AG: Ufafanuzi juu ya uteuzi wa wabunge na kupewa uwaziri

Wazanzibar wote ni watanzania lakini si watanzania wote ni wazanzibar. MATHEMATICALLY ni kwamba zanzibar is subset of tanzania.

So hakuna kilichokiukwa hapo mkuu!

Hahaha...umenifurahisha!
Nimekumbuka mambo ya hisabati SHUFWA na WITILI. Kuna moja hapo haigawanyiki kwa namba nyingine yeyote zaidi ya moja na yenyewe..hahaha!
 
Ukiangalia tovuti ya Bunge katika orodha ya wabunge jaji Werema ni mbunge kwa tiketi ya ccm!
AG anaingia bunguni by virtue of being AG ila hapigi kura!. Pia anahudhuria kikao cha baraza la mawaziri lakini hapigi kura. Hivyo sii kweli Jaji Werema ni mbunge kwa tiketi ya CCM!. Sina tatizo hata akiwa ni mwana CCM, tatizo langu ni professionalism yake inanitia mashaka sana!. Kama issue ya kiapo tuu anaborongo, hiyo mikataba mikubwa si ndio ataona giza kabisa!. No wonder kwa nini taifa linaingia mikataba ya ajabu kabisa!. Watu kama kina Werema kuendelea kuwepo, Tanzania tutaendelea kunyonywa mpaka tutabaki mifupa!. Yaani AG msima anathubutu kutangaza mbunge ambaye hajaapishwa eti ni mbunge!, kule kuapishwa ni kwa nini?. Kama ni kuchaguliwa na wananchi, rais na wabunge wote wanachaguliwa, kwa nini rais tuu ndie awe president elect na wabunge wasiwe?. Huyu AG afunzwe sheria upya!. Mimi naisubiri tafsiri ya Shivji maana hata mahakama nina mashaka nayo!.
 
Hayo ndiyo matatizo ya kuwa na Rais mwenye mamlaka makubwa sana 9Urais wa kifalme). Wananchi waelimishwe kuhusu mapungufu haya kwenye hii katiba ili katika katiba mpya yasahihishwe. Haingii akilini mtu mmoja kuteua wabunge 10 mwenyewe na kuwateua watu wote wenye mamlaka. Lazima mamlaka yagawanywe sasa mengine yaende kwa Bunge, mengine Mahakama na mengine kwa Waziri Mkuu.
 
Wakuu hivi kwa nini watu wote ambao huchaguliwa ama kuteuliwa kushika madaraka ya umma lazima waape? Hapa nina maana ya kiapo chochote kile lakini lazima waape. Kiapo kina maana gani? Kwa nini wasishike tu hayo madaraka bila kuapa?

Mgombea urais akitangazwa na Tume ya Uchaguzi kuwa ameshinda uchaguzi hakuna chombo ama mtu yeyote annayeweza kuhoji ushindi huo mahala popote pale hivyo anakuwa ni Rais kwa kuwa huwezi kwensa popote kutengua ushindi huo. Lakini mbona huyo mtu aliyeshinda hachukui madaraka ya Urais hadi aape? Si angekuwa akishatangazw tu basi anaanza kazi ya Urais?
Basi kiapo kinaonekana kina imuhimu wake kisheria.

Naomba msaada.
 
Ikumbukwe kuwa Raisi aliteua wabunge 3 toka Zanziba i.e Mbarawa,Nahoza na Meghji vilevile Meghli alishawahi kuongoza wizara ambazo si za muungano hapo nyuma i.e Utalii na afya.Nadhani hata mtu wa Zenji anaruhusiwa wizara zingine.

1. Prof Mbawara anaongoza Science & Technology = hii imeongozwa kwenye list ya wizara za muungano
2. Nahodha alikuwa Home affaira na sasa kaenda Defense = hizi zito ni wizara za muungano from inception
3. Meghji - kaolewa Tanzania Bara (Marehemu mume wake Prof Meghji) ni mtu wa Tanzania bara, alikuwa anafundisha chuo cha ushirika Moshi. Mama Meghji pia amewahi kuwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na kutoka hapo ndipo akaingia bungeni kupitia viti maalum. Kwa kifupi huyo mama anahesabika kama mtu wa Tanzania Bara (walau kwa tafrisi ya ndoa za kwetu)

Jambo moja ambalo ni wazi ni kwamba watanzania wa sasa wana uelewa mpana na wanauliza pale wanapoona mambo hayaendi sawasawa. Wakubwa wengi wamekulia kwenye viti vya enzi, na huko nyuma hakukuwa na mtu wa kuuliza wala kukohoa ndio maana hawaoni aibu kutoa majibu ya hovyo kwa makosa yaliyo wazi maana bado wanafikiri watanzania 'hawaelewi' chochote.
 
JK was right as well as AG is right! katiba haijavunjwa na AG ametoa maelezo mazuri na yanayokubalika kikatiba hasa kwa mtu ambaye hatokuwa mvivu ku-refer katiba, kiapo cha bungeni si cha kumthibitisha mtu kuwa mbunge kwa kuwa mtu anakuwa mbunge halali mara baada ya kutangazwa na mkurugenzi wa uchaguzi wa jimbo husika au mara baada ya kuteuliwa na rais, hali kadhalika na kwa wabunge wa viti maalum, kiapo cha bungeni kinamwezesha mbunge kushiriki shughuli za bunge, na maudhui ya kiapo ni uaminifu kwa bunge na si kiapo cha kuwa mbunge, marehemu sumari hakuapa bungeni lakini katika siku zote hizo alihesabika kuwa ni mbunge halali wa arumeru mashariki!
 


“Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge”



Sharti la pili, litahusu kiapo cha Uaminifu katika Bunge kabla Mbunge hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge kwa masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba. Viapo hivyo havitegemeani na vinaweza kufanyika kwa nyakati tofauti.






Imetolewa na Jaji Frederick M. Werema (Mb)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
06 Mei, 2012

Kuwa waziri ni majukumu ya kibunge au la?

Kama katiba inamkataza Mbunge kufanya shughuli za kibunge kabla ya kuapa na pili Waziri au naibu ni lazima atokane na wabunge, Je shughuli za kibunge ni zipi?
 
Angetoa mfano basikama imewahi kutojea rais akanwapisha mtu kuwa waziri kabla mtu huyo hajaapishwa kuwa mbunge ingeoneshaana hoja sasa hivi amejaribu kuhalalisha kilichoharimishwa. Na yeye kama wengine wanawekatafsiri yao juu ya "shughuli za bunge"na kuzifunga kwenye kile kinachofanyika ndan ya bungeni. Kuna haja ya kufungua kesi ya kikatiba hapa.
This is a serious constitutional crisis. Mwanasheria makini angedefine neno " shughuli za bunge" kwa kuangalia mischief behind article 68. Shughuli pekee ambayo Mbunge anaweza kufanya bila kuapishwa ni kuchagua spika wa bunge. Hii Ndio sababu ya kusema hayo maneno.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Yaani kwa watu nisiowapenda kutokana na ubabaishaji wao ni huyu m-baba anayeitwa AG. Mzee mpumbavu sana huyu kwa kiasi kikubwa anaidhalilisha sana taaluma ya sheria. Watu aina ya Werema wako tayari hata kutetea kiny.si!! Wanatuona sisi wa-TZ mazoba wa kukubali uozo wowote! Nafikri huu utetezi wakajadili yeye na nyanya yake, nyamb.ff! Tumechoka Bwana!
 
Hili likatiba letu nalo ni matatizo. Nimepita Ibara ya 66 nimegundua kumbe ni kweli Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Mbunge. Nukuu hii hapa Wakuu:-

66.



(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwa na aina zifuatazo za Wabunge, yaani-

(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi;

(b) Wabunge wanawake wa idadi inayoongezeka, kuanzia asilimia ishirini ya Wabunge waliotajwa katika aya ya (a), (c ) na (d), itakayotajwa mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi kwa taarifa iliyochapishwa katika Gazeti la Serikali baada ya kupata kibali cha Rais, watakaochaguliwa na vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni, kwa mujibu wa ibara ya 78, na kwa kuzingatia masharti ya uwiano wa uwakilishi baina ya vyama hivyo;



(c) Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wake;

(d) Mwanasheria Mkuu;

(e) Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa ibara ya 67, isipokuwa sifa iliyotajwa katika ibara ya 67(1)(b).


Congatulation Werema!

TUMBIRI wa JF
 
Na vipi kuhusu Hussein Mwinyi kuwa Waziri katika Wizara isiyo ya Muungano??


Mimi naona nchi tunachanganyana tu, AG hajui hata tafsiri ya working tool ya taaluma yake, hadi aibu!! Mimi namuona kama mtu unaposema kuwa sheria omtambue mme wakati wa kufunga ndoa ila isjali jinsia yake, mfano ni sawa na kusema mme anakuwa mtu yoyote anayefunga ndoa mbele ya mazabau lakini ukiulizwa jinsia yake isiwe na umhimu!! Ndo sawa na kusema waziri atateuliwa katika wabunge ila haihitaji sifa kamili ya kumfanya mtu kuwa mbunge ambayo ni kula kiapo cha bungeni. Hawa ndg wamechanganyikiwa hadi wanasahau vitu vya msingi. Kwa kweli watanzania tunahitaji kufanya maamuzi mazito.
 
1. Prof Mbawara anaongoza Science & Technology = hii imeongozwa kwenye list ya wizara za muungano
2. Nahodha alikuwa Home affaira na sasa kaenda Defense = hizi zito ni wizara za muungano from inception
3. Meghji - kaolewa Tanzania Bara (Marehemu mume wake Prof Meghji) ni mtu wa Tanzania bara, alikuwa anafundisha chuo cha ushirika Moshi. Mama Meghji pia amewahi kuwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na kutoka hapo ndipo akaingia bungeni kupitia viti maalum. Kwa kifupi huyo mama anahesabika kama mtu wa Tanzania Bara (walau kwa tafrisi ya ndoa za kwetu).

Mkuu
FJM,
Mbona umepapasa wachache. Vipi kuhusu Hussein Mwinyi?

TUMBIRI wa JF

 
Kuwa waziri ni majukumu ya kibunge au la?

Kama katiba inamkataza Mbunge kufanya shughuli za kibunge kabla ya kuapa na pili Waziri au naibu ni lazima atokane na wabunge, Je shughuli za kibunge ni zipi?
kwanini inakuwa ngumu kueleweka!? shughuli za bunge ni zile zinazohusiana na bunge na zinazofanyika bungeni ili kushiriki lazima uape lakini kabla ya kuapa mbunge anaweza kutekeleza majukumu mengine jimboni kwake kama kuhudhuria mabaraza ya udiwani, kusimamia miradi n.k it's very simple to understand!
 
JK was right as well as AG is right! katiba haijavunjwa na AG ametoa maelezo mazuri na yanayokubalika kikatiba hasa kwa mtu ambaye hatokuwa mvivu ku-refer katiba, kiapo cha bungeni si cha kumthibitisha mtu kuwa mbunge kwa kuwa mtu anakuwa mbunge halali mara baada ya kutangazwa na mkurugenzi wa uchaguzi wa jimbo husika au mara baada ya kuteuliwa na rais, hali kadhalika na kwa wabunge wa viti maalum, kiapo cha bungeni kinamwezesha mbunge kushiriki shughuli za bunge, na maudhui ya kiapo ni uaminifu kwa bunge na si kiapo cha kuwa mbunge, marehemu sumari hakuapa bungeni lakini katika siku zote hizo alihesabika kuwa ni mbunge halali wa arumeru mashariki!

Unarudia makosa yale yale ya AG. Waziri au naibu Wazira lazima awe mbunge. Katiba haitoi exemption. Ni mbunge, basi. Kwa tafsiri rahisi sana ni kwamba waziri au naibu waziri anafanya kazi za kibunge. Waziri au naibu waziri anahuduria vikao vya kamati za bunge, anaanda bajeti, anaanda majibu ya wawakilishi wa wananchi (wabunge wenzake). Sasa watafanya hizi kazi kama nani? wabunge wateule? Kama kiapo sio tatizo kwa nini kiwepo?

Kuhusu Marehemu Summari. Strictly speaking, marehemu Summari bado alikuwa mbunge mteule maana hakuwa amekula kiapo.
 
Zamani nilidhani matatizo yetu yanasababishwa na umasikini kumbe ni viongozi, leo AG ameni-prove wrong. Kutatu-cost dolla ngapi pesa za kigeni kama hao wabunge watasubiri june kuapishwa ndipo waanze kazi, tunakimbilia wapi mbona tupo hapa hapa Tanzania? Kwanini serikali inafanya kazi kwa zima moto staili. Juzi mbunge anateuliwa saa nane saa kumi anakuwa waziri why? ina maana rais hana short and long-plan hasa kwa post nyeti kama wizara ya fedha, analeta substitute dakika za nyongeza. There must be something wrong somewhere in ikulu, surely we need total overhaul of the government.

Rais wetu huyu ni mgawa vyeo haangalii ubora? Kama ingekuwa ni kufikiria angekuwa amefanya hivyo siku nyingi lakini ndani ya siku au ndani ya masaa kweli utapataje mtu makini na umemchunguza vipi strength na weakness zake au vetting? Huyu alikuwa anabahatisha tu, akiambiwa na mtu wake wa karibu yupo fulani namfahamu au ndugu yangu basi anajaza orodha yake.
 
Mwanakijiji. Usisahau hatujaanzisha mahakama ya katiba kama zilivyo nchi nyingine. Ila kwa hapo mm pia sioni km kunasheria imevunjwa na pia kusema kutoa mfano wa uteuzi kama huo uliowahi kufanyika kabla sioni mashiko yake maana
mahitaji hayakujitokeza b4.
b
Mahakama kuu chini ya ibara ya 107 ina unlimited jurisdiction katika utoaji haki.
 
Kama wanasheria wetu ndo mbu-mbu-mbu kiasi hiki, basi tusipoangalia siku moja tutapata na viongozi wasioapishwa kabisa! Hata sisi ma-layman wa sheria tunaweza kuona kabisa kwamba mwanasheria anapindisha katiba wazi wazi.
 
Back
Top Bottom