha kwa hiyo halitakwepa kufumuliwa na kuangliwa kwa kina kila na kwenye kila pembe yake. Na hatimaye kukarabatiwa. kama final product ya usahihi wake baadaye utatumiwa kwenye chama fulani au kwenye katiba ya taifa that is another thing. Kwani kama ni kufaulu au kushindwa kwetu ni doc. hiyo ilivyofuatiliwa au kutekelezwa. Hatufanyi yote haya kwa misingi ya itikadi au imani yeyote. kwani ukweli na ustawi wa jamii ni swala la kanuni,sheria na falsafa zilizosimamia ukweli katika ujenzi na utekelezaji wake. Ukweli huo unaweza kutumiwa na chama chochote au katiba ya nchi yeyote nk.

TATU;

Ni kweli dhana ya Ujamaa na kujitegemea ni swala la kikatiba. Na lilikuwa ni agano na dira ya kutafuta uhuru na kujenga uchumi. Ni KANUNI,DHANA, FALSAFA!INAJITGEMEA KAMA UKWELI UNAVYOJITEGEMEA BILA KUJALI CHOMBO CHA KUUBEBEA,CHAMA, NGO ETC UTEKELEZAJI WAKE ULIONYESHA MAPUNGUFU YASIYOKUWEPO KWENYE KATIBA. NAMNA YA KWELI KABISA YA "KUWABANA KWA DHATI MAFISADI VIONGOZI"

Ili kuepuka mchezo mchafu dhidi ya Sheria, Maagano na Maazimio muhimu ya Kitaifa:

BINAFSI HAPA NAUNGA MKONO KATIBA MPYA PAMOJA NA MAMBO MENGINE ITAKAYOKUWA HAITOI MWANYA KWA KILE KILICHONGOFOLEWA KWENYE AZIMIO LA ARUSHA NA MAPUNGUFU MENGNE YA KIUTEKELEZEJI.


Hii itatuepusha na Madhara ya kijamii ambayo yanaepukika kama tukitaka. Na hili lifanyike haraka. Natumaini wenye mamlaka na uongozi watafikishiwa au watayasoma haya na kuyafanyia kazi maramoja. Tuanategemea watakuwa na busara ya kuharakisha "MIITO YETU" kabla ya kulipeleka taifa pale mataifa yanayotuzunguka yalipofikia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom