Afrika: Rais aliyekoswa koswa kupinduliwa, kuuliwa mara nyingi ni yupi?

Milton Obote nafahamu alipinduliwa na Iddi Amin akahamia Tanzania akiwa mzima.

Rawlings sina matukio yake.
Milton Obote alipinduliwa na Marehemu Nduli Iddi Amini wakati Obote akiwa Kwenye mkutano wa Jumuiya ya Madola huko Malaysia.

Alifanikiwa kurudi kwenye Uraisi kwa Msaada wa Majeshi yetu chini ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Obote alifanyiwa majaribio kadhaa ya kumuua na Yoweri Museveni.

Ndipo akaja kupinduliwa Rasmi na Meja Jenerali Tito Okelo na Jenerali Basilio Okelo
 
Nnalikumbuka tukio moja alikuwa Tanzania na akafanikiwa kurudi (kurudishwa) madarakani.

Sababu ni nini?
Afrika miaka ya 60, 70, 80 na 90 mwanzoni kupindua serikali ilikuwa na kama fashion. Chanzo kikubwa cha mapinduzi ilikuwa ni uroho wa madaraka uliokolezwa na vita baridi kati ya USA na Soviet Union. Wengi wa waliokuwa wanapindua walikuwa wanatoa sababu kuwa watawala wameshindwa kuwaletea maendeleo wananchi kama walivyoahidi lakini hata walipokuwa wanapindua serikali zilizo madarakani wale walioingia walikuwa wanafanya vibaya kuliko hata waliopinduliwa. Hiki kilikuwa ni kipindi cha mpito kikichangiwa na vita baridi kati ya Urusi na washirika wake na Marekani na washirika wake. Baada ya vita baridi matukio ya kupindua nchi yalipungua kwa kiasi kikubwa na mpaka muda huu tulionao ni nadra sana kusikia nchi zinapinduliwa.
 
shida sio utabiri kwenye uzi shida ni wewe kijifanya kujua wakati unatoa habari kwingine na kujifanya zako....acha upuuzi bibi!!
Umelewa?

Natoa habari kwingine wapi? Na uzi uko wazi hapa! Unaota?

Wewe hii mada mzigo kwako, hapa hakuna ubishani wa kibavicha.

Hii mada ni nani anaelewa nini. Hebu pitia mada uone inavyoenda kabla hujazuka na utumbo wako.

Punguani wahed.
 
Afrika miaka ya 60, 70, 80 na 90 mwanzoni kupindua serikali ilikuwa na kama fashion. Chanzo kikubwa cha mapinduzi ilikuwa ni uroho wa madaraka uliokolezwa na vita baridi kati ya USA na Soviet Union. Wengi wa waliokuwa wanapindua walikuwa wanatoa sababu kuwa watawala wameshindwa kuwaletea maendeleo wananchi kama walivyoahidi lakini hata walipokuwa wanapindua serikali zilizo madarakani wale walioingia walikuwa wanafanya vibaya kuliko hata waliopinduliwa. Hiki kilikuwa ni kipindi cha mpito kikichangiwa na vita baridi kati ya Urusi na washirika wake na Marekani na washirika wake. Baada ya vita baridi matukio ya kupindua nchi yalipungua kwa kiasi kikubwa na mpaka muda huu tulionao ni nadra sana kusikia nchi zinapinduliwa.
Tumeona hivi karibuni "mapinduzi" kwa style mpya. Kama vile Libya,

Pia Tumeona "intifada" za Tunisia, Egypt.

Tunashuhudia pia upinzani ukitwaa madaraka kwa kura, hayo pia ni mapinduzi?
 
Mwaka 1979 Luteni Jerry Rawlings akiwa Luteni kwenye Jeshi la Anga la Ghana Alipindua Serikali ya Kijeshi iliyokuwa imeshikwa na Luteni Generali Fred Okufo.

Baada ya Kufanikisha Luteni Rawlings akaikabidhi serikali hiyo kwa Utawala wa Raia na uchaguzi ukafanyika

Luteni Rawlings akarudi Kambini katikati ya Miaka ya 80 Rawlings tena akaipindua Serikali ya Kiraia na jeshi likashika Mamlaka mpaka miaka ya 90 ambapo alistaafu jeshi na kufungua chama cha Siasa na Kushinda uchaguzi wa uraisi.
 
Rais Nyerere alikoswakoswa kupinduliwa nadhani zaidi ya mara 8.

Nadhani huyu ndie anaongoza kwa kukoswa koswa kupinduliwa lakini pia hii inaonyesha jinsi ambavyo walinzi wake walikuwa na uwezo kwa kuzuia mapinduzi mara 8.

Kukoswakoswa mara 8 halafu mpaka ukaamua ''kung'atuka'' baada ya miaka zaidi ya 20 ni kipimo kikubwa cha uwezo wa walinzi wake.

Kuna Marais wengine jaribio la kwanza tu huwaondoa madarakani au kuwaua lakini Rais Nyerere aliweza kuhimili majaribio hayo.
Na wewe toa umbumbumbu,walinzi hawana uwezo wa kuzuia mapinduzi bali idara ya usalama wa taifa.
Walinzi huwa ni watu wa kukabiliana na counter attacks on president.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 1979 Luteni Jerry Rawlings akiwa Luteni kwenye Jeshi la Anga la Ghana Alipindua Serikali ya Kijeshi iliyokuwa imeshikwa na Luteni Generali Fred Okufo.

Baada ya Kufanikisha Luteni Rawlings akaikabidhi serikali hiyo kwa Utawala wa Raia na uchaguzi ukafanyika

Luteni Rawlings akarudi Kambini katikati ya Miaka ya 80 Rawlings tena akaipindua Serikali ya Kiraia na jeshi likashika Mamlaka mpaka miaka ya 90 ambapo alistaafu jeshi na kufungua chama cha Siasa na Kushinda uchaguzi wa uraisi.
Hayo ya yeye kupindua nafahamu. Ulipomtaja juu nilifikiri unaongelea kupinduliwa yeye au kukoswakoswa kuuliwa.
 
Hayo ya yeye kupindua nafahamu. Ulipomtaja juu nilifikiri unaongelea kupinduliwa yeye au kukoswakoswa kuuliwa.
[QUOTE
Uko sahihi dada yangu ila basi nafasi tumuachie Milton Obote, japo hata Peter Mutharika wa Malawi amewahi kudai kuyashtukia majaribio Sita ya kutaka kumuua kuanzia Sumu,Bomu,Mdunguaji Sniper lakini ushahidi wake hauweki wazi....I'll go for Obote.
 
Back
Top Bottom