Afrika Kusini na ubaguzi wa rangi, picha hii yazua taharuki


Kingsmann

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Messages
228
Likes
423
Points
80
Kingsmann

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2018
228 423 80
Mama wa mtoto katika shule ya awali ya Laerskool Schweizer-Reneke iliyopo katika jimbo la North West huko Afrika Kusini, amechukizwa vikali baada ya picha inayomuonesha mtoto wake wa kike na watoto wengine watatu wa Kiafrika wakiwa wamekaa peke yao mbali na watoto wengine wa kizungu kwenye darasa lao. Picha hiyo ambayo inasambaa kwa kasi mtandaoni, imesababisha hasira kubwa kwa raia wa nchi hiyo kutokana na kuwa na ishara ya ubaguzi wa rangi.

Picha hiyo ilitumwa kwenye kundi la WhatsApp la shule hiyo na mwalimu wa darasa. "Hii ilipaswa kuwa siku ya kufurahisha kwangu lakini sio,” amesema mzazi huyo. Mama huyo ambaye hakutajwa jina kulinda utambulisho wa mwanae, ameiambia tovuti ya TimesLIVE ya nchini humo kuwa siku ya kwanza katika darasa hilo ilianza vizuri.

Yeye na wazazi wengine waliwapeleka watoto wao na kuambiwa waondoke katika eneo la shule. Saa tatu asubuhi walitumiwa taarifa kutoka kwa mwalimu wa watoto hao kuhusu siku ilivyokwenda kupitia WhatsApp group. Picha hiyo ilionesha watoto 18 wa kizungu wakiwa darasani wamekaa dawati moja lililounganishwa katikati ya darasa, wakati watoto wanne wa Kiafrika wakiwa wamekaa kwenye dawati moja lililowekwa kwenye kona ya darasa hilo. "Nilichoona ni jumbe toka kwa wazazi wa kizungu wakisema asante asante kwenye WhatsApp group, lakini hakuna yeyote aliyesema kuhusu walivyotenganishwa,” alisema mzazi huyo.

Amesema baada ya kujadiliana na mzazi mwingine nje ya WhatsApp group, mzazi huyo aliwasiliana na mkuu wa shule kuuliza kuhusu ukaaji wa watoto hao darasani. TimesLIVE imedai mkuu huyo wa shule alisema hakuwa na taarifa za suala hilo. Wamedai kuwa wanasubiri jibu toka kwa shule hiyo.

Alipoulizwa kuhusu anavyojisikia kutokana na hali hiyo, mama huyo amesema ana matumaini kuwa mwanae mwenye umri wa miaka mitano bado ni mdogo kuweza kutambua kilichotokea.
"Lakini nimechukia,” alisema mama huyo aliyeahidi kuchukua hatua zaidi.

Source: Bongo5
skytanzania-20190109-0001-jpeg.990332
 
Hawachi

Hawachi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2018
Messages
1,001
Likes
1,239
Points
280
Age
26
Hawachi

Hawachi

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2018
1,001 1,239 280
Hasa zamani wanawake wa kiafrika waliolewa lakin sahv si dhan

Sent using Jamii Forums mobile app
Walio olewa huko ni watumwa ambao walichukuliwa Zanzibar kipindi cha Sultan Said baba yake Sultan Qabuus wa Sasa Hapo Oman baada ya kukaa yeye madalakani ndipo ikatungwa hiyo sheria nikupe mfano :Mascat Kuna Wanzazibar wengi wanaongea kiswahili vizuri tu hao wanaluhusiwa kuoa/kuolewa why kwa sababu passport zao sio za Tanzania yaani wanajulikana ni waarabu. Watumwa walio pelekwa huko zamani.
 
R

ruaharuaha

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2018
Messages
846
Likes
643
Points
180
R

ruaharuaha

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2018
846 643 180
Inasikitisha sana...

Wao wanatudharau, sisi tunawanyenyekea kabisa...


Cc: mahondaw

Ndio tatizo Mwafrika was leo, hajiamini. Anafikiri mzungu ni Superior, na yeye inferior, wale ni binadamu kama sisi tofauti wamefundishwa, wanafundishwa kujiamini.

Shuleni wanajifunza kwamba wao wametawala, wamevumbua karibu kila kitu, Sisi tunakariri Livingstone alifanya hivi na ujinga mwingine mwingi.
 
M

mangatara

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2012
Messages
11,980
Likes
8,068
Points
280
M

mangatara

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2012
11,980 8,068 280
Natamani hii picha itufundishe sisi tunaobaguana kiitikadi, kichama na kimkoa na kikanda. Huu uchungu uliouona wewe ndivyo huwa tunajina sisi unavyotupima kikanda au kikabila unapogawa keki yetu kwa kelele kuwa huna chama.
 
kamwendo

kamwendo

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Messages
505
Likes
499
Points
80
kamwendo

kamwendo

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2012
505 499 80
Ninataka tu kumjua mwalimu wa darasa kabla sijachangia.

Ila hii picha inaumiza kwakweli.
 
lhera

lhera

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2018
Messages
527
Likes
655
Points
180
lhera

lhera

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2018
527 655 180
Walio olewa huko ni watumwa ambao walichukuliwa Zanzibar kipindi cha Sultan Said baba yake Sultan Qabuus wa Sasa Hapo Oman baada ya kukaa yeye madalakani ndipo ikatungwa hiyo sheria nikupe mfano :Mascat Kuna Wanzazibar wengi wanaongea kiswahili vizuri tu hao wanaluhusiwa kuoa/kuolewa why kwa sababu passport zao sio za Tanzania yaani wanajulikana ni waarabu. Watumwa walio pelekwa huko zamani.
Ni kweli kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
stroke

stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Messages
16,555
Likes
9,603
Points
280
stroke

stroke

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2012
16,555 9,603 280
Wazungu hatari sana hawa watu wanapandikiza chuki toka utoto : unashangaa kwanini ubaguzi hauishi.
 
R

ruaharuaha

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2018
Messages
846
Likes
643
Points
180
R

ruaharuaha

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2018
846 643 180
Wazungu hatari sana hawa watu wanapandikiza chuki toka utoto : unashangaa kwanini ubaguzi hauishi.
Sio wote mfano USA, UK, France huwezi kufanya hivi, utafunguliwa kesi, kufukuzwa kazi. Your reputation will be in tatters.

Ukweli ni kwamba Wazungu was SA bado wanamiliki kwa asilimia kubwa kila kitu muhimu SA. Ardhi, madini, big businesses.

Solution ingekuwa Kwa Wasauzi weusi kuheshimu elimu, kusoma, ili hata wakipewa ardhi, biashara waweze kutumia hizo nafasi vizuri. Ila hawapendi elimu, kujiongeza.

Serikali yao iwe na sera za maana kuwasaidia watu wao.
 
D

dos.2020

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2009
Messages
1,524
Likes
811
Points
280
D

dos.2020

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2009
1,524 811 280
Watu weusi ni watu wa ajabu sana, Hivi hili nalo limekua ishu? kzi kushuhulika namambo yasiyo na msingi tu.
 
R

ruaharuaha

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2018
Messages
846
Likes
643
Points
180
R

ruaharuaha

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2018
846 643 180
Watu weusi ni watu wa ajabu sana, Hivi hili nalo limekua ishu? kzi kushuhulika namambo yasiyo na msingi tu.
Ni issue gani kubwa zaidi ya hii? tuambie, hapa unazungumzia elimu, mfumo, matabaka, ubaguzi, future of a country, future prospect of blacks kwenye nchi yao. Mustakabali wa nchi.
 
Machozi ya Simba

Machozi ya Simba

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Messages
2,437
Likes
1,311
Points
280
Machozi ya Simba

Machozi ya Simba

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2012
2,437 1,311 280
Kwa hii picha nmesikitika sana kujua kwamba kuna baadhi za shule zina itikadi za kibaguzi hadi sasa, unaweza kujisifia umempeleka mtoto wako shule nzuri ya milioni 30 kwa mwaka ambayo ina watoto wa kizungu kibao ila yanayoendelea huko ukija kuyajua kwa hakika utahamisha mtoto ajichanganye na waafrika wenzae shule za kata.

ubaguzi-jpeg.991535
 
Dalmine

Dalmine

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2016
Messages
2,288
Likes
1,484
Points
280
Dalmine

Dalmine

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2016
2,288 1,484 280
Yote mawili Mkuu!! Jee wewe ni mwendawazimu, mpumbavu au hayawani? Wazee wa wengine lazima walaumiwe kwa kutowafunza watoto wao adabu!! Inaelekea wewe ni mndundu. Mungu akusaidie, inshaa Llaah
Tatizo la hawa viumbe hawana kauli nzuri, kuna mmoja hapo juu kanitusia mama yangu tusi baya sana. Hawa watu wa ajabu sana mkuu, cjui ndivyo wanafundishwa kule kanisani.
 
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
15,023
Likes
12,851
Points
280
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
15,023 12,851 280
Sikilizeni Speech za Julius Malema na Uchochezi wake,Waafrika pia tuna Ubaguzi wa hali ya juu kabisa tumewaua Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa kati Millioni Mbili.
 

Forum statistics

Threads 1,250,095
Members 481,224
Posts 29,720,580