Aga Khan kuachana na NHIF watu wanapiga kelele ila Serikali kufuta Bima ya Toto Afya Kadi hawaoni tatizo

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
516
1,348
Katika mitandao ya kijamii kuna hili la The Aga Khan Hospital linatajwa ila watu wanasahau mapema sana.

Tukumbushane kidogo tarehe
Machi 13, 2023 kutokea Dodoma, tulipata ujumbe huu kupitia vyombo vya habari ukisema.

"MABORESHO KATIKA UTARATIBU WA USAJILI WA WATOTO KUPITIA MPANGO WA TOTO AFYA KADI

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unapenda kuutangazia Umma kuwa, unafanya maboresho ya utaratibu wa usajili na huduma kwa watoto waliokuwa wanasajiliwa kupitia utaratibu wa Bima ya Afya ya "TOTO AFYA KADI". Hivyo, katika kipindi hiki cha maboresho, wazazi wanashauriwa kusajili watoto wao kama wategemezi kupitia Vifurushi vya Bima ya Afya au kupitia shule wanazosoma.

Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi fika katika ofisi za Mfuko zilizo karibu au wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja kupitia namba ya bila malipo 199.

Iliandaliwa na
Anjela A. Mziray
MENEJA UHUSIANO"

Ujumbe huo unaonekana kuibua maswali kuhusu mchakato wa malipo na gharama za huduma katika Hospitali ya Aga Khan ikilinganishwa na hospitali nyingine, Madai kwamba Aga Khan wanataka malipo ya juu zaidi yanaweza kuwa na ukweli kulingana na gharama za huduma zinazotolewa. Ni muhimu kutambua kwamba hospitali kubwa zinaweza kuwa na gharama za uendeshaji ambazo zinachangia kwenye bei za huduma.

Leo chawa wanaruka na Aga Khan Hospital kwa sababu wametoa sababu zao abazo serikali inatakiwa kuwa sikiliza na sababu hizo wanazijua wao sasa chawa wamepewa ujumbe wameanza kuruka nao! Kumbe mkuki kwa nguruwe ni mtamu ila kwa binadamu ni mchungu eeeeh!

"AGA KHAN MMEKOSA UTU NA KUWEKA MBELE MASLAHI KULIKO HUDUMA KWA WANANCHI.

Katika pita pita zangu mtandaoni nimekutana na taarifa iliyozua gumzo ambayo inahusu Hospitali ya Aga Khan kuiiomba NHIF isitishe mkataba wake wa utoaji wa huduma kwa sababu za kiuendeshaji.

Ilinistua na nikalazimika kwenda mbali zaidi ili kujua sababu ya suala hilo. Hakika niliumia sana kuona hospitali hii inalazimisha ilipwe mamilioni ya fedha na NHIF katika utoaji wa huduma zake, bei ambazo hata katika Hospitali nyinginezo tena zilizo ngazi ya juu ya rufaa ya matibabu.

Katika uchunguzi wangu nilioufanya nimebaini madudu mengi ambayo Aga Khan inataka kuibebesha Serikali mzigo wa kuongeza gharama zaidi za huduma kwa wateja wa NHIF kuliko kiwango cha juu kabisa cha malipo kwa huduma.
Nitatoa mifano michache ya huduma za kawaida kabisa ambazo Aga Khan imekuwa ikidai kuongezewa gharama hizo kwenye huduma wanazotoa kwa wateja wa NHIF.

* Hospitali ya Aga Khan wanataka kutoza Shilingi 6,000,000/= kwa huduma za kujifungua kwa njia ya upasuaji wakati Hospitali nyingine zenye hadhi sawa ya rufaa ya Kanda wanatoza kiasi cha Shilingi 230,000/= huku bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ikijumlisha na huduma ziada hutoza kiasi cha Shilingi 600,000/=. Aga Khan wanataka kulipwa maradufu kwa asilimia 100 zaidi kuliko Hospitali nyingine.

* Huduma ya kulaza wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Aga Khan wanataka kulipwa kiasi cha Shilingi 2,278,933, huduma hii kwenye Hospitali nyingine huwa ni kiasi cha shilingi 500,000/= na Shilingi 700,000/= ambayo ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada.

* Aga Khan wanataka kutoza kiasi cha Shilingi 334,546 kwa huduma za uchunguzi kwa kupitia CT-Scan huku Hospitali nyingine zinatoza 120,000 hadi 150,000 ikiwa ni bei ya juu katika baadhi ya Hospitali ukijumuisha na huduma za ziada. Kwanini bei iwe juu hivi? CT-Scan hizi hizi ambazo tumeona Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amezinunua na sasa huduma zinapatikana nchi nzima kwenye Hospitali zote za Rufaa za Mikoa na nyinginezo ngazi za juu. Najiuliza Gharama zote hizo zinakuja kwa msingi upi?

Ifahamike kuwa Aga Khan sio Hospitali ngazi ya Taifa hivyo bado rufaa zao zote wanalazimika kuzipeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili, hata kama ni Hospitali Binafsi ukiweka gharama za juu pamoja na huduma za ziada hawapaswi kuwa na tofauti kubwa ambayo inatishia uhai wa Mfuko.
Kama Taifa ifike mahali tutafakari endapo Aga Khan wana nia kweli ya kutoa huduma za matibabu au la? Je ni wananchi wangapi wataweza kupata huduma kwa gharama hizi katika hospitali hii? Au wamelenga tabaka gani la kulitibia?

Hata hivyo niipongeze sana Serikali kwa hatua kubwa ya kuboresha huduma za matibabu nchini huduma ambazo awali yawezekana zilipatikana nje ya nchi lakini sasa zinapatikana katika hospitali zetu za umma. Kwa hili kongole kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Viongozi wa na Watendaji wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Waziri jembe kabisa Mhe. Ummy Mwalimu.

Ninaamini kwamba katika utoaji wa huduma za matibabu, utu hupaswa kuwa kipaumbele cha kwanza na kuweka maslahi mapana ya kuokoa maisha ya binadamu.

Kwa leo niwaache na tafakari hii ya gharama kubwa zisizo na uzalendo za Aga Khan."

Hawa ni vijana wanaosema kwamba Aga Khan Hospital wamekiuka utaratibu wa NHIF hivyo wamepoteza utu wametanguliza pesa au maslahi kuliko afya za watu.

Nachotaka kuwaambia ni kwamba, hawa wanaosema Aga Khan Hospital wanatanguliza pesa mbona hawakupiga kelele pindi Toto afya kadi inafutwa na serikali kwa kigezo kwamba wanataka kuwasajili watoto kwanjia ya shule ili wajiandikishe wengi walikuwa wapi kukemea hili?

Kuendesha hospital kubwa kama Agha Khan sio mzaha sio siasa pale wanalipa mishahara mingi sana. Sasa kama mapato ni kidogo wafanyeje? Ukienda na bima lazima usubiri cash kwanza

Unaambiwa Aghakan wamekosa Utu kuliko waliotoa Bima ya Toto Afya.
Hii nchi ngumu sana 😂
 
Hii nchi watawala walichokosoea ni kuingiza siasa kwenye huduma za muhimu hasa afya, Umeme na Maji. Wamefeli vibaya mno
 
Back
Top Bottom