Kwa iwavyo vyovyote lazima mwanasheria yeyote kwa kulinda ofisi yake au bosi wake ama mteja wake hasa mwanasheria mkuu wa serikali atafute kifungu cha 'kuzuga na kuficha ukweli'. Hata kama katiba haijafafanua juu ya wabunge wanaoteuliwa na Rais juu ya kuapa kabla hawajateuliwa na Rais ukweli ni kwamba wote wanakuwa-defined na sense nzima ya nani anatambuliwa kuwa mbunge? Tukishapata ile tafsiri unaangalia sheria au katiba inasemaje? Sharti mojawapo lazima Mbunge aape kwanza kabla ya kushiriki shughuli zozote za kibunge na kwa maana hiyo hata kukamilisha kuitwa mbunge lazima awe ameapa, bila kuapa hawezi kushiriki shughuli za bunge. Je shughuli za kibnge ni zipi? Ina maana mawaziri hawa walioteuliwa na Kikwete hawatafanyakazi za kibunge hadi bunge la juni? Hawatashughulikia jambo lolote la kibunge kama kutekeleza maazimio ya bunge yakiwemo ya ufujaji wa fedha za umma na TBS scandal etc? Hivyo ndivyo hata Nassari na mbunge wa viti maalum wa chadema iliwatokea hivi karibuni kule Dodoma. Baada ya kuchaguliwa kwao na majina kuwasilishwa kwenye ofisi ya bunge ndipo ilipangwa siku ya kuapa hawakushiriki shughuli za bunge licha ya kuwepo dodoma na viwanja vya bungeni zaidi ya kupangiwa kufanya rehearsal tu. Hawa wateule wa Kikwete hata rehearsal ya kuapa bungeni hakuna achilia kuapa kwa spika hata katika ofisi ndogo za bunge Dar. Sasa sielewi kama Kikwete alikuwa ameitaarifu hata ofisi ya bunge juu ya uteuzi wa Saada Mkuya masaa machache kabla ya kumteua kuwa naibu waziri wa fedha. Japo ukihoji utaambiwa ofisi ya bunge ilikuwa imetaarifiwa. Hivi ndivyo wananchi tunavyofanywa zumbukuku tunafanywa, kana kwamba sote ni wajinga hata katika maswala ambayo hayahitaji ujuzi wa sheria bali yanataka logical thinking tu. Wananchi tuamke tuanze kukataa ukiukwaji wa katiba na sheria ikibidi hata twende mahakamani kupata tafsiri sahihi badala ya kuburuzwa kienyeji na mwanasheria mkuu anayetetea hata ukiukwaji wa sheria. Ndio maana hata alidiriki kusema hakuna haja ya katiba mpya sijui sasa anasemaje juu ya hilo baada ya mchakato kuanza?