Kila mtu na anavyojisikia,haina mana kama hawajalijua tatizo la zitto ndio kua sio Hospital ya mana sio kweli hata kidogo, ni Hospital nzuri na Doctors wake pia ni hodari kama huamini nenda utajua usinilewe vibaya au sikuombei uumwe la hashaaaa,au unaweza uliza watu hata watu wako wa karibu.......Ndugu wana JF
Hali alivyoeleza Mh Zitto inaonyesha wazi kuwa Aga Khan Hospital ni eneo la biashara. Kama kweli Malaria inawashinda je magonjwa mengine. Ni heri ukatibiwa temeke ukapata vipimo sahihi maana hii hali inatisha. Mimi binafsi nikianga aga khan sipati majibu ya kweli kuhusu home au chochote. Na hili la Zito limening'amua.
Tutafakari kama kuna mtu humu JF ni mtumishi wa AGA KHAN basi awafikishie taarifa.
hajawavunjia heshima maana kaongea ukweli. tatizo sio madaktari, ila ni maabara.Ingelikuwa nchi za nje, Hospitali ingelikwisha toa tamko kumlipua huyo Mbunge maana inaonyesha anawavunjia hadhi
Ukisoma kwenye ukurasa wake a facebook au mwananchi la leo amesema mgonjwa wa malaria madaktari wa muhimbili waliweza kugundua hilo na kumpa dazi ambayo mmemsaidia kupata nafuu, lakini kumbuka pia Zitto alikuwa na tatizo la kipanda uso ugonjwa ambao ukifikia hatua ambayo anayo zitto lazima ukafanyiwe operation na kwa mujibu wa Dr. Kimaryo alipendekeza Zitto aende India.Mimi sina tatizo na aghakhan,
tatizo ni kwanini kabwe apelekwe india,
wakati ugonjwa umeshafahamika,
kuna nini nyuma ya malaria ya zito.
Mkuu, wafanyakazi kwenye mahabara hawana ujuzi wa kutosha kugundua vimelea vya malaria, nilikwisha shuhudia tatizo hilo zaidi ya mara nne na familia yangu; atuwezi kusema ni bahati mbaya. Kitu kingine, wakijuwa unalipiwa na kampuni/mwajili basi wana kawaida ya kukurundikia madawa chungu mzima kutoka India, kama una ujuzi wa fani ya madawa ukiyachunguza unagundua mengine hayahitajiki kabisa wanacho tafuta pale ni ku-inflate bill kwa mwajiri - kuna udanganyifu mkubwa sana.Kila mtu na anavyojisikia,haina mana kama hawajalijua tatizo la zitto ndio kua sio Hospital ya mana sio kweli hata kidogo, ni Hospital nzuri na Doctors wake pia ni hodari kama huamini nenda utajua usinilewe vibaya au sikuombei uumwe la hashaaaa,au unaweza uliza watu hata watu wako wa karibu.......
Wala hauhitaji vifaa "hi-tech" kugundua Malaria. Kwenye Hospitali kubwa Kama Agha Khan and the likes huwa wanatumia vifaa hi-tech kwenye maabara zao kwa ujumla. Ni lazima Uwe na vijidudu wengi wa Malaria ili iweze kuonekana na hizo mashine zao. Mimi binafsi huwa naenda kwenye Zahanati wanazotumia Microscope na huwa napima katika Zahanati tatu tofauti ili kupata uhakika wa majibu, na mara nyingi majibu huwa yanafanana. Kutoweza kugundua Malaria Agha Khan haina maana ya kuwa Agha Khan Hospitali sio makini.Kwani ku detect malaria unahitaji vifaa hi-tech kiasi gani?
Well said mkuu, wana tabia ya ajabu sana - wanapenda sana kurundikia wagonjwa madawa chungu mzima, na ukiangalia karibu yote yanatoka India, na ukiangalia kwa umakini madawa mengi wala hayahitajiki - wanacho tafuta pale ni pesa tu hawajali kama madawa mengine yanaweza kuwadhulu watumiaji.Aga Khan pana matatizo makubwa ya kiutawala mimi binafsi na familia yangu nimeshaapa kutokutibiwa hapo, kulikuwa na Dr. Bigwa alikuwa muhimbili na alikuanafanya part time hapo aliamua kuacha kazi ili kulinda ethetics za udaktari, kumekuwa na tatizo la utawala kushinikiza madktari kuwandikia wagonjwa madawa zaidi au kufanya vipimo visivyohusiana na ungonjwa wenyewe ili waweze kupata hela. Pia kulazimisha wanawake kujifungua kwa operaotion badala ya njia ya kawaida. Nilimpeleka mzee wangu hapo mwaka jana akiwa na tatizo la maumivu ya mgongo wakamfanyia vipimo na kumpa dawa za kutumia lakini nilipata wasiwasi juu ya idadi ya dawa alizopewa nikawasiliana na Dr. aliacha kazi hapo kwani ni Baba mkwe wangu, aliniambia mzee asitumie hizo dawa mpaka tuonane naye pale muhimbili kesho mzee alipofanyiwa vipimo ilionekana ni kweli alikuwa na tatizo kama Aga Khan walivyobaini tatizo ni likiwa aina za dawa alizopewa baadhi yazo hazikulingana na ugonjwa aliyokuwa nao hapo ndipo Dr. Akanieleza kisa cha yeye kuamua kuacha kazi pale Aga Khan. My take nafikiri serekali inapaswa kupaangalia kwa jicho angavu.