Huu mkwara mzito,acha kabisa. Kama ni wa kweli lazimaserikali itoe tamko.Sijui ni kweli?View attachment 1201337
Kwanini South Africa ilaumiwe Kwa kile wanachokifanya raia wake?
Duh mkuu uvivu wa wazulu hauhalalishi watu kuivamia nchi Yao, hata kama ni wavivu haituhusu. Tanzania ni nchi yenye utajili mkubwa Sana, tunayo ardhi kubwa Sana ya kilimo, ufugaji na uvuaji lakini vijana hawataki kulima wanafanya umachinga mijini. Lakini pamojana ardhi kubwa tuliyonayo haihalalishi wageni kuja kwetu kujimegea ardhi yetu kiholela.
Viongozi wetu wamekosa vision. Hata Tanzania hawa machinga ni bomu linalotokota, hizi mbinu zinazotumika sasa hivi za kuwatuliza Kwa kuwapa vitambulisho vya 20,000 na kuwaruhusu wafanye biashara popote pale ispokuwa Ikulu ni za muda Tu. Iko siku watachukuwa njia itakayowaudhi watu wengi kabisa.Kosa kubwa lilifanywa na serikali ya SA kutoa resident permits kwa machinga na watu wengine wa aina hiyo. Na kama hawana permits imekuaje wameachwa hadi wamerundikana mitaani? Hakuna nchi duniani wanaotoa residents permits kwa kazi za umachinga, kwanza machinga halipi kodi wala hatoi ajira kwa mzawa, sasa mtu wa hivi unamruhusu vipi aishi nchini mwako? Nchi makini zinatoa permit kwa watu wenye mitaji mikubwa ambao watalipa kodi na kutoa ajira kwa wenyeji pamoja na professionals ambao wataleta faida kwa nchi na sio mizigo
Aaaah, mkuu hapo sio sawa kusema SA hawana sheria ya kuzuia wahamiaji. Unamaanisha kuwa kwenda South Africa huhitaji kuwa na passport wala visa.Mkuu, hoja yako umeijenga juu ya misingi haramu.
Kinachofanyika South Afrika (SA) ni uhalifu, yaani Wahamiaji Haramu na halali wote wanapigwa na kunyang'anywa mali zao, wanafanyiwa hivyo na Raia (wahalifu) wa SA bila kuungwa mkono na Serikali yao.
Ingekuwa kwamba wahalifu hao wamepata sapoti kutoka katika serikali yao hapo bandiko lako lingekuwa a mashiko.
Mifano uliyonukuu kutoka katika hizo nchi kuunga mkono kinachofanywa huko SA, sio sahihi kwani mambo yanayofanyika katika hizo nchi pamwe na TZ, kuhusu wahamiaji ni mambo ya "KISHERIA"--- ni tofauti na kile kinachofanyika SA.
Inatakiwa serikali ya SA itunge sheria ya kudhibiti Uhamiaji, hapo ndipo tutaweza kuishutumu au kuiunga mkono Serikali ya SA, lakini hatuwezi kuunga mkono uhalifu wanaofanyiwa wahamiaji. Ni bora serikali ya SA iseme wazi kwamba Wahamiaji hawatakiwai hapo ndipo tutapima.
Una shida kwenye kufananisha matukio. Duniani kote hakuna serikalini yenye viongozi weledi inayiweza kuua raia wake kiholela ili kumsalimisha mgeni. Raia ana thamani kubwa kuliko mhamiaji. Israel ukiua mwiisrael mmoja ataua wahamiaji 100. Pili, hakuna jeshi linaloweza kuishinda nguvu ya umma. Tatu, Kama askali akimkinga mhamiaji raia wataanzia kwake kwanza kisha mhamiaji. Nne, hakuna kiongozi wa ANC ambaye atapenda kukosa kura eti kwasababu ya kutetea wahamiaji. SA ilishindwa kumkemea Mugabe alipokuwa akiwanyang'anya wazungu mashamba Kwa kuhofia kurufushwa na wananchi wao, maana hata SA kuna tatizo la ardhi pia kama Zimbabwe.Uzi umeandikwa kihuni mno.
Ni nyuzi kama hizi hua mahsusi kuchochea ujinga vichwani.
Kwamba uzi hautambui tofauti ya uhamiaji na uhamiaji haramu?
Kwamba uzi hautambui haki ya kuishi ni ya wote.
Kwamba uzi unaona kua namna pekee ya kushughulika na wagenj nk kwa raia kushambulia, kupora na kuua. Na siyo vyombo husika vifanye kazi yake.
Kuna mwaka Tz tulifukuzana na wanyasa na wacongo lakini tuliona askari walivyokamata watu waliopora vitu vya wageni. SA hakuna hilo.
Tukiambiwa Africans hatuna akili, tuangalie yanayotokea SA kisha tukumbuke kuna watu wanaunga mkono mpaka wameanzisha uzj.
Aaaah, mkuu hapo sio sawa kusema SA hawana sheria ya kuzuia wahamiaji. Unamaanisha kuwa kwenda South Africa huhitaji kuwa na passport wala visa.
Ukweli ni kwamba wahamiaji wanaingia SA Kwa njia haramu. Ni ngumu Sana kuwadhibiti watu hao ndio maana America pamoja na nguvu na technology walionayo lakini wanajenga ukuta kuzuia wahamiaji. Ulaya suala la wahamiaji limeangusha wanasiasa wengi.
Trump alipata kura nyingi kutoka Kwa wananchi wasiopenda wahamiaji.
Kama viongozi wa SA hawanyi kitu wacha wananchi wafanye kitu wanachoweza kwa manufaa Yao, kila mtu arudi kwao akawahimize wanasiasa wao waboresha hali ya mambo kwao.
Siasa mbovu zinasababisha wakimbizi kwenye mataifa mengine.
Saaawa. Kamata mchukulie sheria...mrudishe basi. Lkn eti kumchoma moto?? Ya wapi hyo?Wazawa kutoziona fursa haihalalidhi wahamiaji haramu kuja kuziona na kuzitumia fursa bila utaratibu. Mbona hata Sisi tunawalalamikia wanyasa kufanya kazi za ndani, wakenya kufanyakazi za mahotelini na uwalimu, wachina kuuza maua kariakoo, wageni kuchimba na kununua madini, kwani wazawa hawazioni fursa hizo?
Hata baba wa aliwakataza wageni kuchimba madini Kwa hasara nakusema hayaozi tutayachimba muda utakapofika.
Tuache utani, wageni ni kero South Africa, vijana wetu walienda huko Kwa kutoroka na kuzamia hata Sisi wazazi tunalofahamu hilo lakini tumekaa kimya. Historia ya kutokomeza apartheid na utengamano umekuwa mwiba Kwa wasouth Africa. Mandela alitaka kulipa fadhila Kwa nchi zilizoshirikiana nazo kuwashinda makaburu. Mbona Sisi tumekomboa Msumbiji lakini watu wetu wanafurushwa huko kila siku? Nusu ya vijana wa Zimbabwe wako South Africa, Malawi, Gambia, Burundi, Zambia, Msumbiji, Tanzania ndo usiseme kabisa.
Huko kwenye mashamba sasa wamejaa hata watanzania wanaofanyakazi hata Kwa bei ya kutupa. Hii inawaudhi wasauzi kwakuwa hawezi sasa kugoma kama walivyozoea kupitia COSATU kuwambana wazungu wawaongeze mishahara ya kuchuma apples.tatizo toka enzi za apartheid, waafrika kusini wengi walikuwa vibarua kwenye makampuni na mashamba ya wazungu, biashara ndogo ndogo zilikuwa zinafanywa na wageni kutoka zimbabwe, mozambique, ethiopha , asians, wazulu hawakuona tatizo sana shida sasa hivi ajira kwenye makampuni ya wazungu hamna hapo ndio wanapowageukia wageni
Una shida kwenye kufananisha matukio. Duniani kote hakuna serikalini yenye viongozi weledi inayiweza kuua raia wake kiholela ili kumsalimisha mgeni. Raia ana thamani kubwa kuliko mhamiaji. Israel ukiua mwiisrael mmoja ataua wahamiaji 100. Pili, hakuna jeshi linaloweza kuishinda nguvu ya umma. Tatu, Kama askali akimkinga mhamiaji raia wataanzia kwake kwanza kisha mhamiaji. Nne, hakuna kiongozi wa ANC ambaye atapenda kukosa kura eti kwasababu ya kutetea wahamiaji. SA ilishindwa kumkemea Mugabe alipokuwa akiwanyang'anya wazungu mashamba Kwa kuhofia kurufushwa na wananchi wao, maana hata SA kuna tatizo la ardhi pia kama Zimbabwe.
Usiwafananishe watanzania na wakenya, wasouth Africa, wasomali, warwanda, nk. Watanzania ni waoga kama kunguru ukiwaonya wanaonyeka lakini wazulu ni wagumu Sana waliokata tamaa wasiokuwa na chakupoteza.
KWA taarifa yako, kupata resident permit nchini Afrika Kusini ni ngumu sana, tena sana.Vile vile kumbuka, hata watoto wa RAIA wa kigeni wanaozaliwa Afrika Kusini hawapewi vyeti vya kuzaliwa, wanaandikiwa tu vikaratasi KWA peni,vikatasi vya madaftari au vya ream paper, nesi au daktari anaandika KWA mkono.Kosa kubwa lilifanywa na serikali ya SA kutoa resident permits kwa machinga na watu wengine wa aina hiyo. Na kama hawana permits imekuaje wameachwa hadi wamerundikana mitaani? Hakuna nchi duniani wanaotoa residents permits kwa kazi za umachinga, kwanza machinga halipi kodi wala hatoi ajira kwa mzawa, sasa mtu wa hivi unamruhusu vipi aishi nchini mwako? Nchi makini zinatoa permit kwa watu wenye mitaji mikubwa ambao watalipa kodi na kutoa ajira kwa wenyeji pamoja na professionals ambao wataleta faida kwa nchi na sio mizigo
Mleta ni UVCCM amejawa na ubaguzi kichwaniSA wanayo haki kabisa ya kuzuia wazamiaji kujaa kiholela huko kwako, lakini si kwa njia hii wanayotumia wazulu. kuua na kupora mali za watu. tatizo ndio liko hapo. mchi zoote ulizotaja hakuna mfumo usiofuata sheria kuzuia wahamiaji haramu kama inavyofanyika sasa hivi SA. Marekani Trump kafikishwa mahakamani kuzuia sera zake za kuzuia wahamiaji. wewe leo jaribu kumvamia mrundi, mchina umuue na kupora mali zake pale kariakoo uone kama hutaozea jela.Ndiyo wazuie kabisa wahamiaji haramu na halali lakini kwa kufuata sheria na haki!