FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,881
- 109,192
Afrika: Rais aliye koswa koswa kupinduliwa, kuuliwa mara nyingi ni yupi?
Katika historia ya karibuni ya Afrika, Marais au watawala wengi wameuliwa au kupinduliwa au kukoswa-koswa kuuliwa na kusalimika.
Tanzania pia tulikuwa na kesi kadhaa za matukio ya kutisha kwa viongozi wetu. Kuna tukio la Marehem Mzee Karume kuuliwa kwa risasi (Mwenyezi Mungu amlaze atapoona panamfaa).
Kuna kesi za majaribio kadhaa kwa Marehemu Mzee Nyerere kutaka kupinduliwa (Mwenyezi Mungu amlaze atapoona panamfaa).
Kuna kesi ya mauaji kwa risasi ya Dr. Kleruu alikuwa mkuu wa mkoa wa Iringa wakati wa utawala wa awamu ya kwanza (Mwenyezi Mungu amlaze atapoona panamfaa).
Jee, ni matukio yepi ya kutisha kwa watawala wa Afrika umewahi kuyasikia kisiri au dhahiri.
Sababu zilizopelekea matukio hayo ni zipi? Chuki, dhulma, udhu wa madaraka au ni wazimu tu?