Afrika Kusini wanayo hoja?

Afrika Kusini wanayo hoja?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,252
Reaction score
16,171
Wamerekani wanajenga ukuta kuzuia wahamiaji, wamewatenga na wazazi wao watoto wa wahamiaji, wamezuia watu kutoka baadhi ya nchi wasiingie Marekani. Ulaya wanazuia wahamiaji wasiingie kwao hadi kusababisha maelfu ya wahamiaji kufa baharini na wengine kusakwa ili kushambiliwa na wananchi kama kule Ufaransa. Wakenya waligomea madaktari wa Tanzania kwenda kufanyakazi za madaktari waliogoma Kwa kudai maslahi yao.

Tanzania tunapambana na wahamiaji haramu kama tunavyofanya Kwa waEthiopia, wachina, waburundi, warwanda kule kwenye mikoa ya pembezoni. Tunawahoji baadhi ya watu ambao mwanzo tulidhani kuwa ni watanzania kama tulivyofanya Kwa Jenerali Ulimwengu, Twaweza, Kabendera, nk. Wananchi tunawalalamikia wachina wanaofanyakazi bila vibali na wanaofanyabiashara ndogondogo za kuuza ice-cream, maua, popcorn, na kufanyakazi bila vibali, etc.

South Africa inasemekana kuwa watu wao 4mil. hawana kazi. Je, Ni wahamiaji wangapi wako South Africa?

Ni wahamiaji wangapi wako South Africa ambao wako South Africa wanafanyakazi na biashara ndogo ambazo zingefanywa na wasouth African wenyewe? Wahamiaji hawa wanasababisha wasouth Africa washindwe kudai maslahi bora kutoka Kwa waajiri wao kwakuwa wahamiaji wako tayari kufanyakazi hata Kwa ujira mdogo saana.
Wahamiaji wengi ndio wanaofanya biashara haramu za madawa ya kulevya, ukahaba na uhalifu mwingine South Africa.

Wahamiaji wanasababisha mifumo ya kutoa huduma kama afya, elimu, maji, usafi, usalama, na makazi kuzidiwa na kusababisha quality kushuka. Wakati haya yote yakitokea viongozi wa South Africa wanashindwa kuchukua hatua Kwa kuogopa na kulindinda michango na jitihada zilizofanywa na nchi nyingine kwenye ukombozi wa South Africa, kulinda uSADC, na kujiona kama kaka mkuu wa nchi zinazoizunguuka south Africa. Hivyo kushindwa kuwazuia au kuwatimua wageni haramu. Walishindwa kuwazuia wageni kufanyakazi biashara au kazi ndogondogo ambazo zinaweza kufanywa na wananchi wao kama vile vinyozi, taxi drivers, mahotelini, mashambani, biashara ndogo ndogo za kuonsha magari na kuuza pipi na maji ya kunywa.

Kwa hili hii wananchi wangefanya nini zaidi ya wanavyofanya?

Je, wanavyofanya Marekani, Ulaya, Msumbiji, Tanzania, nk Kwa wahamiaji haramu ni tofauti Sana na wanachokifanya wasouth Africa?

Kwanini serikali ya South Africa imeshindwa kuwalinda watu wao dhidi ya wahamiaji kama zinavyofanya nchi nyingine Kwa wahamiaji?

Kwanini South Africa ilaumiwe Kwa kile wanachokifanya raia wake?

weny wenyewe?
 
SA wanayo haki kabisa ya kuzuia wazamiaji kujaa kiholela huko kwako, lakini si kwa njia hii wanayotumia wazulu. kuua na kupora mali za watu. tatizo ndio liko hapo. mchi zoote ulizotaja hakuna mfumo usiofuata sheria kuzuia wahamiaji haramu kama inavyofanyika sasa hivi SA. Marekani Trump kafikishwa mahakamani kuzuia sera zake za kuzuia wahamiaji. wewe leo jaribu kumvamia mrundi, mchina umuue na kupora mali zake pale kariakoo uone kama hutaozea jela.Ndiyo wazuie kabisa wahamiaji haramu na halali lakini kwa kufuata sheria na haki!
 
Sijui ni kweli?
IMG-20190908-WA0001.jpeg
 
Ndiyo maana watu wanajichukulia sheria mikononi mwao kwakuwa serikali yao imeshindwa kuwatetea, imeshindwa kukabiliana na wahamiaji hao Kwa visingizio vya kisiasa na historia.

Hata hapa Tanzania tunao wanachi wenye hasira kali ambao hawaozei jela kama unavyosema wewe. Kama serikali haichukui haichukui hatua wanachi hawawezi kukaa kimya.
 
Tatizo siyo wahamiaji, tatizo ni serikali yao.

Sasa basi Kama raia hawawezi
kuwaweka madarakani viongozi wengine wenye fikra mbadala basi wawe wanawachoma na kuwapiga maofisa wao wa serikali siyo wahamiaji labda wataelewa na kuchukua hatua.

Maana vurugu dhidi ya wahamiaji hazijaanza leo na hazijaonesha kuwa suluhisho.
 
hivi tukiangalia kwa undani kabisa, inawezekenaje mgeni akaja akafanikiwa kupitia umachinga,carwash,kiosk,kinyozi na wewe mzawa upo?!? ulishindwa kuziona hizo fursa?!? au kama ndio unaziona sasa unashindwaje kuanzisha shughuli hizo ili ushindane sokoni?!? halafu tumia uzawa wako kupitisha sheria zitakazo kupendelea wewe mzawa si wapo akina MALEMA?!?
 
nyie wateteeni tuu as if hakuna wa SA wanaoishi nigeria au kuwekeza nchi nyingine....
unafkiri hawawezi kupambana ona sasa mmepoteza ndege teari
mnaishi ka mbayuway kwe nchi zatu kisa utahira wenu et wamachinga na wafanya usafi maofisini wanawanyanganya kazi

Haki yanan nyie ni MAPOPOMPO kishenzi yan
 
Wazawa kutoziona fursa haihalalidhi wahamiaji haramu kuja kuziona na kuzitumia fursa bila utaratibu. Mbona hata Sisi tunawalalamikia wanyasa kufanya kazi za ndani, wakenya kufanyakazi za mahotelini na uwalimu, wachina kuuza maua kariakoo, wageni kuchimba na kununua madini, kwani wazawa hawazioni fursa hizo?

Hata baba wa aliwakataza wageni kuchimba madini Kwa hasara nakusema hayaozi tutayachimba muda utakapofika.

Tuache utani, wageni ni kero South Africa, vijana wetu walienda huko Kwa kutoroka na kuzamia hata Sisi wazazi tunalofahamu hilo lakini tumekaa kimya. Historia ya kutokomeza apartheid na utengamano umekuwa mwiba Kwa wasouth Africa. Mandela alitaka kulipa fadhila Kwa nchi zilizoshirikiana nazo kuwashinda makaburu. Mbona Sisi tumekomboa Msumbiji lakini watu wetu wanafurushwa huko kila siku? Nusu ya vijana wa Zimbabwe wako South Africa, Malawi, Gambia, Burundi, Zambia, Msumbiji, Tanzania ndo usiseme kabisa.
 
Tatizo siyo wahamiaji, tatizo ni serikali yao.

Sasa basi Kama hawawezi
kuwaweka madarakani viongozi wengine wenye fikra mbadala basi wawe wanawachoma na kuwapiga maofisa wao wa serikali siyo wahamiaji labda wataelewa na kuchukua hatua.

Maana vurugu dhidi ya wahamiaji hazijaanza leo na hazijaonesha kuwa suluhisho.
Mbona Sisi tuliwafurusha wahamiaji na mifugo Yao? Kwahiyo viongozi wa South Africa lazima ipige deki ya wahamiaji haramu wote warudi kwao, pili wageni wasifanye lazi ndogo zinazoweza kufanywa na wazawa, wabakie wale wanaohitajika Tu. Sio kubakisha mtu anayeuza soda, pampas, na sigara eti wana maduka.
 
nyie wateteeni tuu as if hakuna wa SA wanaoishi nigeria au kuwekeza nchi nyingine....
unafkiri hawawezi kupambana ona sasa mmepoteza ndege teari
mnaishi ka mbayuway kwe nchi zatu kisa utahira wenu et wamachinga na wafanya usafi maofisini wanawanyanganya kazi

Haki yanan nyie ni MAPOPOMPO kishenzi yan
Kaka wanaofukuzwa kule sio wageni wenye utaalumu unahitajika kule wala wawekezaji wa maana. Bali ni watu waliokimbia ukandamizaji kwenye nchi zao. Ni watu ambao wameshindwa kubadili mambo kwenye mataifa Yao, ni watu ambao kura zao kwenye box la kura haziheshimiwi.
 
Viongozi wa ANC ni ajabu sana, yaani eti wamekosa solution ya hilo tatizo au wanalilea kwa manufaa yao.
 
Kaka wanaofukuzwa kule sio wageni wenye utaalumu unahitajika kule wala wawekezaji wa maana. Bali ni watu waliokimbia ukandamizaji kwenye nchi zao. Ni watu ambao wameshindwa kubadili mambo kwenye mataifa Yao, ni watu ambao kura zao kwenye box la kura haziheshimiwi.
sasa niambie hao wanyonge waibaje kazi za wazawa?
 
Back
Top Bottom