Afrika: Rais aliyekoswa koswa kupinduliwa, kuuliwa mara nyingi ni yupi?

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,820
109,107
Afrika: Rais aliye koswa koswa kupinduliwa, kuuliwa mara nyingi ni yupi?

Katika historia ya karibuni ya Afrika, Marais au watawala wengi wameuliwa au kupinduliwa au kukoswa-koswa kuuliwa na kusalimika.

Tanzania pia tulikuwa na kesi kadhaa za matukio ya kutisha kwa viongozi wetu. Kuna tukio la Marehem Mzee Karume kuuliwa kwa risasi (Mwenyezi Mungu amlaze atapoona panamfaa).

Kuna kesi za majaribio kadhaa kwa Marehemu Mzee Nyerere kutaka kupinduliwa (Mwenyezi Mungu amlaze atapoona panamfaa).

Kuna kesi ya mauaji kwa risasi ya Dr. Kleruu alikuwa mkuu wa mkoa wa Iringa wakati wa utawala wa awamu ya kwanza (Mwenyezi Mungu amlaze atapoona panamfaa).

Jee, ni matukio yepi ya kutisha kwa watawala wa Afrika umewahi kuyasikia kisiri au dhahiri.

Sababu zilizopelekea matukio hayo ni zipi? Chuki, dhulma, udhu wa madaraka au ni wazimu tu?
 
Rais Nyerere alikoswakoswa kupinduliwa nadhani zaidi ya mara 8.

Nadhani huyu ndie anaongoza kwa kukoswa koswa kupinduliwa lakini pia hii inaonyesha jinsi ambavyo walinzi wake walikuwa na uwezo kwa kuzuia mapinduzi mara 8.

Kukoswakoswa mara 8 halafu mpaka ukaamua ''kung'atuka'' baada ya miaka zaidi ya 20 ni kipimo kikubwa cha uwezo wa walinzi wake.

Kuna Marais wengine jaribio la kwanza tu huwaondoa madarakani au kuwaua lakini Rais Nyerere aliweza kuhimili majaribio hayo.
 
Unaweza kutukumbusha ni yalikuwaje? Na yote hayo yaliwekwa wazi au baadhi tu?

Sababu ni zipi? Maana kujaribiwa kupinduliwa mara "nane" kusema kweli si mchezo (kama ni kweli).
 
Back
Top Bottom