Wamerekani wanajenga ukuta kuzuia wahamiaji, wamewatenga na wazazi wao watoto wa wahamiaji, wamezuia watu kutoka baadhi ya nchi wasiingie Marekani. Ulaya wanazuia wahamiaji wasiingie kwao hadi kusababisha maelfu ya wahamiaji kufa baharini na wengine kusakwa ili kushambiliwa na wananchi kama kule Ufaransa. Wakenya waligomea madaktari wa Tanzania kwenda kufanyakazi za madaktari waliogoma Kwa kudai maslahi yao.
Tanzania tunapambana na wahamiaji haramu kama tunavyofanya Kwa waEthiopia, wachina, waburundi, warwanda kule kwenye mikoa ya pembezoni. Tunawahoji baadhi ya watu ambao mwanzo tulidhani kuwa ni watanzania kama tulivyofanya Kwa Jenerali Ulimwengu, Twaweza, Kabendera, nk. Wananchi tunawalalamikia wachina wanaofanyakazi bila vibali na wanaofanyabiashara ndogondogo za kuuza ice-cream, maua, popcorn, na kufanyakazi bila vibali, etc.
South Africa inasemekana kuwa watu wao 4mil. hawana kazi. Je, Ni wahamiaji wangapi wako South Africa?
Ni wahamiaji wangapi wako South Africa ambao wako South Africa wanafanyakazi na biashara ndogo ambazo zingefanywa na wasouth African wenyewe? Wahamiaji hawa wanasababisha wasouth Africa washindwe kudai maslahi bora kutoka Kwa waajiri wao kwakuwa wahamiaji wako tayari kufanyakazi hata Kwa ujira mdogo saana.
Wahamiaji wengi ndio wanaofanya biashara haramu za madawa ya kulevya, ukahaba na uhalifu mwingine South Africa.
Wahamiaji wanasababisha mifumo ya kutoa huduma kama afya, elimu, maji, usafi, usalama, na makazi kuzidiwa na kusababisha quality kushuka. Wakati haya yote yakitokea viongozi wa South Africa wanashindwa kuchukua hatua Kwa kuogopa na kulindinda michango na jitihada zilizofanywa na nchi nyingine kwenye ukombozi wa South Africa, kulinda uSADC, na kujiona kama kaka mkuu wa nchi zinazoizunguuka south Africa. Hivyo kushindwa kuwazuia au kuwatimua wageni haramu. Walishindwa kuwazuia wageni kufanyakazi biashara au kazi ndogondogo ambazo zinaweza kufanywa na wananchi wao kama vile vinyozi, taxi drivers, mahotelini, mashambani, biashara ndogo ndogo za kuonsha magari na kuuza pipi na maji ya kunywa.
Kwa hili hii wananchi wangefanya nini zaidi ya wanavyofanya?
Je, wanavyofanya Marekani, Ulaya, Msumbiji, Tanzania, nk Kwa wahamiaji haramu ni tofauti Sana na wanachokifanya wasouth Africa?
Kwanini serikali ya South Africa imeshindwa kuwalinda watu wao dhidi ya wahamiaji kama zinavyofanya nchi nyingine Kwa wahamiaji?
Kwanini South Africa ilaumiwe Kwa kile wanachokifanya raia wake?
weny wenyewe?