AG: Ufafanuzi juu ya uteuzi wa wabunge na kupewa uwaziri

Kwa iwavyo vyovyote lazima mwanasheria yeyote kwa kulinda ofisi yake au bosi wake ama mteja wake hasa mwanasheria mkuu wa serikali atafute kifungu cha 'kuzuga na kuficha ukweli'. Hata kama katiba haijafafanua juu ya wabunge wanaoteuliwa na Rais juu ya kuapa kabla hawajateuliwa na Rais ukweli ni kwamba wote wanakuwa-defined na sense nzima ya nani anatambuliwa kuwa mbunge? Tukishapata ile tafsiri unaangalia sheria au katiba inasemaje? Sharti mojawapo lazima Mbunge aape kwanza kabla ya kushiriki shughuli zozote za kibunge na kwa maana hiyo hata kukamilisha kuitwa mbunge lazima awe ameapa, bila kuapa hawezi kushiriki shughuli za bunge. Je shughuli za kibnge ni zipi? Ina maana mawaziri hawa walioteuliwa na Kikwete hawatafanyakazi za kibunge hadi bunge la juni? Hawatashughulikia jambo lolote la kibunge kama kutekeleza maazimio ya bunge yakiwemo ya ufujaji wa fedha za umma na TBS scandal etc? Hivyo ndivyo hata Nassari na mbunge wa viti maalum wa chadema iliwatokea hivi karibuni kule Dodoma. Baada ya kuchaguliwa kwao na majina kuwasilishwa kwenye ofisi ya bunge ndipo ilipangwa siku ya kuapa hawakushiriki shughuli za bunge licha ya kuwepo dodoma na viwanja vya bungeni zaidi ya kupangiwa kufanya rehearsal tu. Hawa wateule wa Kikwete hata rehearsal ya kuapa bungeni hakuna achilia kuapa kwa spika hata katika ofisi ndogo za bunge Dar. Sasa sielewi kama Kikwete alikuwa ameitaarifu hata ofisi ya bunge juu ya uteuzi wa Saada Mkuya masaa machache kabla ya kumteua kuwa naibu waziri wa fedha. Japo ukihoji utaambiwa ofisi ya bunge ilikuwa imetaarifiwa. Hivi ndivyo wananchi tunavyofanywa zumbukuku tunafanywa, kana kwamba sote ni wajinga hata katika maswala ambayo hayahitaji ujuzi wa sheria bali yanataka logical thinking tu. Wananchi tuamke tuanze kukataa ukiukwaji wa katiba na sheria ikibidi hata twende mahakamani kupata tafsiri sahihi badala ya kuburuzwa kienyeji na mwanasheria mkuu anayetetea hata ukiukwaji wa sheria. Ndio maana hata alidiriki kusema hakuna haja ya katiba mpya sijui sasa anasemaje juu ya hilo baada ya mchakato kuanza?
 
Mi naona ndg. yetu Mbatia naye ameshakuwa msaliti, maana alikuwa mtetezi wa wanyonge, sasa ni mtetezi wa tumbo lake, anafumbia ukiukwaji mkubwa wa katiba kisa na yeye yumo kwenye orodha. Kama ataanza kulipwa mshahara na posho mwezi huu kabla ya kuapishwa utakuwa ni wizi na CAG itabidi achukue hatua.
 
Mbona AG pia hajatolea ufafanuzi wa Dk. Mwinyi kupewa Wizara isiyo ya Muungano. Je, napo Rais hajavunja katiba? Mbona hakuna Mtanganyika aliyeshika wizara yoyote Zanzibar?

Wazanzibar wote ni watanzania lakini si watanzania wote ni wazanzibar. mathematically ni kwamba zanzibar is subset of tanzania.

So hakuna kilichokiukwa hapo mkuu!
 
"It is error alone which needs the support of government. Truth can stand by itself."
 
walewale! Hana jipya. Katumwa kusafisha njia maana kesho wanaapishwa kinyume cha katiba. Tuna viongozi wabovu sana. Mtu anatumwa kukiuka taaluma yake kwa sababu za kisiasa na yupo tayari! Hovyo kabisa!!!?

fungua kesi mahakamani!!
 
Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe 4 Mei, 2012 alitangaza mabadiliko katika safu ya Baraza la Mawaziri. Katika uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Mheshimiwa Rais aliwateua Mawaziri wapya kutoka miongoni mwa Wabunge aliokuwa amewateua na kuwatangaza. Baada ya uteuzi huo, kumetolewa maoni kwamba hatua ya Mheshimiwa Rais kuwateua Wabunge Wapya ambao hawajaapishwa Bungeni kuwa Mawaziri ni kitendo cha uvunjaji wa Katiba.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayachukulia maoni haya kama ni jambo lenye maslahi ya jamii na linalohitaji kufafanuliwa; kwa upande mmoja lakini pia, kutolewa kwa elimu ya Umma; kuhusu Mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge.

Msingi wa Katiba tunaoanza nao ni maelekezo ya masharti yaliyomo kwenye Ibara ya 55(4) kwamba:

“Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge”

Pili, ni mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge aliyopewa na masharti ya Ibara ya 66(1)(e) yenye aina ya Wabunge wasiozidi kumi watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za ibara ya 67 na angalau Wabunge watano kati yao wakiwa Wanawake. Wabunge aliowateuwa Mheshimiwa Rais wanatokana na Ibara hii.

Tatu, baada ya hatua zote hizi ikumbukwe kwamba aliyeteuliwa au kuchaguliwa kuwa Mbunge anakuwa Mbunge ama baada ya kutangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi; au baada ya kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa wale Wabunge wa viti maalum au anapochaguliwa na Baraza la Wawakilishi au anapoteuliwa na Rais akitumia Mamlaka yake ya uteuzi yanayotokana na Ibara ya 66(1)(e). Hivyo Wabunge wanaohusika hawahitaji kuapishwa kwanza Bungeni ili wawe Wabunge. Kiapo cha Mbunge Bungeni kinamwezesha tu kushiriki katika shughuli za Bunge.

Katiba ya nchi haiweki kwa Rais masharti kwamba kabla ya kumteua Mbunge wa aina hiyo kuwa Waziri au Naibu Waziri Mbunge huyo awe ameapishwa Bungeni kwanza. Masharti mawili muhimu na ya kuzingatia ni kwamba mteule wa nafasi ya uwaziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka kwa mujibu wa Ibara ya 56 ya Katiba, awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge. Sharti la pili, litahusu kiapo cha Uaminifu katika Bunge kabla Mbunge hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge kwa masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba. Viapo hivyo havitegemeani na vinaweza kufanyika kwa nyakati tofauti.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inasisitiza kwamba Wabunge ambao hawajaapishwa ndani ya Bunge ni Wabunge na wanapoteuliwa kushika nafasi ya Uwaziri au Naibu Waziri ni halali kwa kuwa uteuzi huo haukiuki masharti yoyote ya Kikatiba au Sheria. Aidha, katika kutekeleza madaraka ya kazi ya Uwaziri au Naibu Waziri Mbunge atahitaji kiapo mbele ya Rais hata kama hajaapishwa Bungeni. Busara ya uandishi wa Katiba na Sheria imetambua kwamba kunaweza kukatokea uteuzi wa aina hiyo wakati Bunge limeahirishwa kama ilivyo sasa. Masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba yatazingatiwa katika kikao cha Bunge kijacho.

Bila shaka ufafanuzi huu utaleta uelewa katika jambo hili na kuepusha mikangayiko isiyokuwa ya lazima.

Imetolewa na Jaji Frederick M. Werema (Mb)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
06 Mei, 2012

spin doctor at work

Watanzania wa leo si mabwege tena.
 
Nashauri AG aombe msamaha kwa ukiukwaji wa katiba na hatimaye tuone katiba inafuatwa.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Zamani nilidhani matatizo yetu yanasababishwa na umasikini kumbe ni viongozi, leo AG ameni-prove wrong. Kutatu-cost dolla ngapi pesa za kigeni kama hao wabunge watasubiri june kuapishwa ndipo waanze kazi, tunakimbilia wapi mbona tupo hapa hapa Tanzania? Kwanini serikali inafanya kazi kwa zima moto staili. Juzi mbunge anateuliwa saa nane saa kumi anakuwa waziri why? ina maana rais hana short and long-plan hasa kwa post nyeti kama wizara ya fedha, analeta substitute dakika za nyongeza. There must be something wrong somewhere in ikulu, surely we need total overhaul of the government.
 
Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe 4 Mei, 2012 alitangaza mabadiliko katika safu ya Baraza la Mawaziri. Katika uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Mheshimiwa Rais aliwateua Mawaziri wapya kutoka miongoni mwa Wabunge aliokuwa amewateua na kuwatangaza. Baada ya uteuzi huo, kumetolewa maoni kwamba hatua ya Mheshimiwa Rais kuwateua Wabunge Wapya ambao hawajaapishwa Bungeni kuwa Mawaziri ni kitendo cha uvunjaji wa Katiba.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayachukulia maoni haya kama ni jambo lenye maslahi ya jamii na linalohitaji kufafanuliwa; kwa upande mmoja lakini pia, kutolewa kwa elimu ya Umma; kuhusu Mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge.

Msingi wa Katiba tunaoanza nao ni maelekezo ya masharti yaliyomo kwenye Ibara ya 55(4) kwamba:

“Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge”

Pili, ni mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge aliyopewa na masharti ya Ibara ya 66(1)(e) yenye aina ya Wabunge wasiozidi kumi watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za ibara ya 67 na angalau Wabunge watano kati yao wakiwa Wanawake. Wabunge aliowateuwa Mheshimiwa Rais wanatokana na Ibara hii.

Tatu, baada ya hatua zote hizi ikumbukwe kwamba aliyeteuliwa au kuchaguliwa kuwa Mbunge anakuwa Mbunge ama baada ya kutangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi; au baada ya kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa wale Wabunge wa viti maalum au anapochaguliwa na Baraza la Wawakilishi au anapoteuliwa na Rais akitumia Mamlaka yake ya uteuzi yanayotokana na Ibara ya 66(1)(e). Hivyo Wabunge wanaohusika hawahitaji kuapishwa kwanza Bungeni ili wawe Wabunge. Kiapo cha Mbunge Bungeni kinamwezesha tu kushiriki katika shughuli za Bunge.

Katiba ya nchi haiweki kwa Rais masharti kwamba kabla ya kumteua Mbunge wa aina hiyo kuwa Waziri au Naibu Waziri Mbunge huyo awe ameapishwa Bungeni kwanza. Masharti mawili muhimu na ya kuzingatia ni kwamba mteule wa nafasi ya uwaziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka kwa mujibu wa Ibara ya 56 ya Katiba, awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge. Sharti la pili, litahusu kiapo cha Uaminifu katika Bunge kabla Mbunge hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge kwa masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba. Viapo hivyo havitegemeani na vinaweza kufanyika kwa nyakati tofauti.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inasisitiza kwamba Wabunge ambao hawajaapishwa ndani ya Bunge ni Wabunge na wanapoteuliwa kushika nafasi ya Uwaziri au Naibu Waziri ni halali kwa kuwa uteuzi huo haukiuki masharti yoyote ya Kikatiba au Sheria. Aidha, katika kutekeleza madaraka ya kazi ya Uwaziri au Naibu Waziri Mbunge atahitaji kiapo mbele ya Rais hata kama hajaapishwa Bungeni. Busara ya uandishi wa Katiba na Sheria imetambua kwamba kunaweza kukatokea uteuzi wa aina hiyo wakati Bunge limeahirishwa kama ilivyo sasa. Masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba yatazingatiwa katika kikao cha Bunge kijacho.

Bila shaka ufafanuzi huu utaleta uelewa katika jambo hili na kuepusha mikangayiko isiyokuwa ya lazima.

Imetolewa na Jaji Frederick M. Werema (Mb)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
06 Mei, 2012

AG makes me laugh!what a a joke!full usanii!haya twende tutafika,na mtakuja kuyajibu hata mkipelekwa na machela mahakamani mtayajibu tu!
 
Tena nimepata kigezo kingine, Sheria ya uchaguzi kifungu cha 48(3) inatamka kuwa, Mbunge akijihudhuru, akifa, ama kiacha nafasi yake kwa namna yoyote ile anayepaswa kutoa taarifa ni Spika. Kama anayosema Werema ni kweli, basi swali linakuja, endapo wabunge hawa wateule wakitaka kujiuzuru kabla ya tarehe 12/6/2012 siku ya kuanza kwa bunge, anayetoa taarifa hiyo ni nani? Je, ni Bunge? Hata kama wakipata dharura, kwa mfano Mbatia, je, Bunge litawajibika kama mbunge, ama itakuwaje? Hoja ya mwisho, mbunge mteule anaweza kujiuzuru ubunge ama anakataa tu uteuzi?
 
Mwanakijiji. Usisahau hatujaanzisha mahakama ya katiba kama zilivyo nchi nyingine. Ila kwa hapo mm pia sioni km kunasheria imevunjwa na pia kusema kutoa mfano wa uteuzi kama huo uliowahi kufanyika kabla sioni mashiko yake maana
mahitaji hayakujitokeza b4.

Angetoa mfano basikama imewahi kutojea rais akanwapisha mtu kuwa waziri kabla mtu huyo hajaapishwa kuwa mbunge ingeoneshaana hoja sasa hivi amejaribu kuhalalisha kilichoharimishwa. Na yeye kama wengine wanawekatafsiri yao juu ya "shughuli za bunge"na kuzifunga kwenye kile kinachofanyika ndan ya bungeni. Kuna haja ya kufungua kesi ya kikatiba hapa.
 
Hii nifunika kombe,mbona aja tufafanulia swala la Huseni mwinyi kuteuliwa kua waziri wa Afya akati wizara ya Afya aipo kwenye swala la Muungano?ikumbukwe kua Huseni Mwinyi alipewa uwaziri wa Ulinzi sababu wizara hii ipo kimuungano.ikumbukwe pia Huseni Mwinyi alipo kua naibu waziri wa Afya alikua nimbunge wa bara,sasa ivi Huseni sio mbunge wa bara.Je pia katiba aija vunjwa?
 
Jamani labda sijafuatilia vizuri mada hii. Hivi hawa wabunge walioteuliwa na rais (nominated MPs) na kuwa mawaziri watafanyaje ile michakato ya kuandaa budget na mielekeo yake katika kamati za Bunge ambazo zitaanza kukutana hivi punde? Chukulia wizara ya fedha kwa mfano -- wote watatu -- yaani Waziri (na manaibu wake wawili) ni nominated MPs na wizara hiyo ndiyo wizara mama katika masuala ya kuandaa budget.

Watajibizana vipi na wajumbe wa kamati au hizo hazichukuliwi kama ni shughuli za Bunge? AG Werema afafanue hapo!
 
Mkuu Invicible, asante kutuletea taarifa hiyo ya AG humu na huu ni moja tuu ya uthibitisho jinsi tulivyo na wanasheria vilaza wa kutupwa!.

Kwa vile sheria zetu nyingi tumerithi tafsiri sahihi ya kiapo ni "taking an oarth to the office". Kama rais akisha chaguliwa na wananchi na kutangazwa na NEC kuwa ni mshindi, kwanini hawi rais mpaka baada ya kiapo?. Kama mbunge akishatangazwa basi ni mbunge kile kiapo ni cha nini?.

Mhe. Werema asituletee ukilaza wake wa kutafsiri sheria ndivyo sivyo, kiukweli rais akiwaapisha wale wabunge wateule wake hiyo kesho atakuwa amevunja katiba na hii sii mara ya kwanza kwa rais kuvunja katika huku AG ameshona mdomo!.

JK alipoyasamehe yale majizi ya EPA, alitumia mamlaka gani?. Obstruction of justice ni criminal offence as well, mbona hawamshauri rais asivunje katiba!.

Katiba inasema rais atateu mawaziri miongoni mwa wabunge, mbunge hawi mbunge bila kuapishwa!.

Nasisitiza AG wetu ni kilaza mpaka basi!.

Nawahakikishia, JK akiwaapisha hao mawaziri watatu hiyo kesho, Jumanne asubuhi watu wanatinga mahakamani kuiomba mahakama kuu itoe tafsiri halisi Mbunge ni nani?.
 
Mh. AG umesema viapo vya uwaziri na ubunge vyaweza kufanyika kwa nyakati tofauti.
Issue: Ni kwa mpangilio gani? Kipi kinaanza au ni zig- zag tu? Na kama ni hivyo hivi vifungu vya katiba vina mantiki kweli?
Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe 4 Mei, 2012 alitangaza mabadiliko katika safu ya Baraza la Mawaziri. Katika uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Mheshimiwa Rais aliwateua Mawaziri wapya kutoka miongoni mwa Wabunge aliokuwa amewateua na kuwatangaza. Baada ya uteuzi huo, kumetolewa maoni kwamba hatua ya Mheshimiwa Rais kuwateua Wabunge Wapya ambao hawajaapishwa Bungeni kuwa Mawaziri ni kitendo cha uvunjaji wa Katiba.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayachukulia maoni haya kama ni jambo lenye maslahi ya jamii na linalohitaji kufafanuliwa; kwa upande mmoja lakini pia, kutolewa kwa elimu ya Umma; kuhusu Mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge.

Msingi wa Katiba tunaoanza nao ni maelekezo ya masharti yaliyomo kwenye Ibara ya 55(4) kwamba:

“Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge”

Pili, ni mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge aliyopewa na masharti ya Ibara ya 66(1)(e) yenye aina ya Wabunge wasiozidi kumi watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za ibara ya 67 na angalau Wabunge watano kati yao wakiwa Wanawake. Wabunge aliowateuwa Mheshimiwa Rais wanatokana na Ibara hii.

Tatu, baada ya hatua zote hizi ikumbukwe kwamba aliyeteuliwa au kuchaguliwa kuwa Mbunge anakuwa Mbunge ama baada ya kutangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi; au baada ya kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa wale Wabunge wa viti maalum au anapochaguliwa na Baraza la Wawakilishi au anapoteuliwa na Rais akitumia Mamlaka yake ya uteuzi yanayotokana na Ibara ya 66(1)(e). Hivyo Wabunge wanaohusika hawahitaji kuapishwa kwanza Bungeni ili wawe Wabunge. Kiapo cha Mbunge Bungeni kinamwezesha tu kushiriki katika shughuli za Bunge.

Katiba ya nchi haiweki kwa Rais masharti kwamba kabla ya kumteua Mbunge wa aina hiyo kuwa Waziri au Naibu Waziri Mbunge huyo awe ameapishwa Bungeni kwanza. Masharti mawili muhimu na ya kuzingatia ni kwamba mteule wa nafasi ya uwaziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka kwa mujibu wa Ibara ya 56 ya Katiba, awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge. Sharti la pili, litahusu kiapo cha Uaminifu katika Bunge kabla Mbunge hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge kwa masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba. Viapo hivyo havitegemeani na vinaweza kufanyika kwa nyakati tofauti.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inasisitiza kwamba Wabunge ambao hawajaapishwa ndani ya Bunge ni Wabunge na wanapoteuliwa kushika nafasi ya Uwaziri au Naibu Waziri ni halali kwa kuwa uteuzi huo haukiuki masharti yoyote ya Kikatiba au Sheria. Aidha, katika kutekeleza madaraka ya kazi ya Uwaziri au Naibu Waziri Mbunge atahitaji kiapo mbele ya Rais hata kama hajaapishwa Bungeni. Busara ya uandishi wa Katiba na Sheria imetambua kwamba kunaweza kukatokea uteuzi wa aina hiyo wakati Bunge limeahirishwa kama ilivyo sasa. Masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba yatazingatiwa katika kikao cha Bunge kijacho.

Bila shaka ufafanuzi huu utaleta uelewa katika jambo hili na kuepusha mikangayiko isiyokuwa ya lazima.

Imetolewa na Jaji Frederick M. Werema (Mb)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
06 Mei, 2012
 
Mbona AG pia hajatolea ufafanuzi wa Dk. Mwinyi kupewa Wizara isiyo ya Muungano. Je, napo Rais hajavunja katiba? Mbona hakuna Mtanganyika aliyeshika wizara yoyote Zanzibar?
Ikumbukwe kuwa Raisi aliteua wabunge 3 toka Zanziba i.e Mbarawa,Nahoza na Meghji vilevile Meghli alishawahi kuongoza wizara ambazo si za muungano hapo nyuma i.e Utalii na afya.Nadhani hata mtu wa Zenji anaruhusiwa wizara zingine.
 
Tundulisu hebu pitia hapa umwone huyu jamaa anahalalisha uvunjaji wa sheria za nchi alaf ukamchape fimbo kule Bungeni
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom