Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,199
- 10,713
Maisha yanakwenda kasi sana, huku joto kali sana na bado tunapewa taarifa kuwa kuna El Ninò inakuja, yaani purukushani kibao. Kila mtu anapitia changamoto za maisha kwa namna yake, wapo waliopoteza wapendwa wao, wapo waliofukuzwa kazi na kuna wengine wanaumwa magonjwa, kila mtu ana vita yake ya kupambana.
Ubongo wa binadamu ni wa ajabu sana, ukipata moto sana kuna nyakati utafanya mambo ambayo utajutia kama sio kuanza kuomba mitandao ifute baadhi ya vitu ulivyovifanya.
Sasa kuna post ya bi mdada mmoja ambaye ni single mother kwenye mitandao ya kijamii wa Facebook. Dada kaamka vizuri anaoga zake na kujiandaa kwa ajili ya sherehe ya mtoto wake, akafanya booking ya photoshoot kisha akaipost na kuweka caption ndefu ya makasiriko.
Akapiga picha kadhaa na kuamua kuchagua picha moja ikiwa na ujumbe ambao ni mzito sana.
Picha inamuonesha akiwa amejifunga kanga pekee akiwa anamtazama mwanaye wa kiume wakati wa kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa.
Katika ujumbe huo, bi mdada huyo alimkumbusha mwanaye kuwa alimzaa akiwa mtupu na kumlea kwa shida bila msaada wa mtu yeyote duniani.
Wapo ambao waliona kama ni Ai na kulichukulia tukio hili kama kituko cha kawaida—huku mtoto mwenyewe akionekana kuwaza kutazama tu maungo ya mama yake.
Wataalamu mtanisaidia hapa ila huyu mdada ni kesi bora na ni ishara ya wazi ya msongo mkubwa wa mawazo. Tuna watu ndani ya jamii wanapokabiliwa na magumu katika maisha, mtandao umekuwa uwanja wa kumwaga dukuduku na maumivu ya moyo.
Tusipojali afya ya akili kama jamii basi tunatengeneza bomu kubwa mbeleni, mizigo ya maisha itaendelea kutuvua nguo hadharani! Leo Elizabeth amepiga picha hii na mtoto wake akiwa mtupu, kesho tutasikia mtoto wake amekuwa Uncle Twiiii ila mwisho wa siku maisha binafsi ya mtu ni ya mtu mwenyewe.